Marekani na Uingereza zaanza kuondoa raia wake Lebanon na sisi Afrika Mashariki tusizubae tena

Marekani na Uingereza zaanza kuondoa raia wake Lebanon na sisi Afrika Mashariki tusizubae tena

Kama alisema kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake, unadhani hapa atashindwa kusema kila mtu abebe mzigo wake? Ama aliyekuchilimicha ndio atakuchilimua. 😂
 
Zikiwa zimepita siku nne tangu kifo cha mkuu wa Hamas, Ismail Haniyeh kitokee, hali ya usalama katika ukanda huo si shwari huku Marekani ikiwataka raia wake kuondoka.

Tovuti ya BBC leo Jumapili Agosti 4, 2024 imeripoti kuwa: “Ubalozi wa Marekani mjini Beirut umewataka raia wake kuondoka Lebanon kwa haraka, huku mvutano ukiwa unaoongezeka Mashariki ya Kati.”

Lebanon ni miongoni mwa nchi zilizopakana na Israel ambayo ipo katika mvutano na Hamas na nchi zinazoiunga mkono Palestina.

Taarifa ya Marekani iliambatana na iliyotolewa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, David Lammy ambaye alisema hali ya kikanda, "inaweza kuzorota zaidi."

Iran imeapa kulipiza kisasi dhidi ya Israeli kufuatia kifo cha mkuu wa Hamas, pia mauaji yake yalikuja saa chache baada ya Israel kumuua kamanda wa Hezbollah, Fuad Shukr huko Beirut.

Inahofiwa kuwa, Hezbollah yenye makao yake nchini Lebanon, kundi linaloungwa mkono na Iran, linaweza kulipiza kisasi jambo litakaloongeza mvutano.
Jana Jumamosi, Hezbollah ilirusha makombora katika mji wa Beit Hillel kaskazini mwa Israel japokuwa yalidaiwa kudhibitiwa.

Picha zilizotumwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha mfumo wa ulinzi wa anga wa ‘Iron Dome’ wa Israel ukizuia roketi hizo. Hakujawa na ripoti za majeruhi.

Israel imepakana na Lebanon upande wa kaskazini, mpaka huo ulitambuliwa na Umoja wa Mataifa mwaka 2000 kama mpaka rasmi kati ya nchi hizo mbili baada ya Israel kujiondoa kutoka kusini mwa Lebanon.

 
Kufuatia viashiria vya vita kuibuka wakati wowote huko Mashariki ya Kati UK na US wameanza kuwaondoa Raia wa Lebanon na Iran

Afrika Mashariki tuungane Ili nasi tuwaondoe Raia wetu kwa haraka

Credit: BBC
Soma Pia:

Hezbollah yawahamisha haraka maofisa wake waandamizi kutokea kambi yao kuu kusini mwa Lebanon, wahofia kipigo cha ISR

John Walebanoni wa bongo siwanasema wenyewe hawana maajabu sasa watu waogope nini?Kwa hao waamerika wamepatwa na hofu ya nini?
 
Wazanzibar wengi wanaishi Lebanon na Iran.Mama atume dege letu dream liner likawachukue Hawa wazanzibar.Wazanzibari Huwa wanaona Iran,Lebanon,Syria na Iraq kama marekani Yao.
 
Back
Top Bottom