round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Walianza kwa kiburi na jeuri lakini muda huu barua zinajazana white house zikiishia na “wako mtiifu”
Ni wiki 2 tu tangu aapishwe ila mambo yanavyoendelea utadhani yupo mwaka wa tatu
COLOMBIA
Rais wa Colombia Gustavo Petro alizikatalia ndege za Marekani kutua zikiwa zimebeba wahamiaji haramu walioingia Marekani kutoka Colombia.
Trump alijibu kwa kuongeza ushuru kwa 25% kwa bidhaa zote zinazoingia Marekani kutoka Colombia na baada ya wiki moja ushuru utapandishwa hadi 50%, ukaguzi mkali zaidi wa shehena za mizigo zinazowasili kutoka Colombia, Pamoja na vikwazo vya visa kwa wanachama wote wa chama cha rais wa Colombia, wafuasi na familia zao.
Ndani ya lisaa kasoro Colombia ilitangaza ndege ya rais itatumwa kuwachukua raia wa Colombia waliokuwa wanatarajiwa kurejeshwa. ofisi ya Rais Petro iliandika "Serikali ya Colombia, chini ya uongozi wa Rais Gustavo Petro, imeandaa ndege ya rais kuwezesha kurejea kwa heshima kwa raia wa Colombia waliokuwa wanatarajiwa kuwasili nchini leo asubuhi"
Trump amekubali kuahirisha ushuru kwa mwezi mmoja huku akifuatilia uwajibikaji kutoka kwa serikali ya Colombia na kufanya mashauriano zaidi na Rais Gustavo ili kupata makubaliano endelevu
MEXICO
Rais wa Marekani, Donald Trump, alitangaza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zote zinazoagizwa kutoka Mexico. Hatua hii ililenga kushinikiza Mexico kuimarisha ulinzi dhidi ya wahamiaji haramu wanaoingia Marekani na kupunguza ulanguzi wa dawa za kulevya hasa fentanyl inayokadiriwa kuwa na nguvu mara 50 zaidi ya heroin na imechangia ongezeko kubwa la vifo vya ku overdose nchini Marekani.
Mexico ilijibu kwa kutishia kutoza ushuru wa kulipiza kisasi kwa bidhaa za Marekani. Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum, alitangaza kwa sauti kali kwamba hapelekeshwi na ushuru utawekwa kwa bidhaa za Marekani.
Hata hivyo, ndani ya siku tatu, Rais wa Mexico aliahidi kuimarisha usalama wa mipaka kwa kupeleka wanajeshi 10,000 wa Walinzi wa Kitaifa kwenye mpaka wa Marekani na Mexico ili kudhibiti uhamiaji haramu na kuzuia usafirishaji wa madawa ya kulevya.
Trump amekubali kuahirisha ushuru kwa mwezi mmoja huku akifuatilia uwajibikaji kutoka kwa serikali ya Mexico na kufanya mashauriano zaidi na Rais Claudia ili kufikia makubaliano endelevu
CANADA
Rais wa Marekani, Donald Trump, alitangaza ushuru wa asilimia 25 kwa bidhaa zote zinazoagizwa kutoka Canada. Hatua hii ililenga kushinikiza Mexico kuimarisha ulinzi dhidi ya wahamiaji haramu wanaoingia Marekani na kuzuia ulanguzi wa dawa za kulevya hasa fentanyl.
Canada ilijibu kwa kutoza ushuru wa kulipiza kisasi kwa bidhaa za Marekani. Waziri mku wa Canada, Justin Turduau, alisisitiza kwamba hapelekeshwi na ushuru utaongezwa kwa bidhaa za Marekani
Hata hivyo, baada ya siku moja, Waziri mkuu wa Canada aliahidi kuimarisha usalama wa mipaka kwa kuboresha bajeti ya ulinzi wa mipakani ya dola bilioni 1.3 (shilingi za kitanzania triioni 3.3) kwa kuongeza helikopta za kisasa, kuongeza ushirikiana kwa vikosi vya Marekani, kuvitambua rasmi vikundi vya ulanguzi kuwa magaidi na kuunda kikosi maalum cha kupambana na walanguzi wa Fetanyl.
Trump amekubali kuahirisha ushuru kwa mwezi mmoja huku akifuatilia uwajibikaji kutoka kwa serikali ya Canada na kufanya mashauriano zaidi na Waziri mkuu Justin Trudeau ili kufikia makubaliano endelevu
VENEZUELLA
Katika kipindi cha utawala wa Rais Joe Biden, serikali ya Venezuela haikuwa ikikubali kupokea wahamiaji waliorejeshwa kutoka Marekani. Hata hivyo, chini ya utawala wa Rais Donald Trump, hali imebadilika. Serikali ya Venezuela imekubali kupokea wahamiaji haramu waliovuka kuingia Marekani ikiwa ni pamoja na wanachama wa genge la uhalifu la Tren de Aragua. Aidha, Venezuela imewaachia huru raia sita wa Marekani waliokuwa wakishikiliwa nchini humo baada ya mazungumzo kati ya Rais Nicolás Maduro na mjumbe maalum wa Rais Trump.
PANAMA
Mfereji wa Panama ni njia ya maji iliyotengenezwa kwa lengo mahsusi la kupunguza muda na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa kwa kuunganisha bahari ya Pacific na Atlantic, wanufaika wakubwa wakiwa ni Marekani
Ni mradi ulioigharimu Marekani pesa nyingi sana kuukamilisha na watu takribani elf 20 walipoteza uhai wenye ujenzi,
Awali mfereji ulikuwa chini ya Marekani, mwaka 1999 kwa makubaliano Marekani iliridhia kuwapa nchi ya Panama wausimamie.
Shida inauja China ilipoanza kuwa na ushawishi mkubwa Panama Canal kiasi inaripotiwa hata vibao vya maelezo vingi vina maandishi ya kachina, sio hivyo tu hata meli za mizigo za Marekani zinatozwa tozo kubwa na meli za kivita za Marekani zinacheleweshwa.
Trump akatangaza atauchukua mfereji wa Panama ama sivyo wazingatie makubalioano wawe fair, wapunguze tozo na kukaa mbali na China.
Rais wa Panama alikataa mapendekezo hayo.
Trump akamtuma Waziri wa mambo ya nje ya Marekani kwenda Panama, siku inayofuata rais wa Panama alitangaza kusitisha kurenew mikataba ya China.
Hata hivyo Trump anaonekana bado kutoridhika na maamuzi hayo, hatua za ziada zinategemewa.