Marekani: Makelele yazuka wakati wa hotuba ya Trump

Marekani: Makelele yazuka wakati wa hotuba ya Trump

Traxtion

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2021
Posts
8,000
Reaction score
16,414
Rais wa Marekani Donald Trump amekosolewa kwa sauti na kelele alipokuwa akitoa hotuba ya Hali ya Taifa. Wakati Warepublican wakimpa Trump shangwe za kusimama alipokuwa akizungumzia sera yake ya uhamiaji, aliwakemea wale ambao hawakusimama akisema, “Mnapaswa kuwa na aibu.”

Tukio hilo la mvutano lilitokea wakati Trump alipowahimiza wabunge kuunga mkono msimamo wa serikali ya Marekani wa kutoa kipaumbele kwa kulinda raia wa Marekani kwanza kuliko raia wa kigeni.

Baadhi ya wabunge wa chama cha Democratic, akiwemo Ilhan Omar na Rashida Tlaib, walimpigia kelele wakionyesha kutokubaliana naye.

 
Angesubutu kwenye mabunge ya afrika sasa weeeeee!!
 
Back
Top Bottom