Marekani iligunduliwa kibahati mbaya wakati wakristo wakifukuzana na maendeleo ya waislamu

Marekani iligunduliwa kibahati mbaya wakati wakristo wakifukuzana na maendeleo ya waislamu

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kama tunavyojua kuwa athari ya uislamu uliohuishwa na Muhammad rehma na amani zimshukie ziianza Makka halafu Madina na baada ya hapo zikaenea kila sehemu ya dunia kwa njia moja au nyengine.

Bila kwenda ndani sana na kutumia muda mwingi ni kuwa kutoka Madina Uislamu ulikuwa na makao makuu yake maeneo tofauti kulingana na muda na hekima za Allah aliyetukuka.Miongoni mwa vituo hivyo majina ya sasa ni Syria, Iraq,Uturuki na kwengineko kweny miji midogo midgogo.

Maendeleo makubwa ya waislamu kiellimu ,kiuchumi na kiutamaduni yalifanyika zaidi na kwa mara ya mwanzo nchini Iraq kwa vile walitumia aya za Qur'an zinazotaja umuhimu wa kalamu na kukushanya maandiko yoyote waliyoyapata na wao kuandika na kuchapisha vitabu vingi mno vya fani zote za kielimu walizofanikiwa kuziasisi.

Kutoka Iraq maendeleo ya kielimu ya waislamu yalihamia miji kama vile ya Cordova na Toledo ya Uhispania.Vitabu vya kihistoria vyenye kutaja tamaduni za watu mbali mbali duniani vilivutia sana wasomaji wa Ulaya waislamu kwa wakristo.

Kibiashara waislamu ndio waliokuwa wasafirishaji wa bidhaa mbali mbali kwa njia ya bara na bahari.Walitawala biashara ya viungo kutoka India kuingia Ulaya kuingia Ufaransa mpaka Ureno.Enzi hizo nchi hizo zilikuwa na washirikina wengi na wakristo wachache waliokuwa na msimamo mkali zaidi ya wakristo halisi waliopatikana Jerusalem

Watawala wa kikristo wa Ulaya walipatwa na choyo juu ya biashara za waislamu na jinsi uislamu ulivyoenea kwa kasi maeneo yao.Katika mbinu walizobuni ilikuwa ni pamoja na kuwatilia changa waislamu kwenye maendeleo yao na ikiwezekana washike shughuli zao za kiuchumi.

Njia nyepesi ya kufika India ilijulikana ni kupitia ardhini maeneo ya dola ya kiislamu chini ya Uthmania (Ottoman) lakini ilijulikana kwa uhakika wasingeweza kufanya hivyo kwa usalama na kufika India.Ikaonekana njia pekee japo ni ndefu lakini ni kwa kutumia bahari tu.

Mwaka 1492 malkia Isabella na mfalme Ferdinand ambao walikuwa wakereketwa wakubwa wa ukatoliki walikubali kufadhili msafara wa Christopher Columbus kwenda kufuatilia maendeleo ya eneo lililoitwa India ambako waislamu walikuwa wakifanya nalo biashara sana ya viungo na ambalo lilikuwa limeandikwa sana historia yake na waislamu waliokuwa wameishi na kutawala maeneo hayo karne kadhaa zililzopita.

Wakati huo waislamu walikwishachora ramani ya dunia wakionesha bara lote la Asia,Ulaya na Afrika.Wasomi wa kiislamu baada ya kukokotoa duara na muundo wa dunia walitabiri kuna eneo jengine nyuma ya ramani iliyochorwa ambako kutakuwa na ardhi nyengine japo hawakutaja ni eneo gani hilo.

Columbus alianza safari yake kuelekea India na kabla hajafika mbali kutokea Ureno alikooa japo yeye ni mtaliano, inaonekana ama aliisoma vibaya ramani ya dunia au alivutwa na mkondo wa maji kuelekea kusikojulikana.Hali hiyo pia ilichangiwa na kutokuwa na zana rasmi za safari ndefu kama hizo.Mwishowe akaangukia maeneo ya visiwa vya Bahamas katikati ya bara la America.

Baada ya mwaka mmoja Columbus akarudi Ureno na kupokewa kama shujaa akitangaza ameigundua India na ndio maana visiwa hivyo mpaka leo vinaitwa East/West Indies.Mafanikio ya msafara huo yalitangazwa sana ijapokuwa watu aliowateka Columbus na kurudi nao nyumbani walikuwa ni tofauti kabisa na wahindi waliozungumzwa na vitabu vya kihistoria.

Pamoja na kutangazwa sana kwa safari ya Columbus kuna watu na watawala ambao walijua mvumbuzi huyo hakufka alikokusudia kwenda na alifika eneo tofauti.Hivyo utaratibu ukafanywa kutolewa kwa mtu mwengine wa kukamilisha kazi hiyo na ndipo kwa sifa zake akachaguliwa Vasco da Gama.

Vasco da Gama alikuwa mjanja zaidi alijitayarisha vizuri kwa kuwa na kikosi kikubwa cha msafara wake.Baada ya msafara mrefu ulioleta matumani na uliowafikisha Afrika kusinini hatimae walifika Msumbiji.Waislamu wa eneo hilo wakawatilia shaka akina Vasco da Gama na kuanza kuwafanyia vitimbi ndipo haraka Vascoda gama akaondoka kuelekea kaskazini mpaka Malindi nchini Kenya.

Hapo kwa ujasusi wake akajua kuna mwanamaji mmoja hodari sana aitwaye Majjid mwenye asili ya Oman ambaye alikuwa na vifaa vya dira vya kusafiria baharini usiku na mchana.

Vascoda Gama Akaweza kuwashawishi wafanyakazi wa Majid ambao pamoja nao akisafiri nao mara kwa mara kwenda India,Wanamaji hao wakamuongoza Vascoda mpaka akafanikiwa kufika India mwishoni mwaka huo wa 1498.
 
Wako wapi akina Yoda na Mzee Kigogo na mwenzao Kiranga waje uwanjani wakanushe,
 
Ukitaka kujua uislamu unafananaje
Ingia ndani kwako, bidhaa au kitu chochote ambacho hakitoki kwenye nchi za waislamu kitupe😀😀😀
 
Wako wapi akina Yoda na Mzee Kigogo na mwenzao Kiranga waje uwanjani wakanushe,
Hata kama story yako ingekuwa ya kweli, Kwa nini India isisifiwe zaidi kwa sababu hitaji muhimu la wazungu ilikuwa kufika India kupitia baharini hivyo yeyewe ndio ilikuwa kichocheo?!
 
Hata kama story yako ingekuwa ya kweli, Kwa nini India isisifiwe zaidi kwa sababu hitaji muhimu la wazungu ilikuwa kufika India kupitia baharini hivyo yeyewe ndio ilikuwa kichocheo?!
Hapo cha muhimu zaidi ni kuwa waislamu walitangulia sana kimaendeleo kuliko wakristo.
Habari za India kupatikana viungo hilo ni jambo jengine la kimaumbile.Kwa hivyo kama ni sifa ziende kwa huyo aliyeonesha njia za kufika India kwa kuchora ramani zake.
 
Waislamu hawajawahi kufikia hata robo ya Roman Empire kwa maendeleo.
 
Kama tunavyojua kuwa athari ya uislamu uliohuishwa na Muhammad rehma na amani zimshukie ziianza Makka halafu Madina na baada ya hapo zikaenea kila sehemu ya dunia kwa njia moja au nyengine.

Bila kwenda ndani sana na kutumia muda mwingi ni kuwa kutoka Madina Uislamu ulikuwa na makao makuu yake maeneo tofauti kulingana na muda na hekima za Allah aliyetukuka.Miongoni mwa vituo hivyo majina ya sasa ni Syria, Irqq,Uturuki na kwengineko kweny miji midogo midgogo.

Maendeleo makubwa wa waislamu kiellimu ,kiuchumi na kiutamaduni yalifanyika zaidi na kwa mara ya mwanzo nchini Iraq kwa vile walitumia aya za Qur'an zinazotaja umuhimu wa kalamu na kukushanya maandiko yoyote waliyoyapata na wao kuandika na kuchapisha vitabu vingi mno vya fani zote za kielimu walizofanikiwa kuziasisi.

Kutoka Iraq maendeleo ya kielimu ya waislamu yalihamia miji kama vile ya Cordova na Toledo ya Uhispania.Vitabu vya kihistoria vyenye kutaja tamaduni za watu mbali mbali duniani vilivutia sana wasomaji wa Ulaya waislamu kwa wakristo.

Kibiashara waislamu ndio waliokuwa wasafirishaji wa bidhaa mbali mbali kwa njia ya bara na bahari.Walitawala biashara ya viungo kutoka India kuingia Ulaya kuingia Ufaransa mpaka Ureno.Enzi hizo nchi hizo zilikuwa na washirikina wengi na wakristo wachache waliokuwa na msimamo mkali zaidi ya wakristo halisi waliopatikana Jerusalem

Watawala wa kikristo wa Ulaya walipatwa na choyo juu ya biashara za waislamu na jinsi uislamu ulivyoenea kwa kasi maeneo yao.Katika mbinu walizobuni ilikuwa ni pamoja na kuwatilia changa waislamu kwenye maendeleo yao na ikiwezekana washike shughuli zao za kiuchumi.

Njia nyepesi ya kufika India ilijulikana ni kupitia ardhini maeneo ya dola ya kiislamu chini ya Uthmania (Ottoman) lakini ilijulikana kwa uhakika wasingeweza kufanya hivyo kwa usalama na kufika India.Ikaonekana njia pekee japo ni ndefu lakini ni kwa kutumia bahari tu.

Mwaka 1492 malkia Isabella na mfalme Ferdinand ambao walikuwa wakereketwa wakubwa wa ukatoliki walikubali kufadhili msafara wa Christopher Columbus kwenda kufuatilia maendeleo ya eneo lililoitwa India ambako waislamu walikuwa wakifanya nalo biashara sana ya viungo na ambalo lilikuwa limeandikwa sana historia yake na waislamu waliokuwa wameishi na kutawala maeneo hayo karne kadhaa zililzopita.

Wakati huo waislamu walikwishachora ramani ya dunia wakionesha bara lote la Asia,Ulaya na Afrika.Wasomi wa kiislamu baada ya kukotoa duara na muundo wa dunia walitabiri kuna eneo jengine nyuma ya ramani iliyochorwa ambako kutakuwa na ardhi nyengine japo hawakutaja ni eneo gani hilo.

Columbus alianza safari yake kuelekea India na kabla hajafika mbali kutokea Ureno alikooa japo yeye ni mtaliano inaonekana ama aliisoma vibaya ramani ya dunia au alivutwa na mkondo wa maji kuelekea kusikojulikana mpaka akaangukia maeneo ya visiwa vya Bahamas katikati ya bara la America.

Baada ya mwaka mmoja Columbus akarudi Ureno na kupokewa kama shujaa akitangaza ameigundua India na ndio maana visiwa hivyo mpaka leo vinaitwa East Indies.Mafanikio ya msafara huo yalitangazwa sana ijapokuwa watu aliowateka Columbus na kurudi nao nyumbani walikuwa ni tofauti kabisa na wahindi waliozungumzwa na vitabu vya kihistoria.

Pamoja na kutangazwa sana kwa safari ya Columbus kuna watu na watawala ambao walijua mvumbuzi huyo hakufka alikokusudia kwenda na alifika eneo tofauti.Hivyo utaratibu ukafanywa kutolewa kwa mtu mwengine wa kukamilisha kazi hiyo na ndipo kwa sifa zake akachaguliwa Vasco da Gama.

Vasco da Gama alikuwa mjanja zaidi alijitayarisha vizuri kwa kuwa na kikosi kikubwa cha msafara wake.Wakafanikiwa kufika Msumbiji lakini waislamu wa eneo hilo wakawatilia shaka akina Vasco da Gama na kuanza kuwafanyia uadui ndipo haraka Vascodagama akapanda kuelekea kaskazini mpaka Malindi nchini Kenya.

Hapo kwa ujasusi wake akajua kuna mwanamaji mmoja hodari sana aitwaye Majjid mwenye asili ya Oman ambaye alikuwa na vifaa vya dira vya kusafiria baharini usiku na mchana.

Akafanikiwa kuwashawishi wafanyakazi wake waliokuwa wakisafiri mara kwa mara kwenda India na wakamuongoza mpaka akafanikiwa kufika India mwishoni mwa mwaka huo wa 1498.
Hujui kujieleza.Acha ujinga.Rehma rehma.Upuuzi.Nenda Gaza ukakong'ontwe na "mayahudi"!
 
Waislamu hawajawahi kufikia hata robo ya Roman Empire kwa maendeleo.
Kongo ni kubwa kuliko mataifa mengi ya Afrika lakini iko nyuma sana kimaendelea.Hivyo ukubwa si hoja.Muhimu ni kujua kutumia fursa na kuzisambaza kwa wenzako kiutaalamu.
Jee hilo Lilifanywa na utawala wa roma au dola za kiislamu.
 
Watakaokusoma wote watakuona wewe ndio unasema uongo kuhusu kugunduliwa kwa Marekani
Unagunduaje kitu kinachoonekana wewe?Hebu acha uzezeta.Unaamini wazungu waligundua ziwa Nyanza/Victoria ambalo wazinza walikuwa wanaliona kila siku?Tumia akili we mjamaa.
 
Unagunduaje kitu kinachoonekana wewe?Hebu acha uzezeta.Unaamini wazungu waligundua ziwa Nyanza/Victoria ambalo wazinza walikuwa wanaliona kila siku?Tumia akili we mjamaa.
Neno ugunduzi litabaki na maana yake hiyo hiyo.Kwa watu wa Ulaya wazungu waligundua hilo ziwa ijapokuwa lilikuwepo kabla na lilijulikana na wenyeji.
Kugunduliwa kwa Marekani na Columbus ilikuwa ni muhimu kwa Ulaya lakini haina maana kuwa huko America hakukuwa na watu wenye akili.Kama nilivyoeleza mwanzo kote huko Allah alikuwepo na alitoa uongozi wake.
 
Kamusi yako uliyokariri kwenye mbichwa huo ni batili.Unatakiwa utandikwe mijeledi na ufundishwe vitu upya.
 
Kubali tu huu mjadala ni mkubwa na wewe
 
Back
Top Bottom