Marekani hakuna Rais daktari, CPT, Engineer wala Advocate? Kwanini hawapendi kusoma?

Obama na hata Biden ni PhD holders, Bill Clinton ni Professor........sema kwa wazungu hata wenye title hizo za elimu wanaitwa tu kwa majina yao ya awali bila kuzitaja, hawana mambo ya kujikweza au kujenga matabaka......

Utashangaa hakuna mtu anahangaika kumwita rais au waziri mkuu wa nchi kama Marekani na Uingereza mheshimiwa kama ilivyo hapa bongolala.

Nafikri wana discourage kujenga matabaka ndani ya jamii ndo maana inakuwa rahisi hata kuwawajibisha viongozi wanaokiuka sheria na miongozo waliyojiwekea maana hawachukuliwi kama watu special au miungu watu.​
 
Ha ha ha , dah Eti Mheshimiwa Mbunge Dokta. askofu Gwajima, ila Afrika tupo gizani Sana.
Wamegundua sasa wanajiandikisa OPEN UNIVERSITY, zingatia neno "chuo huria" kupata hizo masters na phD bila hata kukanyaga darasani. Wanataka hizo tittle za Docto na wakili ili wakadanganyie wapiga kura.
 
Ushamba na ulimbukeni tu unawasumbua
 
Ushamba na ulimbukeni tu unawasumbua
Na wanajiaibisha sana mikutano ya kimataifa.
Kwenye ile kesi ya Kampuni ya madini kule Canada vs Tanzania, wanasheria wa Tanzania walikuwa zaidi ya 12 na 5 wote ni doctor na professor, lakini kingereza hawajui, basi hizo submission wameandikiwa na kutumiwa wasome tu, yaani kusoma unaweza fikiri ni mtoto wa chekechea.
 
Ni matokeo ya elimu duni.Tunaona rais akipewa phd ndio anaheshimika na sio kusolve shida za wananchi
 
Ni matokeo ya elimu duni.Tunaona rais akipewa phd ndio anaheshimika na sio kusolve shida za wananchi
Na mbwembwe kedekede kumsimika hayo ma heshma yasiyo na impact yeyote.
Rais anapigwa interview BBC na Salim Kikeke anakosa majibu anajikuta anamgeuzia maswali tena kikeke!
 
Nyerere kwanza ni species nyingine, huyu Baba wa Taifa hakutaka ujinga wa hivi vyeo na majina ya ajabu. Alikuwa Mwalimu wa St . Marys [Pugu Seconday] na akawa rais, akaendelea kuitwa Mwalimu Nyerere.
Waliofuata sasa. !
 
Sijawahi kujua kumbe paroko wetu ni Dr. Jamaa yangu ndio alikuja kuniambia Kuwa alisoma na paroko ni Phd holder.
Wakatoliki kaa nao mbali.
Mapadri wengi wana digrii si chini ya tatu . Ukiona ana phD hiyo ana digrii nne,akaamua kupiga masters na phD.
Kwa mambo ya elimu CATHOLIC ndio bora duniani.
 
Ama ni ulimbukeni au kutokujiamini kwa muhusika mbele ya jamii.

Kwa jamii zilizostaarabika watu hawatambiani kwa elimu ya darasani kwani wengi wanayo bali wanatambiana kwa matokeo au matunda yanayotokana na elimu yako!
 
Mkuu umenikumbusha marehemu Mtikila aliwahi kusema waafrika wengi tuna ugonjwa wa Apedomia. Tuna unyani ndani yetu haujaondoka.
 
TAZAMA SHAHADA ZA MADAME CONDOLEEZA RICE

 
Sasa tufanyeje ili Watu waamke na kuanza kupuuzia hizi phD za kuiwa badala za matendo?
Mfano , mtu kama Kasheku Msukuma akitunukiwa phD. ya siasa utalewa, maana ana wa outsmart ma phd wa serikali, mawaziri na hata muongozaji wa mijadala.
Siku taalamu ikianza kulipa kuliko siasa ndiyo jibu tutapata
 
Ama ni ulimbukeni au kutokujiamini kwa muhusika mbele ya jamii.

Kwa jamii zilizostaarabika watu hawatambiani kwa elimu ya darasani kwani wengi wanayo bali wanatambiana kwa matokeo au matunda yanayotokana na elimu yako!
Hata Putin huwezi kuta anaitwa Dr wala Mhe ni Mr Putin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…