Ustadh tongwe
JF-Expert Member
- Nov 22, 2020
- 717
- 1,903
Ukraine nchi kubwa sn km umemsikia rais wa Ukraine alisema Russians wametoka 20% ya nchi ambayo ukubwa wake sawa na uholanziYukraini ni nchi ndogo? Upo timamu kweli?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ukraine nchi kubwa sn km umemsikia rais wa Ukraine alisema Russians wametoka 20% ya nchi ambayo ukubwa wake sawa na uholanziYukraini ni nchi ndogo? Upo timamu kweli?
umechambua vizuri sana, Zelensky hajali wananchi wake waliomchagua na pia hana uhakika anataka nini!Awali ya yote natangaza wazi kwamba mimi ninaiunga mkono Urusi.
Hata hivyo, kwa mtu yeyote ambaye amefuatilia hii vita, hitimisho iko wazi. Urusi pamoja na kuchukua muda mrefu kukamilisha malengo yake tofauti na wengi tulivyodhani ukizingatia uwezo wa Urusi kijeshi, bado ushindi upo kwake.
Kiuchumi na kisiasa, Urusi inapiga hatua kubwa sana japo inakuja kwa gharama ya damu ya wanajeshi wengi na halaiki ya raia. Ila kwa kuwa hii ndiyo njia pekee waliyoina ni sahihi, hawanabudi kulipa gharama ili kuyafikia malengo yao hususani kiusalama kama walivyodai.
Narudi sasa upande wa Ukraine, nadhani Raisi wa Ukraine siyo mwanafunzi mzuri wa historia, na hiyo imempelekea yeye kufanya makosa ya kiufundi toka mwanzo wa mgogoro hata kabla ya vita. Pamoja na kwamba alitambua kuwa na jirani mbabe, mwenye nguvu kubwa kijeshi, hakuona umuhimu wa kutumia diplomasia kutatua migogoro badala yake, alikimbilia kwa rafiki wa mbali huku akitarajia msaada endapo kingenuka.
Hakukua kwamba huyu jirani yake anaogopwa hata na huyo rafiki aliyemkimbilia, hivyo rafiki yake asingeweza kujiingiza ulingoni moja kwa moja kwa kuogopa varangati.
Lakini zaidi ya yote, hakutambua kwamba rafiki yake anamtegemea adui yake kwa vitu vingi ambavyo hawezi kulubali kuvipoteza kisa yeye Ukraine ameshindwa kuyajenga na jirani. Hakutambua pia kuna uwezekano mkubwa sana adui yake akapatana na rafiki yake kidiplomasia na kuyajenga baada ya vita kama ambavyo natabiri kutokea punde tu baada ya Urusi kumaliza shughuli. Kukosa kwake Zelensky kutambua haya, kulimfanya kiburi na jeuri kwa jirani katili. Hapa sasa anavuna mbegu ya jeuri yake.
Mwanzoni mwa vita, Zelensky alitakiwa asomo alama za nyakati. Hata kabla ya vita alitakiwa awe mjanja, angefanya maamuzi yenye tija kwa taifa lake kuliko tunayoyashuhudia.
Kwamba Marekani walikuwa tayari kumtorosha aende kwao ilikuwa ni taa nyekundu. Ilionyesha kwamba Marekani hana nia ya kuingia vitani kumsaidia kwa namna yoyote ile. Pale Zelensky alitakiwa aone umuhimu wa mjadala kidiplomasia, angetumia fursa ile kwenda kwenye meza ili amalize ugomvi. Badala yake, alijihisi kuwa na marafiki wababe. Marafiki wakampa kiburi, akajionyesha kama shujaa anaenda kwenye uwanja wa vita huku amevaa magwanda, alidhani vita ni kitu cha mchezo.
Marafiki wakampamba, akapewa majukwaa ya kuhutubia mabunge, akapewa heshima na mabunge lakini maombi yake hata moja hayakupata majibu.
1. Aliomba anga ifungwe- wakasema hawawezi kuingia kwenye mgogoro moja kwa moja na Urusi. Hiyo hakuona kama taa nyekundu.
2. Akaomba apewe silaha - washirika wakuvuta sana miguu mpaka leo, hajapewa aina ya silaha ambazo zingempa angalau uwezo uwanjani.
3. Akaomba waiwekee mafuta ya Urusi vikwazo - mpaka kesho, wanaendelea kununua mafuta ya urusi.
Kimsingi, Zelensky amesalitiwa na Marekani pamoja na washirika wake.
Lakini pia Zelensky ni mpuuzi sana, kwasababu wananchi wa Ukraine hawakumchagua Joe Biden au Borris au Macron. Walimchagua Afande maamuzi ya kuwalinda na kusimamia nchi yao, ni yeye tu ndiyo mwenye maamuzi juu ya yote toka mwanzo.
Tatizo, Zelensky alikuwa mpuuzi kiasi cha kuingia vitani na silaha za kuomba, kwamba nchi yake inaenda vitani na Urusi kwa silaha za kuokoteza ni ujinga wa hali ya juu. Kwa wanaosoma historia, kuna kitabu kiliandikwa na mwanajeshi mmoja aliyepigana kwenye WW2, kuna sehemu anaeleza kwamba kilichowapa Urusi ushindi dhidi ya Ujerumani ni wingi wa wanajeshi wake, kwamba unaweza kuwaua ukadhani wameisha, mara pap unashangaa wanakuja wengine kwa maelfu. Hivyo vifo vya wanajeshi wa Urusi haimaanishi Urusi inashindwa vita hata kidogo.
Kwa sasa, ningekuwa Zelensky ningeomba poo, yaishe. Akiendeleza ujinga, nahisi Urusi itaendelea kumega ardhi ya nchi yake taratibu mpaka atakapohisi ameridhika. Kwa sasa Mataifa ya Magharibi na Marekani tayari yamegawanyika na wanaona silaha zao hazitoi matokeo ya aina yoyote chanya.
Kuanza vita ni rahisi ila kumaliza vita ni kazi zaidi.
Pole kwa Ukraine, naamini Zelensky anaelewa sasa kwamba Marekani siyo wa kumuamini na anatambua kwamba Urusi siyo Zimbabwe. Vikwazo havisaidii.
achana na huyo kiaziYukraini ni nchi ndogo? Upo timamu kweli?
bila kusahau asilimia 80 iliyobaki haina amani, kila siku makombora ya urusi yanapiga hii ni kuanzia na jiji kuu la kiev, lyiv, kharkiv etcUkraine nchi kubwa sn km umemsikia rais wa Ukraine alisema Russians wametoka 20% ya nchi ambayo ukubwa wake sawa na uholanzi
Unaota dunia ya sasa sio ya Miaka ya zamani huwezi vamia nchi ya mtu ukaikalia kwa mabavu ukabaki salamaUrusi itachukua nchi ile yoye wasiposhituka.
Vijihoja dhaifu na vya kitoto sana hivi.Marekani na UIngereza wamejifunza kutoka vita vya kwanza na vya pili vya dunia. Huku nyinyi mnaenda kwenye vita yeye anarudi nyuma ndiyo kilichowatokea Russia, Germsny na wenzake ambao walikuwa super power.
Bado hamjamsoma Marekani vizuri, vita vya mihemko huwa hapigani. Ukimuona anaisaidia basi ujue kuna faida anatengeneza.
Vita ni biashara kwa bepari kama Marekani. Vita vya kupigana ili uonekane una nguvu au silaha nzito nchi zinazojielewa hawapigani siku hizi.
Pole mkuu, ni Kama naona maumivu yanayokupata🤣🤣🤣Unaota dunia ya sasa sio ya Miaka ya zamani huwezi vamia nchi ya mtu ukaikalia kwa mabavu ukabaki salama
Vita itaebdelea bila kilimo
Urusi anapigana vita ya kishamba katika dunia ya wastaarabu
Awali ya yote natangaza wazi kwamba mimi ninaiunga mkono Urusi.
Hata hivyo, kwa mtu yeyote ambaye amefuatilia hii vita, hitimisho iko wazi. Urusi pamoja na kuchukua muda mrefu kukamilisha malengo yake tofauti na wengi tulivyodhani ukizingatia uwezo wa Urusi kijeshi, bado ushindi upo kwake.
Kiuchumi na kisiasa, Urusi inapiga hatua kubwa sana japo inakuja kwa gharama ya damu ya wanajeshi wengi na halaiki ya raia. Ila kwa kuwa hii ndiyo njia pekee waliyoina ni sahihi, hawanabudi kulipa gharama ili kuyafikia malengo yao hususani kiusalama kama walivyodai.
Narudi sasa upande wa Ukraine, nadhani Raisi wa Ukraine siyo mwanafunzi mzuri wa historia, na hiyo imempelekea yeye kufanya makosa ya kiufundi toka mwanzo wa mgogoro hata kabla ya vita. Pamoja na kwamba alitambua kuwa na jirani mbabe, mwenye nguvu kubwa kijeshi, hakuona umuhimu wa kutumia diplomasia kutatua migogoro badala yake, alikimbilia kwa rafiki wa mbali huku akitarajia msaada endapo kingenuka.
Hakukua kwamba huyu jirani yake anaogopwa hata na huyo rafiki aliyemkimbilia, hivyo rafiki yake asingeweza kujiingiza ulingoni moja kwa moja kwa kuogopa varangati.
Lakini zaidi ya yote, hakutambua kwamba rafiki yake anamtegemea adui yake kwa vitu vingi ambavyo hawezi kulubali kuvipoteza kisa yeye Ukraine ameshindwa kuyajenga na jirani. Hakutambua pia kuna uwezekano mkubwa sana adui yake akapatana na rafiki yake kidiplomasia na kuyajenga baada ya vita kama ambavyo natabiri kutokea punde tu baada ya Urusi kumaliza shughuli. Kukosa kwake Zelensky kutambua haya, kulimfanya kiburi na jeuri kwa jirani katili. Hapa sasa anavuna mbegu ya jeuri yake.
Mwanzoni mwa vita, Zelensky alitakiwa asomo alama za nyakati. Hata kabla ya vita alitakiwa awe mjanja, angefanya maamuzi yenye tija kwa taifa lake kuliko tunayoyashuhudia.
Kwamba Marekani walikuwa tayari kumtorosha aende kwao ilikuwa ni taa nyekundu. Ilionyesha kwamba Marekani hana nia ya kuingia vitani kumsaidia kwa namna yoyote ile. Pale Zelensky alitakiwa aone umuhimu wa mjadala kidiplomasia, angetumia fursa ile kwenda kwenye meza ili amalize ugomvi. Badala yake, alijihisi kuwa na marafiki wababe. Marafiki wakampa kiburi, akajionyesha kama shujaa anaenda kwenye uwanja wa vita huku amevaa magwanda, alidhani vita ni kitu cha mchezo.
Marafiki wakampamba, akapewa majukwaa ya kuhutubia mabunge, akapewa heshima na mabunge lakini maombi yake hata moja hayakupata majibu.
1. Aliomba anga ifungwe- wakasema hawawezi kuingia kwenye mgogoro moja kwa moja na Urusi. Hiyo hakuona kama taa nyekundu.
2. Akaomba apewe silaha - washirika wakuvuta sana miguu mpaka leo, hajapewa aina ya silaha ambazo zingempa angalau uwezo uwanjani.
3. Akaomba waiwekee mafuta ya Urusi vikwazo - mpaka kesho, wanaendelea kununua mafuta ya urusi.
Kimsingi, Zelensky amesalitiwa na Marekani pamoja na washirika wake.
Lakini pia Zelensky ni mpuuzi sana, kwasababu wananchi wa Ukraine hawakumchagua Joe Biden au Borris au Macron. Walimchagua Afande maamuzi ya kuwalinda na kusimamia nchi yao, ni yeye tu ndiyo mwenye maamuzi juu ya yote toka mwanzo.
Tatizo, Zelensky alikuwa mpuuzi kiasi cha kuingia vitani na silaha za kuomba, kwamba nchi yake inaenda vitani na Urusi kwa silaha za kuokoteza ni ujinga wa hali ya juu. Kwa wanaosoma historia, kuna kitabu kiliandikwa na mwanajeshi mmoja aliyepigana kwenye WW2, kuna sehemu anaeleza kwamba kilichowapa Urusi ushindi dhidi ya Ujerumani ni wingi wa wanajeshi wake, kwamba unaweza kuwaua ukadhani wameisha, mara pap unashangaa wanakuja wengine kwa maelfu. Hivyo vifo vya wanajeshi wa Urusi haimaanishi Urusi inashindwa vita hata kidogo.
Kwa sasa, ningekuwa Zelensky ningeomba poo, yaishe. Akiendeleza ujinga, nahisi Urusi itaendelea kumega ardhi ya nchi yake taratibu mpaka atakapohisi ameridhika. Kwa sasa Mataifa ya Magharibi na Marekani tayari yamegawanyika na wanaona silaha zao hazitoi matokeo ya aina yoyote chanya.
Kuanza vita ni rahisi ila kumaliza vita ni kazi zaidi.
Pole kwa Ukraine, naamini Zelensky anaelewa sasa kwamba Marekani siyo wa kumuamini na anatambua kwamba Urusi siyo Zimbabwe. Vikwazo havisaidii.
Wananchi wa Ukraine wanapaswa kuwa na sauti Moja kupingana na kiongozi wao kuhusiana na vita dhidi ya Urusi!
Ama sivyo taifa lao linaenda kuwa taifa la ajabu duniani!
Urusi itachukua nchi ile yoye wasiposhituka.
Angekuwa muwazi kwenye hii vita asingefunga vyama vya upinzani na kuvizuia kufanya kazi au kutoa Naomi Yao kuvifungia vyama vya upinzani, kufunga wanaopinga hii vita na kuwaita wasaliti, kulishikilia Bunge Ayo yote ni kuonesha kwamba maamuzi alichukua kutoka Kwa watu wachache ukrein alikuwa anaweza kuzuia hii vita Kwa asilimia 90 kidiplomasia Ila naona alichukua njia tofauti kwakuisi atapata msaada kamilifu kutoka nje na saivi hawezi kurudi nyuma maana akitaka majadiliano vita akakoma wananchi hawatamuacha madarakaniUnafikiri kwa nini wananchi wa Ukraine hawajapingana na kiongozi wao mpaka sasa kwenye huu uvamizi wa Putin?
Kwa nini unafikiri wananchi wa Ukraine wanapaswa kukubali uvamizi wa Putin kwenye nchi yao?
Angekuwa muwazi kwenye hii vita asingefunga vyama vya upinzani na kuvizuia kufanya kazi au kutoa Naomi Yao kuvifungia vyama vya upinzani, kufunga wanaopinga hii vita na kuwaita wasaliti, kulishikilia Bunge Ayo yote ni kuonesha kwamba maamuzi alichukua kutoka Kwa watu wachache ukrein alikuwa anaweza kuzuia hii vita Kwa asilimia 90 kidiplomasia Ila naona alichukua njia tofauti kwakuisi atapata msaada kamilifu kutoka nje na saivi hawezi kurudi nyuma maana akitaka majadiliano vita akakoma wananchi hawatamuacha madarakani