Mu7
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 1,624
- 1,934
Ndugu yangu alifariki baada ya kusumbuliwa na malaria na shinikizo la damu kwa muda mfupi. Daktari alithibitisha kuwa amefariki dunia na akaandika death certificate. Lakini cha kushangaza, wakati wa kuagwa na ndugu na marafiki nyumbani kwake,
Marehemu alikuwa anatokwa jasho usoni. Hii maana yake nini wajuzi ?
Marehemu alikuwa anatokwa jasho usoni. Hii maana yake nini wajuzi ?
Mkuu hii mada uliyoleta ni very interesting!
Swali la kwanza la kujiuliza je kifo ni nini?
Bado hakuna definition iliyonyooka na kuridhisha kwa makundi yote ya kijamii.
Kifo ni nini basi....
Ni kuondokewa kwa uhai wa kile kilichokuwa kinaishi.
Kisayansi kifo sio tukio la ghafla bali ni safari ya kuondokewa kwa uhai.seli na tishu mbalimbali za mwili hupoteza uwezo wake wa kufanya kazi au kuishi katika spidi mbalimbali.
Hapa kuna utata unaotokea kuhusu ni wakati gani hasa kifo hutokea?
Na kupelekea kuwe na aina mbili za kifo
1-Kifo cha selihai(cellular level)
Hapa seli na tishu zinapoteza uwezo wa kufanya kazi ama kuishi na hivyo kushindwa kutumia oksijeni na hatimaye zinaanza kujivunjavunja na kuoza.ikiwa jambo hili litahusisha seli za mwili mzima basi hiki ni kifo.
selihai hufanya kazi tofauti na spidi ya kufa huwa tofauti labda kwenye tukio ambalo litaharibu seli zote kwa wakati mmoja kwa mfano mlipuko wa nyuklia.
selihai za ngozi au mifupa huweza kuishi masaa mengi kulinganisha na selihai za ubongo zinazochukua madakika tu baada ya mtu kuonekana "amekufa"
2-Kifo cha kimwili(somatic death)
Hapa mwili unapoteza uweza wa kuwasiliana na mazingira na pia unakuwa haujitambui na kupoteza sifa za uhai.
Hivyo kwa ufupi kumjibu mleta mada ni kuwa ni kweli inawezekana kuwa ndugu yako alikuwa yuko kwenye process ya kifo na hivyo kumuona akiendelea kutoka jasho(sisemi mlimzika akiwa hai)
Cha msingi ninachokiona ni kwamba daktari,ndugu,jamaa na marafiki wakikubali kuwa mtu huyu amefariki basi hakuna wa kupinga.
Nadhani nitakuwa nimekufungua kidogo kuhusu possibility ya kuona jasho au hata movement kwa mtu aliyehesabika 'amekufa'
Kwa hisani ya vitabu mbalimbali.