DALA
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 2,256
- 4,647
Awali ya yote natangaza wazi kwamba mimi ninaiunga mkono Urusi.
Hata hivyo, kwa mtu yeyote ambaye amefuatilia hii vita, hitimisho iko wazi. Urusi pamoja na kuchukua muda mrefu kukamilisha malengo yake tofauti na wengi tulivyodhani ukizingatia uwezo wa Urusi kijeshi, bado ushindi upo kwake.
Kiuchumi na kisiasa, Urusi inapiga hatua kubwa sana japo inakuja kwa gharama ya damu ya wanajeshi wengi na halaiki ya raia. Ila kwa kuwa hii ndiyo njia pekee waliyoina ni sahihi, hawanabudi kulipa gharama ili kuyafikia malengo yao hususani kiusalama kama walivyodai.
Narudi sasa upande wa Ukraine, nadhani Raisi wa Ukraine siyo mwanafunzi mzuri wa historia, na hiyo imempelekea yeye kufanya makosa ya kiufundi toka mwanzo wa mgogoro hata kabla ya vita. Pamoja na kwamba alitambua kuwa na jirani mbabe, mwenye nguvu kubwa kijeshi, hakuona umuhimu wa kutumia diplomasia kutatua migogoro badala yake, alikimbilia kwa rafiki wa mbali huku akitarajia msaada endapo kingenuka.
Hakukua kwamba huyu jirani yake anaogopwa hata na huyo rafiki aliyemkimbilia, hivyo rafiki yake asingeweza kujiingiza ulingoni moja kwa moja kwa kuogopa varangati.
Lakini zaidi ya yote, hakutambua kwamba rafiki yake anamtegemea adui yake kwa vitu vingi ambavyo hawezi kulubali kuvipoteza kisa yeye Ukraine ameshindwa kuyajenga na jirani. Hakutambua pia kuna uwezekano mkubwa sana adui yake akapatana na rafiki yake kidiplomasia na kuyajenga baada ya vita kama ambavyo natabiri kutokea punde tu baada ya Urusi kumaliza shughuli. Kukosa kwake Zelensky kutambua haya, kulimfanya kiburi na jeuri kwa jirani katili. Hapa sasa anavuna mbegu ya jeuri yake.
Mwanzoni mwa vita, Zelensky alitakiwa asomo alama za nyakati. Hata kabla ya vita alitakiwa awe mjanja, angefanya maamuzi yenye tija kwa taifa lake kuliko tunayoyashuhudia.
Kwamba Marekani walikuwa tayari kumtorosha aende kwao ilikuwa ni taa nyekundu. Ilionyesha kwamba Marekani hana nia ya kuingia vitani kumsaidia kwa namna yoyote ile. Pale Zelensky alitakiwa aone umuhimu wa mjadala kidiplomasia, angetumia fursa ile kwenda kwenye meza ili amalize ugomvi. Badala yake, alijihisi kuwa na marafiki wababe. Marafiki wakampa kiburi, akajionyesha kama shujaa anaenda kwenye uwanja wa vita huku amevaa magwanda, alidhani vita ni kitu cha mchezo.
Marafiki wakampamba, akapewa majukwaa ya kuhutubia mabunge, akapewa heshima na mabunge lakini maombi yake hata moja hayakupata majibu.
1. Aliomba anga ifungwe- wakasema hawawezi kuingia kwenye mgogoro moja kwa moja na Urusi. Hiyo hakuona kama taa nyekundu.
2. Akaomba apewe silaha - washirika wakuvuta sana miguu mpaka leo, hajapewa aina ya silaha ambazo zingempa angalau uwezo uwanjani.
3. Akaomba waiwekee mafuta ya Urusi vikwazo - mpaka kesho, wanaendelea kununua mafuta ya urusi.
Kimsingi, Zelensky amesalitiwa na Marekani pamoja na washirika wake.
Lakini pia Zelensky ni mpuuzi sana, kwasababu wananchi wa Ukraine hawakumchagua Joe Biden au Borris au Macron. Walimchagua Afande maamuzi ya kuwalinda na kusimamia nchi yao, ni yeye tu ndiyo mwenye maamuzi juu ya yote toka mwanzo.
Tatizo, Zelensky alikuwa mpuuzi kiasi cha kuingia vitani na silaha za kuomba, kwamba nchi yake inaenda vitani na Urusi kwa silaha za kuokoteza ni ujinga wa hali ya juu. Kwa wanaosoma historia, kuna kitabu kiliandikwa na mwanajeshi mmoja aliyepigana kwenye WW2, kuna sehemu anaeleza kwamba kilichowapa Urusi ushindi dhidi ya Ujerumani ni wingi wa wanajeshi wake, kwamba unaweza kuwaua ukadhani wameisha, mara pap unashangaa wanakuja wengine kwa maelfu. Hivyo vifo vya wanajeshi wa Urusi haimaanishi Urusi inashindwa vita hata kidogo.
Kwa sasa, ningekuwa Zelensky ningeomba poo, yaishe. Akiendeleza ujinga, nahisi Urusi itaendelea kumega ardhi ya nchi yake taratibu mpaka atakapohisi ameridhika. Kwa sasa Mataifa ya Magharibi na Marekani tayari yamegawanyika na wanaona silaha zao hazitoi matokeo ya aina yoyote chanya.
Kuanza vita ni rahisi ila kumaliza vita ni kazi zaidi.
Pole kwa Ukraine, naamini Zelensky anaelewa sasa kwamba Marekani siyo wa kumuamini na anatambua kwamba Urusi siyo Zimbabwe. Vikwazo havisaidii.