Mabepari hasa Marekani hana adui wa kudumu. Linapokuja suala la maslahi fulani haoni shida kuungana na adui yake.
Katika hali ya kawaida, je, unaweza kuwa unashirikiana na adui yako kiroho safi tu tena umejiachia, au ndio kushirikiana kwa tahadhari!
Namaanisha hapo kila chi ipo macho kwa mwenzake mana ukizubaa imekula kwako. Na tena unaweza kuta Marekani akawa yupo nyuma nyuma kama hajui lolote ili ajifunze mbinu za wenzake!
Na hapo Iran naye akawa anatoa mbinu dhaifu ili aonekane hajui chochote, mwisho wa siku mazoezi yanaisha, kila nchi inaanza kumchambua mwenzake kuhusu mazoezi waliyofanya.