Marekani: Mbunge apeleka muswada bungeni utakaomruhusu Donald Trump kugombania Urais kwa muhula wa 3

Kwani serikali ya US haina udhibiti wa raia kubeba bunduki?

Sijaelewa hapo
Serikali ya Marekani haina udhibiti wa bunduki wa raia kubeba bunduki, Republicans wanadai second amendment imewapa raia uhuru wa kumiliki bunduki vyovyote watakavyo kwa ajili ya kujilinda bila kufuatiliwa na serikali.

Marekani sheria ya kudhibiti pombe inakataza mtu aliye chini ya miaka 21 kununua, kuuza au kunywa pombe lakini sheria ya kununua bunduki inaruhusiwa kuanzia miaka 18. Unaweza kununua bunduki ukampa mtu kama zawadi bila utaratibu wowote wa serikali wa kufuatilia.
 
Mwisho wa siku wengi wetu tutakuja kukubaliana pamoja kuwa DEMOKRASIA ni mfumo uliowekwa mahsusi na wamagharibi ili kutuwekea mapandikizi yao ili kuendeleza ukoloni mamboleohuku AFRIKA na dunia ya tatu kwa ujumla.

Watu wote wanaweza kuwa wanasiasa ila sio kila mwanasiasa anaweza kuwa kiongozi bora. Waliolitambua hilo kama China, Rusia, etc wamewakumbatia viongozi wao wanaowapeleka mbele bila kutumia huu mfumo na maendeleo yanaonekana.

Imefikia mahali Afrika tuje na/au turudie mifumo yetu ya kiuongozi kuliko kupoteza mabilioni ya pesa, muda na wakati mwingine kuchochea vurugu hadi vifo kila baada ya miaka 4/5 kwa ujinga ule ule tu.
 
Hiyo mission ni impossible. Inahitaji 3 quarters majority in both Houses of the Congress. Where Republicans have narrow majority of 3 in both Houses.

It also needs 38 of the 50 states to vite in its favour. Mission Impossible
 
Highly unlikely lakini kuna huyu jamaa kaandika paper anasema inawezekana.

Attached.
 

Attachments


Mkuu unavyoiweka ni kama raia wa Marekani anaweza akaingia tu dukani akanunua bunduki kama mtu anavyonunua tomato paste.

Meanwhile serikali ya Marekani imeweka background checks kwenye states zote kwa mtu yeyote anayetaka kununua bunduki.

Kusema kwamba Serikali ya Marekani hai-regulate guns sidhani kama haina ukweli
 
kama unaweza kumpa mtu bunduki uliyoinunua bila Regulations zozote hiyo ni sawa na kununua tomato paste tu dukani, halafu sheria za bunduki ni za majimbo, jimbo kama Florida unaweza kuingia dukani ukanunua bunduki kama unavyonunua tomato paste tu.
 
kama unaweza kumpa mtu bunduki uliyoinunua bila Regulations zozote hiyo ni sawa na kununua tomato paste tu dukani, halafu sheria za bunduki ni za majimbo, jimbo kama Florida unaweza kuingia dukani ukanunua bunduki kama unavyonunua tomato paste tu.

Ni za majimbo yes lakini kuna federal law ina-dictate kuwa ni lazima mtu afanyiwe background checks kabla ya kununua bunduki.

Nadhani kuna states zinafanya kupuuza tu mkuu.

Democrats wangeanza kwa kufuta NRA na kuifilisi kabisa. Wenyewe ndo inawapa kiburi gunwoners.
 
Highly unlikely lakini kuna huyu jamaa kaandika paper anasema inawezekana.

Attached.

Veru unlikely lakini AIPAC na genge lake likiamua inawezekana

Najaribu kuisoma ila haifunguki mkuu au ni simu yangu?
 
Sheria za bunduki zinapuuzwa kwa sababu hazina uzito mahakamani, ziko kama mapambo tu, labda mpaka pale silaha itakapotumika kwenye uhalifu na mtu akamatwe ndio zinaweza kurejewa.

Background checks ni mtu anapoenda kununua dukani, huko mtaani kumpa mtu zawadi, kumrithisha au kumuuzia mtu kama mali yako binafsi hakuna background checks inayohitajika, watu wanapeana tu kama karanga.
 
Mbona Tanzania tayari kuna huo mfumo unaouongelea na sasa umetusaidia nini wakati umaskini ndio unaongezeka kila kukicha huku mafisadi wakila bata kwa fedha za umma.
 
Huyo chawa atauwawa na FBI na CIA muda sio mrefu
 
Wazo lako Ni zuri Sana hasa ukizingatia usaili wa mgombea ambao hufanywa kwa njia ya maneno mbali na vitendo hali inayopelekea kuwapata viongozi mahiri wa maongezi mbali na utendaji.
Lkn shida nikwamba siasa imeanza zamani za biblia na upande wangu huwa nahisi imetoka kwa Mungu kabisa
 
Kwenye vitabu vitakatifu, viongozi walikuwa wanateuliwa na Muumba halafu kizazi kinakuwa na muendelezo wa kupokezana madaraka tu. Ila hawakuwa na mfumo wa demokrasia kama ambavyo marekani na dada zake wametuletea.
 
Kwenye vitabu vitakatifu, viongozi walikuwa wanateuliwa na Muumba halafu kizazi kinakuwa na muendelezo wa kupokezana madaraka tu. Ila hawakuwa na mfumo wa demokrasia kama ambavyo marekani na dada zake wametuletea.
Hapana demokrasia ilikuwepo kumbuka kitabu samweli watu walikataa Mungu asiwaongoze Bali wanataka mtawala wanaemtaka ili wawe Kama mataifa mengine,hiyo inamaanisha hata mataifa mengine yalikuwa na mfumo huu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…