Bila kuchokozwa raisi Trump ameamua tu kupiga maeneo ya Yemen akijua hiyo ni nchi dhaifu kwa miaka mingi.
Kwa kujua huko nyuma wameshaipiga sana na kuvunja miundo mbinu mingi ya nchi hiyo lakini bado tu Trump ameelekeza nguvu zake huko huku akijisifu kwamba anashusha kiama huko Yemen
Tukio hili limekuja huku raisi huyo akiwa amechagizwa na wagomvi wake wengi ambao wote wameamua kutokumunea haya katika sera zake za vita vita.
Marekani ingekuwa ina nguvu kubwa kweli za kuionesha dunia basi ingemsaidia Zelensky kumshinda Putin au ingepiga angalau lengo moja la rasilimali za kichina.
Kwa uchache Trump angeipiga Korea Kaskazini au angalau Iran.Kote huko Marekani inaogopa kupata fedheha kama ilizokwishakuzipata huko nyuma na badala yake kuamua kuipiga Yemen bila sababu za msingi.
Kama ni kosa la Houth basi ni kule kusema kuwa wataendelea kushambulia maslahi ya Israel kwa vile inaendelea kuwaonea wapalestina jambo ambalo ni kweli.
Muhimu ni kuwa uchaguzi huo wa Marekani pia hautaweza kuiepusha na kushindwa kwani inapigana na watu dhaifu lakini wenye hamasa kubwa za kujitetea