Beberu Marekani Ametoa Msaada wa Shilingi Tilioni 15 Nchini Tanzania Kwa miaka 20 iliyopita katika Mpango Mmoja tuu wa.kupambana na Magonjwa hasa Ukimwi na Kifua Kikuu na kuokoa maelfu ya maisha ya Watanzania kwenye sekta ya Afya.
Hapo sijagusia MCCL,USAid Wala Wakfu wa Bill & Melinda Gates Foundation kwenye Kifua Kikuu,Malaria nk.
My Take; Sielewi Mnaoshobokea Russia Huwa mnafanya hivyo Kwa Maslahi yapi hasa?
Anaejua kiasi ambacho Russia amewahi toa Kwa Tanzania of any kind anijuze.
Nawashukuru sana beberu USA na nitasimama na Marekani mda wote na wakati wote.
Mungu ibariki Tanzania na Wabariki Mabeberu America.
Urusi imetusaidia sana kwenye vitu vya maana kwa kulinda utaifa wetu, usalama na ulinzi wa nchi yetu. Kwa taarifa yako majeshi yetu yamepata mafunzo toka Urusi na China ikiwemo vifaa vya kijeshi wakati US wamekuwa wakitusaidia sana kwenye mambo ambayo yatawasaidia sana wao kututawala na kwa maslahi yao mfano ushoga, kuharibu mbegu za mazao yetu na kuleta GMOs, kuharibu uzazi wa watz kwa kuleta madawa yenye madhara kwenye uzazi. Kwa ujumla Urusi inasaidia kufanya watz wajitambue kwa kufanyakazi zaidi ili tujitegemee wakati US inawafanya watz kuwa tegemezi.