Marekani: Jaji atengua sera ya Trump ya kuzuia visa nchi 75 ikiwemo Tanzania

Marekani: Jaji atengua sera ya Trump ya kuzuia visa nchi 75 ikiwemo Tanzania

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Jaji Jeannette Vargas wa Mahakama ya Wilaya ya Kusini mwa New York ametengua sera ya utawala wa Trump iliyosimamisha utoaji wa visa za wahamiaji kwa nchi 75, zikiwemo nchi 26 za Afrika. Jeannette amesema sera hiyo ilikuwa “kinyume cha sheria waziwazi” na kwamba ilivuka mamlaka ya Waziri wa Mambo ya Nje, Marco Rubio.

Sera hiyo ilianza kutekelezwa Januari 21, 2026, na ilisimamisha utoaji wa visa kwa madai kwamba waombaji walikuwa katika “hatari kubwa ya kuwa tegemezi kwa mifumo ya misaada ya kijamii” nchini Marekani.

Miongoni mwa nchi za Afrika zilizoathiriwa ni Nigeria, Ghana, Tanzania, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), pamoja na nyingine.

Utawala wa Rais Donald Trump uliitetea sera hiyo ukisema ilikuwa sehemu ya hatua pana za kukabiliana na uhamiaji, kwa lengo la kuzuia raia wa kigeni kutumia vibaya mifumo ya misaada ya kijamii ya Marekani.

1787563423788.png

Soma

==============

A United States judge has struck down a policy introduced by the administration of President Donald Trump suspending the issuance of immigrant visas to applicants from 75 countries, saying the policy exceeded Secretary of State Marco Rubio’s statutory authority.

Judge Jeannette Vargas of Manhattan said in her ruling on Friday in the Southern District of New York that the policy was “patently unlawful” and conflicted with federal immigration law, which explicitly stripped the secretary of state of authority over consular officers’ adjudication of immigrant visas.

“The Policy, which categorically prohibits the issuance of immigrant visas based upon the nationality of the applicant, represents a direct abrogation of this statutory scheme,” she wrote.

Vargas, an appointee of Democratic former President Joe Biden, issued the ruling in a lawsuit filed by immigrant rights groups Catholic Legal Immigration Network and African Communities Together, along with applicants for immigrant visas and US citizens sponsoring family members from the designated countries.

The suspension, which took effect in January of this year, affected applicants from Latin American countries including Brazil, Colombia and Uruguay; Balkan nations such as Bosnia and Albania; South Asian countries like Pakistan and Bangladesh; and many nations in Africa, the Middle East and the Caribbean.

The Department of State said applicants from those countries were “at a high risk for becoming a public charge and recourse to local, state and federal government resources in the United States”.


Source: Al Jazeera & DW Africa
 
Waendele, kuzuiwa watu, wasiingie nchini kwao, uku china akiendelea kuchukua usuper pawa.
China hii ambayo wananchi wake wanazamia Marekani ndiyo inachukua usuper pawa? Wewe unaweza kuzamia Uchina?
 
Back
Top Bottom