Marekani hakuna Rais daktari, CPT, Engineer wala Advocate? Kwanini hawapendi kusoma?

Ili wananchi wao wawatambue kuwa wamesoma maana waafrika tunawaamini sana watu waliosoma hatakama hawana ujuzi na kazi au nyazifa tunazowapa
 
Mbona nilisikia kipindi Joe Biden anatwaa madaraka Hillary Clinton alimu address Dr Biden, au hao JD nao wanatumia title ya Dr?
 
Mbona nilisikia kipindi Joe Biden anatwaa madaraka Hillary Clinton alimu address Dr Biden, au hao JD nao wanatumia title ya Dr?
Utakuwa umechanganya!

Dr. Biden ni mke wa Joe Biden, Jill Biden. Ana Doctor of Education.

Ingia Google utafute Dr. Biden uone kitatokea nini.

Kila lawyer Marekani, kuanzia miaka ya 1950, ana JD, ambayo ni sawa tu na LLB.

 
Kwa wenzetu kusoma sana ni kwenda kutoa huduma muhimu aliyoisomea mhusika kwa wanaoihitaji hiyo huduma ili elimu kubwa yenye manufaa iwafikie wananchi wenzao wengi zaidi ili nchi zao zisonge mbele zaidi kimaendeleo kwa haraka zaidi,
Kwetu sisi mbobezi wa masuala ya Nyuklia anaacha kazi yake ili aende akapate cheo kikubwa cha kisiasa !
Kwetu sisi mbobezi katika nyanja za Injinia anaacha kazi yake anaenda kutafuta cheo cha kisiasa !!

Yote hiyo ni kwa sababu hatusomi kwa maana ya kupata elimu ili ije iwe ni chachu ya maendeleo kwa Nchi zetu bali husoma ili kutafuta fursa ya kupata mali nyingi tuweze kula Bata kiulaini !
 
Na viongozi wa Afrika ndio wanaongoza kwa kuzitaka , wakikutana Umoja wa Mataifa pale US-New York , kila Rais wa Afrika akisimama utaskia Hon Doctor ABC, alafu anaenda kukopa kwa mtu ambaye hana hiyo doctor, professa etc.
Kazi kweli kweli
 
VIJANA tutor wanafanya masters na phD ili wateuliwe kwenye bodi na nyadhifa za kisiasa. Kila mtu anawaza pa kupiga maana sisi ni vipofu.
 
Niulize swali hapa:
Kuna elimu inaitwa Egyptology, yaani elimu kuhusu Egypt. Elimu kuhusu Marekani, inaitwaje? Americanology? Watu waliosomea mambo ya taifa la Marekani, discipline yao inaitwaje?
Ubeberu-ology...
 
Familia Mbili zilizoshi/Zitazoshika urais Tanzania :
1. Ali Hassa Mwinyi- Rais wa Tanganyika
2. Hussein Mwinyi- Rais wa Zanzibar
1. Abei Karume
2. Karume JR.
1. Samia Suluhu.
2................Hafith Hassan 2030-35[Zanzibar]
Sio shida. Kwanza Makanyaga Kakosea kidogo John Adams hana udugu na Andrew Jackson.

John Adam rais wa 2 ni Baba wa John Quincy Adams rais wa 6.


William Harrison rais wa 9 ni Babu wa Benjamin Harrison rais wa 23.

Theodore Roosevelt rais wa 26 ana udugu na FDR (Franklin Delano Roosevelt) rais wa 32. Hata First Lady wa FDR, Eleanor Roosevelt ni mpwa wa Theodore Roosevelt. Hivyo walioana ndugu.

JFK, Rais wa 35, mdogo wake RFK (Alikuwa AG wakati wa uongozi wa kaka yake na baadae Senetor) ilikuwa agombee mwaka 1968 ila aliuawa na Sirhan Sirhan. Ted Kennedy ( alikuwa Senator kwa muda mrefu) mdogo wao mwingine akataka kugombea mwaka 1980. Mwanae Ted anayeitwa Patrick Joseph Kennedy aliwahi kuwa US Rep. Nadhani mnamjua Robert F. Kennedy Jr. mtoto wa RFK aliyeuawa 1968 alitaka kugombea mwaka huu.

George H. W. Bush rais wa 41 ni Baba wa George W. Bush rais wa 43. Mdogo wake George W. Bush, Jeb Bush (alikuwa Governor), alitaka kugombea mwaka 2016.
 
Inasababishwa na kutojiamini tu

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Sisi ni malimbukeni wa kila kitu, tunafanya mpaka kununua tusichokibobea, mtu anataka aitwe Injinia wakati alisoma masomo 7 ya art.
 
Hii ya kujiita CPA iko Tanzania tu.

Hakuna mahala pengine Duniani wahasibu wanaanza na CPA Maji ya Shingo, hakuna. Ni Tanzania pekee.

Vyeo vinavyojulikana hapa Duniani ni Eng, Dr, hii ni medical na Phd, Advocate ingawa sio sana.

Tanzania hapa hata watu wa manunuzi, taaluma isiyo na maana yoyote wanajiita PSPT Maji ya Shingo.

Tanzania kuna mambo ya hovyo sana.
 
We nae mwinyi hakuna na elimu kiivyo alikuwa form six sasa angetumia title gani nyerere alitumia title yake ya mwalimu..
Mtu kazaliwa 1925 haya mambo ya Form 6 aliyakuta kweli? Au mimi ndio sielewi.

He acquired a Diploma from the University of Adult Education, Dublin England between 1954-56. Hon. Mwinyi is a teacher by profession, he taught at Mangapwani and Bumbwini Primary Schools in Zanzibar. Further, Hon. Mwinyi possesses a certificate of excellence in English Language obtained at the Institute of Regent, England in 1960 and a Certificate of Excellence in Arabic Language he obtained at Cairo, Egypt in 1972-74.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…