Kweli Mkuu,
Historia ni somo zuri, watawala wajiangalie na kujitathmini maana sasa ni Nicholas Maduro kabla ya hapo kina Jean Pierre Bemba, Manuel Noriega ...
Panama city , Panama
Kupanda na kushuka kwa Kiongozi wa Panama
Jenerali Manuel Noriega katika historia ya watawala wa Latino Amerika. Mmoja wa viongozi ktk historia wanaokumbukwa siyo kwa mazuri.
Bali jinsi Manuel Noriega alivyotawala nchi kwa kutumia 'mkono wa chuma' lakini mwisho wake akaishia jela nchini Marekani baada na kupatikana na hatia kwa kushiriki kwake ktk kupanga, kusaidia, kufadhili na kushiriki biashara ya madawa ya kulevya kujinufaisha yeye na genge lake.
Jenerali Manuel Noriega alikulia kijijini kwao karibu na mpaka wa nchini yake ya Panama na nchi jirani ya Colombia. Utotoni Noriega alipata bahati mbaya na kuugua ugonjwa wa surua ulioharibu uso wake kiasi cha kupewa jina la utani la 'uso wa tunda la nanasi' - a.k.a Lapina. Pamoja na majanga hayo alifanikiwa kujiunga na elimu ya sekondari katika shule bora ya vipaji mjini Panama city na kujifunza masomo ikiwemo humanities ( arts na history).
Source: Military learning
Ndoto zake Noriega akiwa shuleni ni kuja kuwa Psychiatrist au president wa taifa la Panama. Akiwa shuleni alianzisha kikundi cha vijana wenziwe wa kisoshalisti ili kupinga siasa za kibwanyenye na ubeberu. Noriega alijifunza kwa bidii sana masomo yake lakini hakuweza kufaulu vizuri kutimiza ndoto ya kuwa daktari maana alikuwa average student.
Pamoja ya kushindwa masomo chuoni Noriega aliweza kuajiriwa kama chemist / muuza madawa ktk duka mjini Panama city. Bahati nyingine ikamuangukia Noriega baada ya kutambulishwa kwa kaka yake wa tumbo lingine aliyekuwa anafanya kazi ubalozini mjini Lima, nchini Peru. Akamfahamisha Noriega kuna skolashipu za chuo cha Kijeshi kama atapenda kujiunga na jeshi.
Lakini Noriega alikuwa tayari ana umri wa miaka zaidi ya 20 wakati Chuo kilihitaji awe chini ya miaka 20 , kwa kutumia ujanja wa mjini Noriega aliweza kupata cheti kipya cha kuzaliwa na ghafla umri wake ukawa miaka 18 yaani miaka 4 pungufu ya umri wake halisi. Hivyo Noriega akaweza kupata skolashipu hivyo na kujiunga na chuo cha Kijeshi nchini Peru kwa mafunzo.
Baada ya miaka 4 ktk chuo hicho cha Kijeshi nchini Peru, Noriega alifanikiwa kuhitimu degree ya uhandisi na kurejea kwao Panama. Akapangiwa kazi ya kuwa surveyor. Siku moja alimtembelea rafiki yake katika kambi ya Polisi National Guards pwani ya pacific.
Bahati ya mtende ikamwangukia maana Kanali mmoja kamanda wa Jeshi la Polisi la National Guards machachari, mtoto-wa-mjini na maarufu Omar Torrijos alitembelea pia kambi hiyo ya Polisi, hivyo ghafla bin vuu surveyor Noriega akakumbana uso kwa uso na colonel Omar Torrijos. Noriega akajikuta ana stand attention kijeshi bila kujijua, Kanali Torrijos akagundua kuwa huyu kijana Noriega amepitia mafunzo ya kijeshi.
Kanali mtoto wa mjini Omar Torrijos akamwalika Noriega ktk sherehe maalum na kumshawishi ajiunge na jeshi maalum la National Guards huo ukawa mwanzo wa nyota ya Noriega kupaa kwa kasi jeshini.
Luteni Manuel Noriega akateuliwa kuwa mkuu wa intelehensia jimbo moja la Kusini la Panama. Noriega kutokana na cheo hicho alipelekwa kwa mafunzo zaidi na ripoti ya kadi ya mafunzo yake ktk maktaba ya CIA ilionesha alikuwa mwanafunzi mzuri yaliyepata alama za juu ktk somo la Psychological warfare. Somo lililokuwa muhimu katika kupambana na wapinzani wa Kikomunisti.
Omar Torrijos swahiba wake Manuel Noriega, akaongoza mapinduzi ya kijeshi nchini Panama na kukoleza vita dhidi ya mabeberu waliokuwa wanamiliki mfereji maarufu wa usafiri wa meli kubwa za baharini wa Panama canal.
Mabeberu hawakupenda sera za mapinduzi za Omar Torrijos hivyo wakapanga mapinduzi kumgoa Omar. Wakasubiri Omar Torrijos akiwa safarini Mexico na kuandaa mapinduzi ya mengine. Omar Torrijos kusikia mapinduzi hayo akamuagiza swahiba wake Kapteni Noriega kuzima jaribio hilo.
Kapteni Manuel Noriega alifaulu kuzima jaribio hilo na kufanikisha kurejea Panama Jenerali Omar Torrijos. Omar alirejea kishujaa na wakapanda gari moja la wazi pamoja na Noriega wakipita mitaani huku wakipunga mikono kwa wananchi wengi waliojitokeza kuonesha mshikamano dhini ya mabeberu.
Baada ya tukio hili la Manuel Noriega kufanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi dhidi ya Omar Torrijos mara kwa mara kiongozi huyo mwana-mapinduzi wa Panama alisikika akimwita kapteni Noriega kishikaji kama 'kichaa wangu' a.k.a gangster wangu. Na kwenda mbali zaidi Dikteta Omar Torrijos akasema Noriega anajua nini cha kufanya hata bila ya kumwambia, anachohitaji Noriega ni wao kutazamana machoni tu na tayari kila mmoja anajua nini kifanyike.
Noriega nyota yake ikazidi kupaa na akapewa cheo cha u Luteni Kanali na kuwa mkuu wa military intelligence akitambulishwa kama G -2. Kupitia wadhifa huo mpya wenye nguvu, Lt Kanali Manuel Noriega akawa masikio na macho ya Diktekta Omar Torrijos kwa Noriega kufungua mafaili ya siri kuhusu taarifa za viongozi wote ktk serikali na wale wapinzania wa diktekta huyo. Hivyo Noriega aliogopwa na wengi hata wale waliokuwa na nyadhifa kubwa kuliko Noriega.
CIA hawakuwa mbali ktk kufuatilia nyendo za Noriega na kufungua faili la siri kutunza ripoti za habari lukuki kuhusu kamanda huyu 'mzalendo' nambari moja na kutabiri siku za usoni anaweza kuwa Kamanda Mkuu wa Majeshi yote na hata kiongozi diktekta wa Panama.
Utabiri wa CIA kuhusu 'nyota' ya Manuel Noriega ulitimia baada ya ndege iliyombeba Diktekta Jenerali Omar Torrijos ilipoanguka ktk milima ya Panama mwezi Julai 1981. Uvumi kuhusu ajali hiyo ulizagaa kuwa kulikuwepo bomu ndani ya ndege na kuwa Manuel Noriega alihusika kulipenyeza humo.
Uchunguzi wa ajali hiyo ya ndege iliyopora maisha ya Jenerali Omar Torrijos ulibaini ni ajali tu ya kawaida ya ndege na siyo kama uvumi ulivyokuwa umetapakaa kuwa Noriega anahusika. Miaka miwili ya msuguano wa nani amrithi Omar Torrijos ilipita na hatimaye Manuel Noriega akaibuka kama kiongozi wa Panama. Hii ilichukua muda kutokana na viongozi waandamizi wa kijeshi na kisiasa kumuona Noriega si mwenzetu, ni 'wakuja' asiye na ushawishi wala makundi ya kumbeba kuweza kuongoza nchi kama Rais.
Baada ya utawala wake wa miaka 6 kama Kiongozi wa Panama, Jeneralia Manuel Noriega aliondolewa madarakani na jeshi la Marekani mwaka 1989 kisha kupekekwa nchini Marekani na kupatikana na hatia ya kuhusika na kushiriki katika kusaidia madawa ya kulevya kuingia Marekani. Alihukumiwa miaka 40 jela na baada ya miaka 20 aliachiwa na kufunguliwa mashtaka mengine nchini Ufaransa lakini akaachiwa na kurejea nchini Panama kufunguliwa mashitaka ya kuwapoteza wapinzani wake.
Mr. Noriega in 2011, after he was flown home to serve 20 years for the disappearances of political opponents in the 1980s.Credit...Esteban Felix/Associated Press