Marekani: Siasa ya chakula!

Quickly

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
1,056
Reaction score
649
Habarini wadau,
Huwa sipatikani kwa urahisi kwenye hili forum la JF Chef. Katika pita pita zangu niliona habari ya kuvutia kutoka Marekani.
Kama mjuavyo, kuna baadhi ya nchi duniani zinazo wapa watoto chakula cha mchana bure( au kwa bei ya chini), hasa nchi tajiri. Huko Marekani First Lady Michelle Obama amekuwa na mradi yake maalum inayoitwa Healthy Hunger-Free Kids(Watoto walio na afya na bila njaa). Huo mradi ameufatilia hadi bungeni likapitishwa rasmi kwenye Congress(Bunge) ya Marekani kama Healthy Hunger-Free Kids Act ya 2010. Rais Obama ameipitisha huo mwaka.

Hata hivyo wakumponda ponda hawakosi. Wamezindua kampeni ya kumponda First Lady wakitoa mifano ya school luch zilizo bora kuliko za Marekani, kusudi kumshusha hadhi na uchapakazi wa huyo rais Obama.
Tizama picha:













(ndiyo ugiriki!!!. lile nchi lililo filisika mwaka juzi!!!)



Photos Of School Lunches From Around The World Put America To Shame
 
zaidi:

Uingereza(UK)


Taiwan


Taiwan



Chile


Ufilipino(Phillipines)


Estonia---hilo nyekundu sijui nini hilo


Brazil
 
Zaidi:

Slovakia

Slovakia


Madagascar


Nigeria


Honduras


Kenya


Kenya - hili linaitwa githeri, sawa na makande


Ghana


Uchina- aisee samaki nzima!!!


Djibouti


Ireland
 
binafsi naona la korea bora zaidi. proteini, vitamini kila kitu. Inavutia kwa macho pia.
 
natamani nikasome huko chuo...au chuo hawapewi msosi!!!
nakushauri utembee uone mengi. Mimi nimeshawahi kula konokono katika hoteli moja ya wanigeria pamoja na supu liitwalo ogbono. Korea nenda ukasome urudi ututengenezee samsung phone na tablet.
 
Hivi mnaiita mlenda pia?? Natamani utoe picha za chakula za ki asili.
Mkuu...akitoa picha za chakula cha kiasili atakuwa ameenda nje ya mada unless kama vinatumika kama lunch ya wanafunzi shuleni!
 
Hivi mnaiita mlenda pia?? Natamani utoe picha za chakula za ki asili.

Hiyo picha ilikua ni kwa hisani ya Amavubi mkuu. Huu uzi unautani lakini kuna jambo la msingi sana tunatakiwa kujifunza namna ya kuwapatia watoto wetu chakula bora shuleni. Wakati mwingine tunalalamika watoto wanauele2wa mdogo na sio wabunifu kumbe njaa na uhaba wa chakula bora nao unachangia.

Wenzetu wanawekeza mapema sana sana kwenye kumjengea mtotot uwezo kimwili na kiakili. Kama serikali itaamua kubeba gharama za ada, sio mbaya kama wazazi tutaanza kuchangia chakula cha watoto ila uwepo utaratibu na usimamizi mzuri ili mradi usijekugeuka saccos ya wajanja wachache.
 
Likumbukwe pia lishe duni kwa kiumbe yoyote inapokua linaadhiri uerevu wake(IQ) milele. Kesho naja na picha zaidi za hizi schoil lunch. Labda uone kila picha kwa makini utoe nani mshindi. Tumia kigezo cha food group zilizoko kwenye kila sahani na sio urembo wake. Kazi kwenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…