Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 10,509
- 16,734
Marekani inaendelea kuwa kituko katika dunia kwa kulazimika kufanya juhudi za haraka kumaliza vita ilivyovianzisha kwa tamaa ya kutanua utawala wake kupitia NATO.
Juhudi za kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine zilianza tangu utawala wa raisi Biden.Kwa sasa juhudi hizo chini ya raisi Trump zimepata kasi ya hali ya juu kiasi kwamba kuchelewa kwake kumeitia hofu Marekani yenyewe.
Itakumbukwa kwamba raisi Zelensky aliingia madarakani kupitia uchaguzi wa kidemokrasia akiungwa mkono na Marekani na mataifa ya Nato.Mataifa hayo yalimuona Zelensky kama kibaraka mzuri wa kulitikisa taifa la Urusi na kulimaliza kabisa ili sera za nato zitawale kote mashariki ya mbali.
Baada ya takriban miaka 3 bila mafanikio yoyote huku Urusi ikiendelea kuimega Ukraine.Wakati huo huo Marekani ikionekana kuishiwa na misaada yote ya kuendelea kumsaidia Zelensky.Sasa raisi Putin analazimika kutumia mbinu zote ikiwemo kumpiga chenga Zelensky ili vita vimalizike na wao wapate kupumua.
Trump katika kuchanganyikiwa na vita hivyo amekuwa akifanya mazungumzo na Putin na kumtenga Zelensky ambaye amesikika akilalamika kama mtoto yatima kuhusiana na jinsi anavyotengwa na anavyoona nchi yake ikimalizwa.
Ili vita kumalizika kwa haraka Trump amependekeza Zelenksy kuacha kabisa kudai maeneo ya thamani ambayo Putin ameshayadhibiti.
Raisi Trump akimuona Zelensky kama haeleweki na hajafahamu Marekai ilichokiona amelazimika kuwashirikisha viongozi wa mataifa ya Ulaya ndani ya ikulu ya Marekani ili wasaidie kumshika masikio Zelensky.