Marekani inazidi kujiabisha tu eti kwa kujidai “kususia Michezo ya Olimpki ya Majira ya Baridi ya Beijing”

Marekani inazidi kujiabisha tu eti kwa kujidai “kususia Michezo ya Olimpki ya Majira ya Baridi ya Beijing”

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
1641441294967.png


Na Pili Mwinyi

Mwanzoni mwa mwezi Disemba 2021 serikali ya Marekani ilitangaza kususia Michezo ya Olimpki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022, kwa kile walichodai kwamba wanapinga ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na China, hivyo haitaleta maafisa wake kuja China kushiriki michezo hiyo. Ajabu ni kwamba hata mwezi haujamalizika Marekani imeomba viza kwa ajili ya maafisa wake kuja China kwenye michezo ya Olimpiki.

Waswahili wanasema njia ya muongo ni fupi, Marekani bila ya aibu ilifuta kauli yake ya kususia michezo ya olimpiki ikisahau kwamba nyuma yake kuna nchi kadha ilizozihadaa na kuziingiza kwenye mtego wake wa kususia. Hivyo Iikaamua kuleta maombi ya kupatiwa viza kwa ajili ya maafisa wake 18 ambao ni walewale iliosema kwamba hawatakuja kushiriki michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing, eti kwa kisingizio kwamba wanakuja China ili kutoa msaada wa kiusalama na matibabu kwa wanariadha wa Marekani, na kama haitoshi Marekani imesema baadaye inaweza kuwasilisha maombi mengine ya viza kwa ajili ya maafisa wake 40.

China imeweka wazi kwamba inataka kufanya michezo hii ya mwezi Februari kuwa salama kadiri iwezavyo. Na kutokana na janga la COVID-19, ilifanya maamuzi magumu ya kuacha kufanya sherehe kubwa na kuzuia watazamaji kutoka nchi za nje. Ina maana kwamba huu ni uamuzi wa China kukubali kuwapatia viza maafisa hao au la, ikizingatiwa kwamba Marekani hadi sasa imeshindwa kuzuia kuenea kwa COVID-19 miongoni mwa maafisa wa ngazi ya juu.

Lakini wahenga wanasema “ada ya mja hunena, muungwana ni vitendo” Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian, alisema China bila kinyongo itashughulikia maombi ya viza ya Marekani kwa mujibu wa utaratibu wa kimataifa, kanuni husika na kanuni ya usawa. Hata hivyo aliionya Marekani kufuata moyo wa Olimpiki kivitendo, kujiepusha kufanya michezo kuwa suala la kisiasa, na kuacha maneno na vitendo potovu vinavyovuruga au kudhoofisha Michezo ya Olimpiki ya Majira ya baridi ya Beijing.

Awali msemaji wa ikulu ya Marekani Jen Psaki, alisema Marekani haitaichukulia michezo ya Olimpiki ya Beijing kama michezo ya kawaida kwasababu ya ukatili wanaofanyiwa watu wa Xinjiang. Je nini kimewafanya hadi waamue kubadilisha mawazo yao na sasa kuiona ni michezo ya kawaida kama inayoandaliwa na nchi nyingine, ama kuna nini hasa ndani yake?

Wakati wanatangaza kususia michezo hii, nchi kama Uingereza na Canada pamoja na Australia nazo pia zilifuata nyayo za Marekani, huku nchi za Ulaya zikishinikizwa kufuata msimamo huo, lakini ni Ubelgiji tu ndio iliyofuata mkumbo huo. Naona kwa namna fulani, dhana ya kisiasa ya nchi za Magharibi hasa Marekani, ni kueneza propaganda dhidi ya China, ambapo wanasiasa wanaonekana kana kwamba wanalazimishwa kuichukia China.

Ni dhahiri kwamba huu ulikuwa ni uchokozi wa makusudi ambao hauna maana wala msingi wowote na unaharibu vibaya moyo wa mshikamano wa kimataifa ambao unabebwa na michezo ya Olimpiki. Kwanza kabisa wanasiasa wa Marekani hata kama wangesusia kweli, basi isingekuwa tatizo, kwa kuwa hawajalazimishwa kuhudhuria, kwani ni hiari yao kuja ama kutokuja.

Sheria ya Olimpiki inasema wazi kwamba wanasiasa wanaruhusiwa kuhudhuria michezo hiyo katika nafasi rasmi tu tena kwa mwaliko wa kamati zao za kitaifa za Olimpiki, ambapo uamuzi wa mwisho unakuwa chini ya Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) na nchi mwenyeji. Ndio maana IOC ilisema inaheshimu maamuzi ya Marekani, kwani uwepo wa maafisa hao hautaongeza wala kupunguza chochote.

Kwa wale walioifuata Marekani kususia michezo hii kuna maneno mawili tu ya kuwaambia “kiko wapi sasa”. Ni dhahiri kwamba Marekani imewaingiza mkenge wenzake na kuwa kigeugeu kwa kudai kwamba itasusia michezo, lakini baadaye imewaombea maafisa wake viza ya kuja kushiriki michezo hiyohiyo ambayo imeisusia. Marekani ikiwa kama nchi kubwa na inayoheshimika duniani, inapaswa kukaa chini na kujiuliza itaendelea kujiabisha hadi lini kutokana na chuki zake dhidi ya China?
 
wamarekani wana tabia za kiswahili sana kuliko hata uswahili wa mzaramo wetu
 
Back
Top Bottom