John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Kijana Payton Gendron, 18, ambaye aliwaua watu 13 kwa kuwafyatulia risasi, 10 kati yao wakiwa wenye rangi nyeusi inaelezwa alipanga kufanya mauaji zaidi kama angetoroka eneo la tukio Jijini New York, Marekani.
Kamishna wa Polisi, Joseph Gramaglia amesema: “Alitaka kwenda kwenye gari alekee Jefferson Avenue ili kuendelea kufyatua risasi kama alivyofanya eneo la Buffalo."
Inaelezwa FBI wamelazimika kuingilia kati kuchunguza tukio hilo linalodaiwa kutokana na chuki dhidi ya Watu Weusi aliyokuwa nayo kijana huyo.
Rais wa Marekani, Joe Biden na mkewe, Jill Biden wanatarajiwa kutembelea eneo hilo la tukio leo Mei 17, 2022.
Source: CNN