Marekani yaiwekea vikwazo kampuni ya programu ya Pegasu

Marekani yaiwekea vikwazo kampuni ya programu ya Pegasu

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Marekani yaiwekea vikwazo kampuni ya programu ya Pegasu

Serikali ya Marekani imeiweka kampuni ya Israel inayotengeneza programu ya udukuzi ya Pegasus kwenye orodha ya makampuni mabaya, ikiishtumu kwa kutengeneza na kusambaza programu ya ujasusi kwa serikali za kigeni, zilizoitumia vibaya kuwapeleleza waandishi habari na wanaharakati. Kampuni hiyo, NSO, ilikumbwa na kashfa kuhusiana na ripoti kwamba maelfu ya watetezi wa haki za binadamu, waandishi habari, wanasiasa na watendaji wa biashara duniani waliorodheshwa kama walengwa wa programu ya Pegasus.

Simu janja zilizoathiriwa na Pegasus hugeuzwa kuwa vifaa vya ujasusi vya mfukoni, zikiwaruhusu watumiaji kusoma ujumbe wa mlengwa, kuangalia picha zake, kufuatilia maeneo waliko na hata kuwasha camera zao pasipo wao kujua. Washington pia imeiorodhesha kampuni ya Israel ya Candiru, kampuni ya usalama wa computer ya PTE (COSEINC) ya Singapore, na Positive Technologies ya Urusi, ambazo zilituhumiwa kuuza vifaa vya udukuzi.
 
Iyo Pegasus ni hatarii. Ndio Kagame anaitumia. Pia MBS anaitumia hadi alimdukua kashoghi na familia yake. UAE falme za kiarabu inatumia sana hii program. Kagame alinichekesha aliooulizwa kama wanatumia GA iyo makitu katika ujasusi akachekaa na kujibu ni njia ya kishamba ya ujasusi Rwanda wananjia zingine siyo za kishamba kama Pegasus.
 
Unadhani ile mitambo aliyokuwa anatembea nayo kila mahali ikiwa zawadi ya kuanzisha ubalozi Israel ni ya Nini?
Waulize Membe Kinana Makamba na Nape masengenyo yao kwa Mwendazake yalipatikana vipi?😎
 
Back
Top Bottom