Marekani: Jakaya Kikwete ameshiriki katika Mkutano wa Mageuzi katika Elimu

Marekani: Jakaya Kikwete ameshiriki katika Mkutano wa Mageuzi katika Elimu

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Kikwete, Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia Masuala ya Elimu Duniani (Global Partnership for Education) - GPE) ameshiriki katika Mkutano wa Mageuzi katika Elimu uliondaliwa na Umoja wa Mataifa, tarehe 19 Septemba, 2022 Jijini New York, Marekani.

Katika picha; Mheshimiwa Rais Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya Global Partnership for Education) na:

1. Mhe. Dkt. Phillip Mpango, Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

2. Mhe. António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

3. Mhe. Anne Beathe Tvinnereim, Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa wa Norway

IMG-20220920-WA0015.jpg
IMG-20220920-WA0017.jpg

IMG-20220920-WA0011.jpg
IMG-20220920-WA0014.jpg
IMG-20220920-WA0016.jpg

IMG-20220920-WA0012.jpg
IMG-20220920-WA0013.jpg
 
Huyu Mheshimiwa amekidhi kabisa vigezo vya kuwekwa kwenye chungu kimoja na Vasco Da Gama, Ibn Batuta, Christopher Columbus, Bathromew Diaz, Marcopolo, na wengineo wengi.
 
Ninemuona the humble gentleman Dkt Phillip Mpango kwenye iyo picha. Pia JK mtu poa tu ila alipokosea ni kumsaliti Rais Lowasa.
 
Hivi wakiendaga huko kweli wanaleta mabadiliko kwenye mifumo yetu? Au ndo wameenda Tu.

Kama wangekuwa wanatendea kazi kwa vitendo hivyo wanavyoenda kujifunza ughaibuni basi tungekuwa mbali. Haya Vacation njema kwao
 
Shida ya Watanzania uwezo wetu wa kutumia fursa kama hizo kujiendeleza ndiyo shida inapoanzia.
Naona hapo Kuna suala la matumizi ya teknolojia kwenye Elimu,sasa mimi nasubiri kuiona hiyo teknolojia kwenye Elimu yetu.
 
Back
Top Bottom