Marekani ana nini? Ameipiga ban Iranian Airlines, na nchi zote zimefuata maelekezo

😁😁😁
Watakaokuwepo hai mwaka 3000 huko watajivunia Tanzania ya Superpower πŸ€ͺ

Japo Sina uhakika hata kufikia Uchumi wa kati kama tutakuwa tumefika, maana saivi tumerudi Uchumi wa chini chini kabisa
 
Vip akija kma wakoloni
 
Vip akija kma wakoloni
Mkuu kama huoni sasahivi tunatawaliwa kuliko hata enzi za ukoloni?
Rasilimali zote wanabeba wao kuanzia huko geita mpaka chunya,
Bei za bidhaa wanapanga wao, mifumo yote tunayotumia ni ya kwao
Grants na mikopo yote huwa ni kwa ajili ya miradi yao ambayo wanajua inafadhili maslahi yao and not otherwise

Na ndio maana hawaangaiki na serikali za afrika hata ziwe dictator kiasi gani, wao wataangaika na wewe kama umeminya maslahi yao mfano mzuri ni gadafi
 
Ataangukaje wakati kampiga China gap ya $12T iyo Gap ni uchumi wa German,France and UK combined
Kwa Sasa uchumi wa Marekani unategemea mafuta ya mashariki ya kati kuuzwa US $
Siku waarabu wakijaniaruka na kuikataa US $ katika biashara Yao ya mafuta Marekani atakuwa kama joka la kibisa
 
Kwa Sasa uchumi wa Marekani unategemea mafuta ya mashariki ya kati kuuzwa US $
Siku waarabu wakijaniaruka na kuikataa US $ katika biashara Yao ya mafuta Marekani atakuwa kama joka la kibisa
Waarabu ni watu wanafiki sana mkuuu hawawezi hata kufukilia kesho wao ni wavivu na kupenda kujipendekeza sana hapo jamaaaa mkuu
 
Sio nchi zote mkuu usipende kudanganya. Nchi zilizotii hadi sasa ni Uturuki na baadhi ya gulf nations. Ila sio zote. China,Urusi,Armenia wote wamekataa kutii hilo agizo. Iraq nao wamekataa japo kuna majadiliano ya kubadili flight destinations.
Hii ni kawaida ya mipumbavu ya JF
Huwa inajilopokea Kama iko kwenye kilabu cha pombe huko vijijini
 
Unauliza swali ambalo unajua majibu yake,ni kweli kwamba hujui nguvu ya Marekani kwenye hii dunia...?
 
Ukisema Marekani inajifia au kufirisika kuna matendo lazima yaambatane nayo ❗️

Au kusema Tajiri yule kwasasa anafirisika nayeye kuna matendo yatakuwa ni mapya ayo matendo ndio yanatoa ishara ❗️

Sasa Marekani matendo yake hatuwezi kusema
kwasasa ni Ubabe
Hapana πŸ‘ˆ

Kwasasa yupo kwenye kudondoka
Ndiomana Vikwazo vyake
vyasasa vinatoa picha uyu kwasasa kachanganyikiwa

Shirika la ndege la Air Iranian
linanini kwake vikwazo kama ivyo vinaipa nini Marekani ‼️

Shirika lile ni dogo sana ❗️unataka liwekewe mipaka
Ni wazi nchi ndogo ndizo
zitaumia βœ…οΈ
 
Biashara ya kimataifa kwa kiasi kikubwa inatumia dola ya Marekani na mitandao ya Marekani. Mfano, biashara ya mafuta kwa kiasi kikubwa inatunia dola ya Marekani, settlement system ya Marekani, malipo yanafanyiwa settlement hapo lower Manhattan Federal Reserve New York branch.

Hata hapa JF usishangae ikiwa traffic inapitia Marekani.

Ukitumia mfumo wa kibenki wa malipo wa SWIFT tu, umetumia mifumo ya Kimarekani. Ukitumia Visa, Mastercard, American Express, Discover, etc, yote hiyo ni mifumo ya Marekani.

Zaidi, uchumi wa Marekani ni mkubwa sana duniani. Vikwazo maana yake ni kwamba kampuni za Kimarekani haziruhusiwi kufanya biashara na wewe, mtu yeyote aliye Marekani au raia wa Marekani haruhusiwi kufanya biashara na wewe.

Maana yake mashirika yote ya ndege yenye ndege za Kimarekani kama Boeing yakienda Iran yatashindwa kufanya kazi kama za maintenance na Boeing, yatashindwa kwenda Marekani, yatashindwa kusafirisha Wamarekani. Yatashindwa kuwekeza katika masoko ya hisa ya Marekani. Yatashindwa kupata bima za makampuni ya bima ya Marekani. Yatashindwa kupata mikopo ya mabenki ya Marekani.

Ndege za Iran zitashindwa kujaza mafuta nje ya Iran kwenye nchi yoyote inayofanya biashara na Marekani, zitashindwa kupata insurance kutika makampuni yanayofanya biashara na Marekani, zitashindwa kufanya maintenance kwa kutumia makampuni yanayofanya biashara na Marekani.

Makampuni mengi ya ndege, ya bima, ya kutengeneza bidhaa hayataki kupigwa ban kufanya biashara Marekani.

Marekani ina uchumi wa asilimia 26 ya uchumi wa dunia.

Hiyo ni zaidi ya robo. Ndiyo maana kila siku unasikia Trump anatishia watu tariff. Uchumi mkubwa sana huu kuuachia. Usingekuwa mkubwa hivuo, Trump asingekuwa na nguvu ya kutishia tariffs kila mara.

Mwaka 2025 by nominal dollats Marekani ilikuwa na uchumi (GDP) wa $30.7 trillion out of the world's $115 trillion . Trillion, not billion.

Marekani ana 4% ya watu na 26% ya uchumi. Katika uzalishaji wa dunia zaidi ya $1 katika kila $4 zinazalishwa na uchumi wa US.

Uchumi huu ndio unaipa nguvu Marekani kuweka vikwazo.

Ila kuna wachumi wengi wanapinga vikwazo hivi vya kiuchumi wakisema kimsingi vitaudhoofiaha uchumi wa Marekani kwa kufanya watu wasiuamini mifumo ya Kimarekani na kujipanga vingine.

Mfano Ulaya wameshaanza kujipanga kuachana na mifumo ya teknolojia ya Marekani wajitegemee wenyewe zaidi.
 
Kijana punguza mis information? Una maana gani ukisema ZOTE? kwamba mpaka China, Russia na allies wengine ambao ndio miaka yote wamekua partners wa Iran? Pia vikwazo wameshawekewa miaka mingi tokea 2018 so hamna jipya
Sawa
 
Kwa Sasa uchumi wa Marekani unategemea mafuta ya mashariki ya kati kuuzwa US $
Siku waarabu wakijaniaruka na kuikataa US $ katika biashara Yao ya mafuta Marekani atakuwa kama joka la kibisa
Si wakatae tu hata leo sasa wameshindwa nini, unafikiri waarabu wenyewe wajinga wachukue sarafu zingine halafu wazipeleke wapi.

Watu ambao hamjawahi kufanya biashara ya kimataifa hakuna mjualo ni ushabiki tu wa kwenye vijiwe vya tangawizi na kahawa.
 
Si wakatae tu hata leo sasa wameshindwa nini, unafikiri waarabu wenyewe wajinga wachukue sarafu zingine halafu wazipeleke wapi.

Watu ambao hamjawahi kufanya biashara ya kimataifa hakuna mjualo ni ushabiki tu wa kwenye vijiwe vya tangawizi na kahawa.
Dollar ni matumizi yak ndiyo inaipa value , ndio maana aliingia mkataba wa petrodollar na ukienda kinyume unavamwa anzia na Iraq alipoanza kuuza mafuta yake wa Euro...Unaweza kufanya biashara na mwingine , ila bidhaa kubwa zimewekwa hivyo ...Saudia kukubali kwake matumizi ya dollar hapo amejanga urafiki , USA analazimisha pesa yake itumike , kuwa na uchumi mkubwa ni kwama pesa yake inakwua traded sana kila kona na anapata faida za moja kwa moja.

Mfumo wa dunia wa kufanya biashara ni unequal exchange , mfano wewe una kataratasi lako ambalo ni hela ya kenya na mimi langu la TZ tunafanyaje hapo biashara ?Dollar ni medium kila mtu anapeleka pesa yake kwenye value ya dollar ili kuwe na uniformity ya kufanya biashara , ilienda kupitia mabenk ya dunia ...Anachofanya USA , atakayefanya biashara na Iran anamuwekea vikwazo mpaka kumpandishia ushuru ..Still Iran anaweza kufanya biashara na nchi kama china , Russia .


Uchumi wa dunia sio mnavyofundishwa darasani bali ni umafia , hayo madeni anayodaiwa USA anadaiwa na nan? Kuna utapeli sana , kwa vile watu ni kama mazuzu wanafuata yale yale na wamekariri ..Hofu ya USA ni crypto currency , iran wanatumia sana crypto currency ...Dollar ikitemwa basi USA hana ujanja .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…