Marekani kuipa airtime ya kutosha Wimbo mpya wa Diamond na Neyo

Marekani kuipa airtime ya kutosha Wimbo mpya wa Diamond na Neyo

BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Posts
12,320
Reaction score
11,327
Diamond Platnumz amedai wimbo wake mpya ambao haujatoka ‘Marry You’ aliomshirikisha Ne-Yo utachezwa mpaka kwenye vituo vya redio na runinga nchini Marekani.

Hitmaker huyo wa wimbo wa ‘Salome’ amesema kuwa nyimbo nyingi za wasanii wa Afrika walizowashirikisha wasanii wa Marekani zimekuwa hazichezwi nchini humo.

“Namshukuru Mungu Ne-Yo kanitunuku ni kama bahati wimbo wangu uchezwe mpaka Marekani lakini kwa wasanii wengine wanakataaga,” amekiambia kipindi cha 255 cha Clouds FM.

Tayari video ya wimbo huo imeshafanyika tangu mwezi Septemba mwaka huu huko jijini Los Angeles, Marekani lakini bado haijajulikana muda wa kuachiwa rasmi.

1478324742211.png
 
Teh teh huyu jamaa kwahiyo Msanii anayeshirikishwa ndiye anaamua kama wimbo uchezwe US? Mi nafikiri ubora wa wimbo ndicho kigezo kikubwa kama ni wimbo wa hovyo utawekwa kapuni tu!!
 
Diamond kama ameshaanza kupotea....Toka alivyoboronga kwenye MTV hakuna mtu mwenye tyme naye..
 
Diamond kama ameshaanza kupotea....Toka alivyoboronga kwenye MTV hakuna mtu mwenye tyme naye..
jamaniii mbona aibu kwa mtu mzima kuongea hivi
Ndo hivyo...Anahitaji nguvu ya ziada kuinuka...

Kitendo cha ku-perform poor kwenye MTV na kukosa tuzo ni safari tosha yeye kuanza kusahaulika kwenye game ya mziki....
kwa hiyo ronaldo alipokosa tuzo kwa miaka 4 mfululizo alikua mbovu au ?
au p square kutochukua tuzo kwamba wamepotea au hawajui

jamaniii
 
Back
Top Bottom