The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Kwa kile kinachoitwa muendelezo wa Marekani kuiwekea mbinyo China, sasa Marekani inatarajia kuziondoa kampuni zote za kichina kwenye masoko ya hisa ya Marekani kwa kutofuata kanuni za ukaguzi wa Marekani.
Kanuni za ukaguzi wa Marekani zinataka kila kampuni inayouza hisa zake Marekani ikaguliwe na CAG wake ilikuepuka udanganyifu. Miaka na miaka China imekua ikikataa kampuni zake kukaguliwa na CAG wa marekani kwa kigezo cha usalama wa Taifa
Mwaka 2013 China ikafanikiwa kuwashawishi maafisa wa utawala wa Obama wakawekeana mikataba kua CAG wa Marekani akiomba taarifa za Ukaguzi wa kampuni za China atapewa lakini toka hapo hajawahi kupewa taarifa yoyote. Mkataba huo uliomba kampuni za China kuuza hisa zake Marekani bila kukguliwa na CAG wa Marekani, kwamba zitakua zinakaguliwa na wakaguzi wa kichina na iwapo CAG wa marekani atataka taarifa atapewa.
Sasa wamarekani wengi wanasema China imekua ikipewa upendeleo usio wa kawaida kwenye masoko ya Marekani huku ikivunja sheria na kuhatarisha maslahi ya wawekezaji wa Kimarekani.
Trump anatarajia kufutahiyo MOU ya mwaka 2013 na kuzifuta kampuni zote za kichina ambazo hazikaguliwi na Marekani.
Kampuni kama Alibaba, Baidu na nyingine kubwa za Kichina zinatarajia kuondolewa kwenye masoko makubwa ya hisa kama Newyork Stock Exchange, Nasdq na mengine.
Exclusive: Trump administration to soon end audit deal underpinning Chinese listings in U.S. - official