Ngoja nianze na Osama Bin Laden
Afghanistan ilikuwa katika hali ya vita ya wenyewe kwa wenyewe na miezi michache baada ya kufika kwa Osama kundi la Taliban lilivamia mji mkuu wa Kabul na kutangaza
Emirati ya Afghanistan likaendelea kutawala sehemu kubwa ya nchi.
Katika maeneo yaliyokuwa chini ya serikali ya Taliban Osama aliweza kuanzisha makambi mbalimbali alipopokea na kufunza wanajihadi kutoka nchi mbalimbali. Pamoja na Aiman az-Zawahiri alitoa tamko la fatwa mnamo tar. 23 Februari 1998 waliposema "Kuwaua Wamarekani na wanaoshikamana nao -kama ni wanajeshi au watu raia- ni wajibu wa kila Mwislamu mwenye uwezo wa kuyatekeleza katika nchi yoyote kwa kusudi la kuleta ukombozi wa msikiti wa al Aqsa na Masjid al-Haram (msikiti wa Makka) na kuwafukuza wanajeshi wao kutoka nchi zote za Uislamu ..
Kwa msaada wa Mungu tunamwita kila Mwislamu anayemwamini Mungu kutekeleza amri wa Mungu na kuwaua Wamarekani na kupora pesa zao kila mahali anapoikuta"
Mwaka uleule wa 1998 mabomu mawili yalipuliwa kwenye mashambulio ya kigaidi ya 7 Agosti 1998 katika Afrika ya Mashariki dhidi ya balozi za Marekani huko Nairobi na Dar es Salaam yaliyoua zaidi ya watu 300 na kuwajeruhi maelfu. Serikali ya Marekani ilijaribu kuwashawishi viongozi wa Taliban kuwakabidhi bin Laden lakini hadi 2001 badi hawakufikia mapatano.
Tarehe 12 Oktoba 2000 wanajihadi wa al Qaida walishambulia maonowari USS Cole nchini Yemen. Tarehe 9 Septemba 2001 wapiganaji wa al Qaida walimwua mpinzani wa Taliban
Ahmad Shah Massoud kwa bomu.
Tendo hili lilifuatwa na shambulio la 11 Septemba 2001 katika Marekani lililoua takriban watu 3,000. Marekani ilidai tena Afghanitan imkabidhi bin Laden lakini viongozi wa Taliban walikataa wakadai kuonyeshwa uthebitisho. Rais Bush wa Marekani alijibu kwa kushambulia Afganistan tar. 7 Oktoba 2001; baada ya kutekwa kwa Kabul bin Laden alikimbia kwenye mipango ya milima ya Tora Bora na kutoka huko katika maeneo ya Pakistan kaskazini-mashariki ambako serikali ya taifa ilikuwa na athira ndogo.
Jitihada wa Wamarekani kumkamata zilikuwa bila mafanikio. Inaaminiwa ya kwamba Osama bin Laden aliendelea kujificha nchini Pakistan, labda kwa msaada wa sehemu ya huduma ya usalama ya kijeshi ya nchi hiyo. Alitoa matagazo mbalimbali kwa njia ya kanda za video zilizosambazwa duniani kwa njia ya intaneti.
Kuna dalili ya kwamba aliishi kwa siri tangu mwaka 2006 katika mji wa Abbottabad kwenye nyumba alipouawa mwaka 2011.
Nitarejea mkuu.....