Marekani inapata faida gani kugombanisha majirani?

Webabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2010
Posts
8,870
Reaction score
14,258
Kila penye ugomvi duniani unaohusu ndugu na majirani lazima Marekani atakuwepo upande mmoja wapo wa watu hao.

Ukienda Pakistan na Afghanistan utamkuta Mmarekani,Ukienda Urusi na Ukraine ni hivyo hivyo na ukienda Korea Kaskazini na Korea kusini hali ni hiyo hiyo. Vivyo hivyo ukienda Palestina na Israel.

Si lazima uwe ugomvi mkubwa hata ugomvi mdogo wa ndani lazima Marekani atakuja upande wa adui yako.

Je, kugombanisha na kuwa mchokozi kwa Marekani ni hobi au kuna faida yoyote kwa taifa hilo.
 
Sio tu kugombanisha pia hataki vita Viishe, hapo Ukraine kama Atakua na Dalili za Kushinda watapunguza misaada ili kubalance.

Libya walisupport waasi, walivyoingia madarakani sasa hivi wana support waasi wengine ambao wanapinga waasi wa mwanzo.

Kukiwa na Vita wanapata Faida mbalimbali ila Faida kubwa zaidi ni Kuuza Silaha.

Mwaka 2018 Nchi zilitumia Dola Bilioni 1800 kununua Silaha, hio ni Trilioni 1.8 ya kimarekani, sawa na Quadrilion zaidi ya 4 za kitamzania. Bajetu yetu zaidi ya miaka 100.
 
Kukiwa na Vita wanapata Faida mbalimbali ila Faida kubwa zaidi ni Kuuza Silaha,

Kama ni hivyo itachukua muda gani ndugu kuzinduka na kulinda maisha yetu.
 
Kila penye ugomvi duniani unaohusu ndugu na majirani lazima Marekani atakuwepo upande mmoja wapo wa watu hao.
Ukienda Pakistan na Afghanistan utamkuta Mmarekani,Ukienda Urusi na Ukraine ni hivyo hivyo na ukienda Korea Kaskazini na Korea kusini hali ni hiyo hiyo. Vivyo hivyo ukienda Palestina na Israel. Si lazima uwe ugomvi mkubwa hata ugomvi mdogo wa ndani lazima Marekani atakuja upande wa adui yako.
Jee kugombanisha na kuwa mchokozi kwa Marekani ni hobi au kuna faida yoyote kwa taifa hilo.
Sasa kwa nini hao wakubali kuchonganishwa na Marekani hadi kuchukiana na kuuana wenyewe kwa wenyewe? Unakuta wana dini moja Mungu mmoja wa kweli lugha moja kwa nini wakubali likafiri kutoka mbali huko aje awachonganishe tena kutumia dini yao kupigana, kuchukiana kuchinjana. Kwa nini iwe hivyo?
 
Dunia hii usipokua mstarabu utabaki Kama mpuuzi, utapigwa ,utadhalilishwa, huwezi simama KWa watu wastarabu na kile unahamini ni mawazo yako na hakuna wa kukufanya kitu, mfano uteke, ubake haki za watu, uwe mungu mtu, upoke KILA kitu kisa tu umejiwekea maulinzi, wakati haki zote za kimungu KWa mwanadam ni sawa na za binadam wengine bila kujali cheo Chako, mtapata kazi kubwa Sana , So USA washughulikia wahuni nasema Kama bado basi ikaongeze bajeti, Dunia imejaa Sana wahuni na ni lazima tiwa adabu bila kujali ni Afrika au mataifa menginge.
 
Mleta uzi, kuna mahali umesema; "si lazima uwe ugomvi mkubwa hata ugomvi mdogo wa ndani lazima Marekani atakuja upande wa adui yako."

Sasa, kumbe ugomvi tayari upo! Pia, kwanini aje upande wa adui yako? Je, hawezi kuja upande wako?

Hapo umejipinga wewe mwenyewe, maana kwenye title ya uzi umeitaja Marekani kuwa ndiyo inayogombanisha majirani. Lakini, kwenye content ya uzi unasema kuna ugomvi tayari unaendelea ambapo Marekani anakuja baadaye.

Waingereza wanasema, contradiction!

Iko hivi:
Marekani huchagua upande ili kulinda maslahi yake kama ambavyo nchi nyingine yoyote inavyofanya. Tofauti ni kuwa, kutokana na ushawishi wake mkubwa wa kisiasa, kiuchumi, kijeshi na kiutamaduni duniani, Marekani husababisha matokeo ama athari kubwa pale inapochagua upande hasa katika mgogoro.

Marekani hii ambayo unasema iko upande wa Korea Kusini, Israel na Ukraine kwa sasa, ndiyo hiyohiyo ambayo ilikuwa upande wa Urusi ama USSR katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia (WW2) ikiisaidia USSR kwenye masuala ya kijeshi na kiraia katika kushinda vita ya kukomboa maeneo yake yaliyovamiwa na Adolf Hitler mwaka 1941 (Operation Barbarossa).

Kuna msemo maarufu unaotumika sana kuielezea Marekani na sera yake ya masuala ya kigeni (foreign policy), unasema: "America has no permanent friends or enemies, only interests."

Swali:
Je, Marekani ndiyo iliyoigombanisha USSR na Ujerumani ya Adolf Hitler?
 
Issue ni Puppets leader, vita vingi unavyoviona duniani si matakwa ya wananchi, kuna watu wachache wana amua hao wengi wakitaka ama wasitake inakua.

Hakuna serikali ambayo ni 100% ya kidini Dunia nzima.
 
Dunia hii usipokua mstarabu utabaki Kama mpuuzi, utapigwa ,utadhalilishwa, huwezi simama KWa watu wastarabu na kile unahamini ni mawazo yako na hakuna wa kukufanya kitu, mfano uteke, ubake haki za watu, uwe mungu mtu, upoke KILA kitu kisa tu umejiwekea maulinzi, wakati haki zote za kimungu KWa mwanadam ni sawa na za binadam wengine bila kujali cheo Chako, mtapata kazi kubwa Sana , So USA washughulikia wahuni nasema Kama bado basi ikaongeze bajeti, Dunia imejaa Sana wahuni na ni lazima tiwa adabu bila kujali ni Afrika au mataifa menginge.
Kuna msemo mmoja waswahili wanasema Ukipenda Boga penda na ua lake.

Kama unaamini wanachokifanya ni Ustaarabu utakubali kuolewa na mwanaume mwenzako? Utakubali kubadilishwa Jinsia?

Wanachofanya Marekani ni Wizi tu nchi nyingi walizovamia baadae wanakiri ni Makosa, Wamevamia Iraq na kusema wana silaha za maangamizi mpaka leo hakujapatikana chochote,

Afghanistan huko wakulima wa watu wa Taliban wame wa hype wee mpaka leo tunawaona wapo vile vile, hawana uwezo wowote wa kijeshi kulipua Pentagon.
 
Sio tu kugombanisha pia hataki vita Viishe, hapo Ukraine kama Atakua na Dalili za Kushinda watapunguza misaada ili kubalance.

Libya walisupport waasi, walivyoingia madarakani sasa hivi wana support waasi wengine ambao wanapinga waasi wa mwanzo.

Kukiwa na Vita wanapata Faida mbalimbali ila Faida kubwa zaidi ni Kuuza Silaha,

Mwaka 2018 Nchi zilitumia Dola Bilioni 1800 kununua Silaha, hio ni Trilioni 1.8 ya kimarekani, sawa na Quadrilion zaidi ya 4 za kitamzania. Bajetu yetu zaidi ya miaka 100.

Sasa kwa nini hao wakubali kuchonganishwa na Marekani hadi kuchukiana na kuuana wenyewe kwa wenyewe? Unakuta wana dini moja Mungu mmoja wa kweli lugha moja kwa nini wakubali likafiri kutoka mbali huko aje awachonganishe tena kutumia dini yao kupigana, kuchukiana kuchinjana. Kwa nini iwe hivyo?
Anatumia kila kinachowezekana.Kuanzia dini mpaka ukabila na ubaguzi wa rangi..
 
Sio tu kugombanisha pia hataki vita Viishe, hapo Ukraine kama Atakua na Dalili za Kushinda watapunguza misaada ili kubalance.

Libya walisupport waasi, walivyoingia madarakani sasa hivi wana support waasi wengine ambao wanapinga waasi wa mwanzo.

Kukiwa na Vita wanapata Faida mbalimbali ila Faida kubwa zaidi ni Kuuza Silaha.

Mwaka 2018 Nchi zilitumia Dola Bilioni 1800 kununua Silaha, hio ni Trilioni 1.8 ya kimarekani, sawa na Quadrilion zaidi ya 4 za kitamzania. Bajetu yetu zaidi ya miaka 100.
Kama ni kweli anafanya hivi, basi tumsifie kwa akili kubwa alokuwa nayo.
 
Dunia hii usipokua mstarabu utabaki Kama mpuuzi, utapigwa ,utadhalilishwa, huwezi simama KWa watu wastarabu na kile unahamini ni mawazo yako na hakuna wa kukufanya kitu, mfano uteke, ubake haki za watu, uwe mungu mtu, upoke KILA kitu kisa tu umejiwekea maulinzi, wakati haki zote za kimungu KWa mwanadam ni sawa na za binadam wengine bila kujali cheo Chako, mtapata kazi kubwa Sana , So USA washughulikia wahuni nasema Kama bado basi ikaongeze bajeti, Dunia imejaa Sana wahuni na ni lazima tiwa adabu bila kujali ni Afrika au mataifa menginge.
Takbiiirrrrrr
 
Kama ni hivyo itachukua muda gani ndugu kuzinduka na kulinda maisha yetu.

Crusade hiyo kesha ianzisha Putin, lakini kwa bahati mbaya ni mataifa/watu wachache Duniani wanao tambua lengo kuu la Putin pamoja na mataifa mengine makubwa kijeshi ambayo yana unga mkono harakati za Putin lakini hawataki kujionyesha moja kwa moja labda itakapo bidi kifanya hivyo ili wainusuru Dunia dhidi ya kikundi cha mafiosa mambo leo, mataifa hayo yatasaidiana na Urusi kuwadhibiti. Wameanza na BRICS alliance mengine yatafuata zikiwemo taasisi za kifedha, maendeleo na finally masuala ya ushirikiano wa kijeshi - kwa bahati mbaya au nzuri the other side never saw it coming!!
 
Mleta uzi, kuna mahali umesema; "si lazima uwe ugomvi mkubwa hata ugomvi mdogo wa ndani lazima Marekani atakuja upande wa adui yako."

Sasa, kumbe ugomvi tayari upo! Pia, kwanini aje upande wa adui yako? Je, hawezi kuja upande wako?

Hapo umejipinga wewe mwenyewe, maana kwenye title ya uzi umeitaja Marekani kuwa ndiyo inayogombanisha majirani. Lakini, kwenye content ya uzi unasema kuna ugomvi tayari unaendelea ambapo Marekani anakuja baadaye.

Waingereza wanasema, contradiction!

Iko hivi:
Marekani huchagua upande ili kulinda maslahi yake kama ambavyo nchi nyingine yoyote inavyofanya. Tofauti ni kuwa, kutokana na ushawishi wake mkubwa wa kisiasa, kiuchumi, kijeshi na kiutamaduni duniani, Marekani husababisha matokeo ama athari kubwa pale inapochagua upande hasa katika mgogoro.

Marekani hii ambayo unasema iko upande wa Korea Kusini, Israel na Ukraine kwa sasa, ndiyo hiyohiyo ambayo ilikuwa upande wa Urusi ama USSR katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia (WW2) ikiisaidia USSR kwenye masuala ya kijeshi na kiraia katika kushinda vita ya kukomboa maeneo yake yaliyovamiwa na Adolf Hitler mwaka 1941 (Operation Barbarossa).

Kuna msemo maarufu unaotumika sana kuielezea Marekani na sera yake ya masuala ya kigeni (foreign policy), unasema: "America has no permanent friends or enemies, only interests."

Swali:
Je, Marekani ndiyo iliyoigombanisha USSR na Ujerumani ya Adolf Hitler?
Mkuu unaupiga mwingi sana.
 
Kuna msemo mmoja waswahili wanasema Ukipenda Boga penda na ua lake.

Kama unaamini wanachokifanya ni Ustaarabu utakubali kuolewa na mwanaume mwenzako? Utakubali kubadilishwa Jinsia?

Wanachofanya Marekani ni Wizi tu nchi nyingi walizovamia baadae wanakiri ni Makosa, Wamevamia Iraq na kusema wana silaha za maangamizi mpaka leo hakujapatikana chochote,

Afghanistan huko wakulima wa watu wa Taliban wame wa hype wee mpaka leo tunawaona wapo vile vile, hawana uwezo wowote wa kijeshi kulipua Pentagon.
Mbona mwapokea misaada yao je tz nayo imeolewa? Ndio Nchi za Magharibi agenda yao ya kusaport ushoga ipo ila je kabla yao dunia hii , Hata tanzania Ushoga umeanza leo,?

Ninaposema USA Watia nchi za kipuuzi nidham lazima kuwaunga mkono,haipunguzi chochote,

Hivi KWa mataifa yetu uchwara Afrika, na mengine bila kuwa na mtu mkubwa kidunia wa kuyaratibu Kama USA wafikili Hali itakuaje, mfano for 95% ya viongozi wa Afrika ni wezi tu, that's wanajipendekeza kuendea kuiba,
Takbiiirrrrrr
Amen
 
Iraq ilikuwa ni Nchi inayosaidiwa? Kabla ya vikwazo vya USA walikuwa na Uchumi mkubwa Kushinda hadi Uingereza, Kama Unavyoona Qatar, Libya, Dubai na wengineo Iraq walikuwa na pesa na maendeleo kedekede.

Kaja mzee wa ustaarabu kaacha Yatima, magofu mabovu bovu, kaiba mafuta na udhalimu kibao. Kama unafikiri kutoa roho za mamilioni ya watu wasio na hatia ni ustaarabu kaa nao ustaarabu wako.
 
Back
Top Bottom