Marekani wasema tena 'hawako tayari' kusindikiza meli za mafuta katika Mlango-Bahari wa Hormuz

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
57,035
Reaction score
46,479
Wanaukumbi.

Waziri wa Nishati wa Marekani Chris Wright anasema kuwa jeshi la wanamaji la nchi yake haliko tayari kusindikiza meli za mafuta kupitia Mlango wa bahari wa Hormuz.

Hakuwa akisema hivyo Jumanne. Kwa hakika, saa 48 zilizopita, alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kwamba Jeshi la Wanamaji la Marekani lilifanikiwa kusindikiza meli ya mafuta kupitia njia kuu ya maji.

Bei ya mafuta ilishuka kutokana na habari hiyo njema, baada ya tweet hiyo kutoweka dakika chache baadaye kabla ya Ikulu ya White House kuthibitisha kwamba hapana, jeshi la wanamaji lilikuwa halijaandamana na meli iliyobeba mafuta kupitia mkondo huo.

Na bei ya mafuta ilipanda tena.
Siku ya Alhamisi, Wright aliiambia CNBC: "Itatokea hivi karibuni lakini haiwezi kutokea sasa.

Hatuko tayari. Mali zetu zote za kijeshi hivi sasa zinalenga kuharibu uwezo wa kukera wa Iran na sekta ya utengenezaji ambayo hutoa uwezo wao wa kukera."

Chanzo: BBC
 
Rais wa Cuba, Miguel Díaz-Canel, ametoa tangazo la kushtua kupitia televisheni ya taifa akibainisha kuwa serikali yake imekubali kuanza mazungumzo na Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump, hatua hii inatajwa kuwa ni matokeo ya shinikizo kubwa ambalo nchi hiyo imekuwa ikikabiliana nalo, jambo lililopelekea Cuba kubadili mwelekeo wake wa kidiplomasia ili kunusuru hali ya mambo nchini humo.

Mabadiliko haya makubwa katika sera za kigeni za Cuba yanaashiria kuanza kwa sura mpya ya mahusiano kati ya mataifa hayo mawili ambayo yamekuwa na mivutano ya muda mrefu, ingawa maelezo ya kina kuhusu makubaliano hayo bado hayajawekwa wazi, mazungumzo haya yanatarajiwa kuangazia masuala mtambuka ya kiuchumi na kisiasa, huku jumuiya ya kimataifa ikifuatilia kwa karibu kuona jinsi utawala wa Trump utakavyopokea hatua hiyo ya Havana.

Ikumbukwe siku za nyuma Trump alisema baada ya Iran Kituo kinachofuata ni Cuba anaweza kuichukua kirafiki au Kimabavu, Sasa miguel ameona atupe taulo tu bado anautaka urais wa Cuba😁

#mchululu_updates
 
Merikani na washirika wake nasikia wanajadili kujenga mfereji kama wa Suez ili ku bypass Hormuz. Kama kweli huu ujenzi itakuwa very complex na utachukua muda mrefu.
Mfereji ujengwe kutoka wapi kwenda wapi mkuu? Hapo Suez Canal palikuwa nchi kavu ndo huo mfereji ukajengwa kuunganisha mabara mawili( Asia na Ulaya). Hapa kubypass Hormuz maana yake uipasue Saudi Arabia katikati ili kujenga Canal?
 
Rais wa Cuba, Miguel Díaz-Canel, ametoa tangazo la kushtua kupitia televisheni ya taifa akibainisha kuwa serikali yake imekubali kuanza mazungumzo na Marekani chini ya utawala wa Rais Donald Trump, hatua hii inatajwa kuwa ni matokeo ya shinikizo kubwa ambalo nchi hiyo imekuwa ikikabiliana nalo, jambo lililopelekea Cuba kubadili mwelekeo wake wa kidiplomasia ili kunusuru hali ya mambo nchini humo.

Mabadiliko haya makubwa katika sera za kigeni za Cuba yanaashiria kuanza kwa sura mpya ya mahusiano kati ya mataifa hayo mawili ambayo yamekuwa na mivutano ya muda mrefu, ingawa maelezo ya kina kuhusu makubaliano hayo bado hayajawekwa wazi, mazungumzo haya yanatarajiwa kuangazia masuala mtambuka ya kiuchumi na kisiasa, huku jumuiya ya kimataifa ikifuatilia kwa karibu kuona jinsi utawala wa Trump utakavyopokea hatua hiyo ya Havana.

Ikumbukwe siku za nyuma Trump alisema baada ya Iran Kituo kinachofuata ni Cuba anaweza kuichukua kirafiki au Kimabavu, Sasa miguel ameona atupe taulo tu bado anautaka urais wa Cuba😁

#mchululu_updates
Kuongea sio kutupa taulo.

weka kumbukumbu! kamwe Marekani haitowai kuivamia Cuba. labda kutokea Mapinduzi ndani ya Cuba. kitu kisichowezekana

Sababu Usalama wa taifa wa Cuba ni namaaaa kaaaa mbaliii sana.!!

Uyu VLADIMIR PUTIN unaemjua wewe na alikuwa Mkuu wa KGB ya zamani ni zao la Cuba 🇨🇺 kama sio Cuba tusingemjua Putin,

kuipiga Cuba ni sawa na kuipiga Russia!!

kumbuka pia Cuba. ipo juu ya Usawa wa bahari!!

na Florida. ipo chini sana

Fahamu Cuba na Florida zipo karibu sana!!!!

So kuongea nikujaribu kumpumbaza mjinga mjinga km Trump mwenye kupenda sifa,,
 
Wanaukumbi.

Waziri wa Nishati wa Marekani Chris Wright anasema kuwa jeshi la wanamaji la nchi yake haliko tayari kusindikiza meli za mafuta kupitia Mlango wa bahari wa Hormuz.

Hakuwa akisema hivyo Jumanne. Kwa hakika, saa 48 zilizopita, alitangaza kwenye mitandao ya kijamii kwamba Jeshi la Wanamaji la Marekani lilifanikiwa kusindikiza meli ya mafuta kupitia njia kuu ya maji.

Bei ya mafuta ilishuka kutokana na habari hiyo njema, baada ya tweet hiyo kutoweka dakika chache baadaye kabla ya Ikulu ya White House kuthibitisha kwamba hapana, jeshi la wanamaji lilikuwa halijaandamana na meli iliyobeba mafuta kupitia mkondo huo.

Na bei ya mafuta ilipanda tena.
Siku ya Alhamisi, Wright aliiambia CNBC: "Itatokea hivi karibuni lakini haiwezi kutokea sasa.

Hatuko tayari. Mali zetu zote za kijeshi hivi sasa zinalenga kuharibu uwezo wa kukera wa Iran na sekta ya utengenezaji ambayo hutoa uwezo wao wa kukera."

Chanzo: BBC
Wanaogopa kifiro
 
Attachments

  • 2026-03-12_23-22-12_0.mp4
    941 KB
Merikani na washirika wake nasikia wanajadili kujenga mfereji kama wa Suez ili ku bypass Hormuz. Kama kweli huu ujenzi itakuwa very complex na utachukua muda mrefu.
Utajengwa eneo gani?
 
Hakuna nchi yenye uwezo wa kuthubutu kupita pale kwa hiari, au kwa jeshi bila ruhusu ya waIran wenyewe.
Trump jinga sana lilisema kuwa watapita na meli za kijeshi Maersk wakasema sisi tumefunga kupita huko😅
 
Wamechokoza mamba wakati wanaishi pembeni ya mto 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom