mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Marekani imekuwa ikijaribu kuzuia maendeleo ya nchi inazozihofia kwa kuziwekea vikwazo kwa matumaini kwamba zitadhoofika kiuchumi na kuzifanya zisiendelee kijeshi hata kuzifanya zisiwe tishio tena. Mategemeo yake ni kuwa zitakuja kumpigia magoti na kumwabudu kana kwamba kuwepo kwao kunategemea hisani ya marekani!
MIFANO:
1. Iran: Taifa la Iran limekuwa tishio kwa Marekani kwa maana ya nguvu za kiuchumi kupitia mafuta na kisha uchumi huo kuendeleza kujiimarisha kijeshi kitu ambacho ni tishio kwa Marekani. Marekani inataka lisiwepo Taifa linaloweza kumvimbia kama halikubaliani na matakwa yake!! Kwa hiyo Marekani iliiwekea vikwazo lukuki vya kiuchumi nchi ya Iran kwa matarajio kwamba itaporomoka sana kiuchumi na kijeshi hivyo kuilazimisha kusalimu amri na kuiangukia marekani.
Kinyume chake Iran haikuporomoka kihivyo kiasi cha kushindwa kuendeleza mipango yake ya kujiimarisha kijeshi na kuwa tishio kubwa zaidi kwa marekani kuliko awali. Sasa hivi Iran iko mstari wa mbele katika teknologia ya drones za kivita, makombora ya masafa marefu, na utaalamu wa teknologia ya nyuklia!. Ia ina meli na manowari za kivita na vyote hivi imejiendeleza yenyewe pamoja na uwepo wa vikwazo. Kwa sasa Iran ni tishio zaidi kijeshi kuliko ilivyokuwa kabla ya vikwazo. Kwa hiyo kwa Iran havikuweza kuipatia Marekani matokeo iliyoyatarajia.
2. Korea ya kaskazini: Korea ya Kaskazini ilikuwa tishio kwa Marekani tangu wakati wa vita vya korea. Ili kuizuia korea ya kaskazini isijiimarishe kiuchumi na kijeshi, Marekani pia iliiwekea vikwazo korea ya kaskazini mbali na vile vya umoja wa mataifa. Lakini pamoja na vikwazo hivyo Korea ya kaskazini imekuwa tishio zaidi leo kijeshi kwa kufanikiwa kutengeneza silaha za nyuklia, makombora ya masafa marefu, kurusha satelite angani na kadhalika. Pia kwa sasa Korea ya kaskazini ni tishio zaidi kijeshi kuliko ilivyokuwa kabla ya vikwazo!! Kwa sasa Marekani haiwezi kuthubutu kuishambulia Korea ya kaskazini kama ilivyofanya Libya au Iraq.
3. Urusi: Pia Marekani na washirika wake waliamini kuwa kwa kuiwekea vikwazo Urusi itaporomoka sana kiuchumi na kuilazimisha isalimu amri kwenye vita vyake na Ukraine!! Kinyume chake vikwazo hivyo vimeshindwa kuilazimisha urusi kusalimu amri badala yake uchumi wa nchi za magharibi ndio ulioathirika, na mataifa yanayoinukia kama India, Brazil, China nk yameamua kuanza kutumia fedha ya nchi zao kwenye biashara ya kimataifa na kuanza kupunguza matumizi ya dola ya marekani kitu ambacho marekani haikutarajia. Kwa sasa Urusi ni tishio zaidi kwa nafasi ya marekani maana kwa sasa urusi inayaongoza mataifa mengine kuangusha upolisi wa marekani kimataifa/American hegemony, na marekani si tena sauti ya mwisho kama ilivyokuwa inajiamini. A multipolar world is developing under the guidance of Russia and China!
Kama hiyo haitoshi, waswahili husema sikio la kufa halisikii dawa!! Hivi sasa Marekani inaiandama sana China kwa kuanza kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kupiga marufuku kuishirikisha teknologia ya juu katika vitu mbali mbali kama vile semiconductors technology. Lengo ni kuikwamisha isiwe tishio zaidi kiuchumi na kijeshi!! Ninashangaa: Kama ilishindwa kuikwamisha Iran na korea ya kaskazini kujiimarisha kijeshi je itafanikiwa kwa China?
Uncle Sam keshaanza kuadhirika mdogo mdogo na bado!