Marekani hakuna Rais daktari, CPT, Engineer wala Advocate? Kwanini hawapendi kusoma?


Wewe akili yako itakuwa sawa na ya Musukuma ....!!

Musukuma mwenyewe anaulilia huo Udaktari ....!!
 
Hapa ukipata urais ujue na udakitari lazima utapewa hata kama haukusoma kukuongezea uzito.
 
Sisi tuna ulimbukeni sana kwenye hizi issue za titles. Kila mtu saivi ana title, naona hata engineers wanakuja na Eng.
 
Sisi tuna ulimbukeni sana kwenye hizi issue za titles. Kila mtu saivi ana title, naona hata engineers wanakuja na Eng.
Walianza Engineers wanataka majina yao yawe Eng ERon, haya wamekuja wahasibu wanataka CPA[T], yani tuna upuuzi mwingi hizo nguvu tungeenda kuchimba mitaro tuelekeze maji kwenye mabwwa umeme usikatike.
 
Huku kwetu wanasiasa Ma-dr wanazidiwa akili na akina Msukuma. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wenzio wapo wapo miaka 300 mbele yetu mambo ya elimu walishamalizana hayana mpango ,hapa kwetu ni utapeli mtu anahonga apate masters, PhD na ujinga mwingine ili awe kiongozi apate easy money.

Tunawajua hata research mmeandikiwa ndio maana hamna maendeleo binafsi zaidi ya wizi.
 
Ni kwasababu hawana kitu kichwani.
 
Ujazo vs ubora. Tusilaumu kitu, tunaochagua ni sisi wananchi kwa hiyo mambo yakienda kombo tuanze kwanza kujipa lawama sisi wapiga kura.
Kura yako inabadilisha kitu kweli kwa hapa Tanzania!!??
 
Sio ujinga tu na ushamba pia, kuitwa Dr wakati kichwani mweupe kunasaidia nini. Angalia nchi iko gizani, hakuna sukari, dola hazionekani, kila kitu bei juu halafu wanasiasa vilaza wanapigana vikumbo kwa kununua Phd
Ndiyo wanachoweza
 
Huku kwetu kila kiongozi anaona ni ufahari kuitwa Dr. Hata kama kichwani ni empty head. Badala ya kuumiza vichwa kuzifanyia nchi zao mambo makubwa; wao wako busy kupeana, na hata kununua kabisa vyuoni hayo majina ya Udokta!!
 
Ni ushamba na ulimbukeni unawasumbua marais wa Africa. Ndiyo maana unakuta mtu kaukwaa urais halafu chap chuo flan kinamtunuku degree ya heshima ili aitwe Rais dr. fulani.

Kichekesho wakimaliza muda wao wa urais hao hao waliokuwa wakimuita Rais Dk. Jk wakati akiwa rais wanaanza kumuita rais mstaafu JK. Ile title ya dk wanaicha as if akistaafu na huo udokta unastaafu.

Waafrika tunashida sana
 
Hata raia wao wengine ambao wana phd za maana ukikutana nao utasikia call me Harison. Ila Mtanganyika utasika naitwa CPA, Dr ambilikile mhanga phd in social law.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…