Marekani yaondoka nchini Afghanistan mikono mitupu baada ya vita ya miaka 20

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG111345166194.jpg

Kamanda Mkuu wa jeshi la Marekani Jenerali Kenneth McKenzie tarehe 30 Agosti alitangaza kwamba, Marekani imemaliza kuondoa vikosi vyake kutoka nchini Afghanistan, ikimaanisha kuwa, operesheni ya kijeshi ya Marekani iliyoendelea kwa miaka 20 nchini Afghanistan imemalizika rasmi. Vita hii ambayo ilianza kwa kupindua utawala wa Taliban ilimalizika kwa Taliban kuchukua madaraka tena. Wakati huohuo Marekani pia imeshindwa kutimiza lengo lake la kuangamiza ugaidi nchini Afghanistan, badala yake, makundi ya kigaidi yameongezeka nchini humo.

Tarehe 11 Septemba, mwaka 2001, magaidi waliteka nyara ndege za abiria na kugonga minara miwili ya Jengo la Biashara ya Kimataifa huko New York, ambayo ni alama ya uchumi wa Marekani, na kuua takriban watu 3,000. Karibu mwezi mmoja baadaye, Marekani ilianzisha vita dhidi ya Afghanistan kwa kisingizio cha “kupambana na ugaidi”. Wakati huo, Marekani ilikuwa na malengo mawili ya kimkakati: moja lilikuwa kuondoa utawala wa Taliban ili kuondoa "mwavuli wa kinga" wa kundi la kigaidi la al-Qaeda lililokuwa likiongozwa na Osama Bin Laden, na lingine lilikuwa kuifanya Afghanistan itekeleze "demokrasia" ya kimarekani. Lakini, miaka 20 baadaye, baada ya kulipa zaidi ya dola trilioni 2 za kimarekani kwa matumizi ya vita na maisha ya wanajeshi 2,461, Marekani imeshindwa kutimiza malengo hayo.

Awali, wakati Rais Joe Biden wa Marekani alipoeleza sababu ya uamuzi wa kumaliza vita huko Afghanistan, alisema Marekani imepata "ushindi mzuri" nchini humo, na kwamba “jeshi la Marekani limeondoa kabisa wapiganaji wanaopinga Marekani, na hawawezi kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Mareknai”. Lakini, mara tu sauti yake iliposhuka, tawi la Khorasan la Kundi la Kigaidi la IS lilifanya shambulizi kubwa la kigaidi katika Uwanja wa Ndege wa Kabul tarehe 26 Agosti, kwa kulenga wanajeshi wa Marekani waliokuwa wanaondoka, na kusababisha vifo vya watu 170, wakiwemo wanajeshi 13 wa Marekani.

Marekani imepigana na magaidi nchini Afghanistan kwa miaka 20, lakini idadi ya makundi ya kigaidi nchini humo imeongezeka hadi zaidi ya 20 kutoka chini ya 10. Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka 2001, kulikuwa na mashambulizi 20 ya kigaidi nchini Afghanistan, ambayo yalisababisha vifo vya watu 177. Lakini mawaka jana, mashambulizi 2,373 ya kigaidi yalitokea nchini humo na kusababisha vifo vya watu 6,617. Afghanistan imekuwa nchi iliyokumbwa zaidi na mashambulizi ya kigaidi duniani. Vita iliyoanzishwa na Marekani na kuwepo kwa vikosi vya nchi hiyo nchini Afghanistan kwa muda mrefu vimeleta uhasama mkubwa wa wenyeji kwa Marekani, na kuchochea kukua kwa makundi ya kigaidi. Baada ya shambulizi la Uwanja wa Ndege wa Kabul, Gazeti la New York Times la Marekani limesema, ingawa Marekani na washirika wake wamezuia makundi ya kigaidi yakiwemo IS na Al Qaeda kupata maeneo ya kujiendeleza, lakini zimeshindwa kuyazuia kuendelea kufanya mashambulizi ya kigaidi. Makundi hayo yamepata njia za kukabiliana na shinikizo kubwa la jeshi la Marekani.

Licha ya hayo, jaribio la Marekani la kukuza “demokrasia ya Kimarekani” nchini Afghanistan pia limeshindwa. Wakati jeshi la Marekani lilipoingia nchini Afghanistan, aliyekuwa Rais wa Marekani George W Bush alifuata “nadharia ya amani ya kidemokrasia”. Kwa maoni yake, utawala wa uovu, uonevu na chuki katika Mashariki ya Kati, ni vyanzo vya matishio dhidi ya Marekani, na njia ya kutokomeza vyanzo hivyo ni “demokrasia ya Kimarekani”.

Lakini sasa miaka ishirini imepita. Vita ya Marekani nchini Afghanistan imesababisha vifo na majeruhi ya zaidi ya Waafghanistan 100,000, na zaidi ya watu milioni 10 kukimbia makazi yao. Ile inayoitwa serikali ya kidemokrasia ya Afghanistan iliyoungwa mkono na Marekani imedhoofishwa na ufisadi. Kile Marekani inacholeta kwa watu wa Afghanistan sio amani na demokrasia, bali ni maumivu na uchungu usio na mwisho. Balozi wa zamani wa Marekani nchini Afghanistan Peter Michael McKinley kwenye makala yake juu ya hali ya hivi karibuni nchini Afghanistan, amesema jaribio la Marekani la kuilazimisha Afghanistan kupokea mfumo wa demokrasia ya kimagharibi limeshindwa. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema, hali ya Afghanistan inathibitisha tena kwamba mfumo wa demokrasia uliolazimishwa kupokelewa na nchi nyingine hautadumu kwa muda mrefu.

Kuanzia Vietnam hadi Afghanistan, hali halisi imethibitisha kwamba vita haitaweza kuileta Marekani manufaa kila mara. Sasa ni wakati wa Marekani kusahihisha vitendo vyake!
 
Maadui wanapopeana ushauri
Nalog off
 
Lakini kuna mwaka picha zilivuja wanajeshi wa Marekani wakilinda mashamba ya mihadarati huko Afghanstan. Inawezekana ndio kunufaika huko.

Tatizo Marekani anapiga propaganda sana. Unakuta alikuwa ana ajenda yake ya siri huko Afghanistan.
 
Itikadi ya Watelaban ni ngumu kuivunja... Ukifuatilia chimbuko lao, inasemekana mwanzoni hawakuwa na maulamaa.Ni muunganiko wa wanafunzi wakimbizi,waliokuzwa kwenye jamii zilizofuata mfumo dume,bila elimu ya darasani wala stadi za kazi Katika mazingira kama hayo,vita ilimaanisha,ajira(kazi ya kipato),amani kwao ni ukosefu wa ajira na kipato.Misingi ya itikadi kali,haikuwa tu suala la kanuni,bali ni kudumu kisiasa.
Marekani wanatambua hilo tangu Mwanzo..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Mbona sababu za US kuingia Kabul ziko wazi? Hivi mlitaka wacheke na wale magaidi? Ukisema wametoka mikono mitupu kwani mtandao wa Al Qaeda haukusambaratishwa? Nini chanzo cha kuuwawa kwa Osama kama sio hao wapiganaji waliokamatwa huko Afghanistan?
 
Mmarekani anapenda sana vita hata kama anaindoka Afghanistan bado atatafuta mahala pengine pa kufanyia uchokozi wake
 
Marekani pia imeshindwa kutimiza lengo lake la kuangamiza ugaidi nchini Afghanistan
Hoja mfu hii!

Lengo kubwa la Marekani ilikuwa kuondoa uwezekano wa mashambulizi makubwa kama lile la Sept 11 kuendelea kutekelezwa. Hakuna ubishi kuwa wamefanikiwa kwny hilo.

Kuhusu demokrasia, Taliban wenyewe wanakiri kuwa wamebadilika kwa mambo mengi sasa. Mfano, watatoa uhuru kwa wanawake kwny nyanja za masomo, ajira, nk.
Pia, wameahidi kuwa kamwe hawatokubali tena Afghanistan kuwa maficho ya magaidi wa kimataifa (global terror haven) kama mwanzo, nk.

Wametambua makosa yao, wamejifunza kwa gharama kubwa, na hawataki kusababisha kushambuliwa tena.

So, kusema Marekani imetoka mikono mitupu kabisa, si kweli
 
Lakini kuna mwaka picha zilivuja wanajeshi wa Marekani wakilinda mashamba ya mihadarati huko Afghanstan. Inawezekana ndio kunufaika huko.

Tatizo Marekani anapiga propaganda sana. Unakuta alikuwa ana ajenda yake ya siri huko Afghanistan.
Wameshaondoka na faida kubwa....
 
Mbona sababu za US kuingia Kabul ziko wazi? Hivi mlitaka wacheke na wale magaidi?
Ajabu..

Wanasahau kuwa hata Tanzania chini ya Nyerere ilipochokozwa na Iddi Amin Dada, matokeo ilikuwa ni kuingia huko Uganda na kumfurusha Dada kwa kipigo
 
View attachment 1927150
Kamanda Mkuu wa jeshi la Marekani Jenerali Kenneth McKenzie tarehe 30 Agosti alitangaza kwamba, Marekani imemaliza kuondoa vikosi vyake kutoka nchini Afghanistan, ikimaanisha kuwa, operesheni ya kijeshi ya Marekani iliyoendelea kwa miaka 20 nchini Afghanistan imemalizika rasmi. Vita hii ambayo ilianza kwa kupindua utawala wa Taliban ilimalizika kwa Taliban kuchukua madaraka tena. Wakati huohuo Marekani pia imeshindwa kutimiza lengo lake la kuangamiza ugaidi nchini Afghanistan, badala yake, makundi ya kigaidi yameongezeka nchini humo.

Tarehe 11 Septemba, mwaka 2001, magaidi waliteka nyara ndege za abiria na kugonga minara miwili ya Jengo la Biashara ya Kimataifa huko New York, ambayo ni alama ya uchumi wa Marekani, na kuua takriban watu 3,000. Karibu mwezi mmoja baadaye, Marekani ilianzisha vita dhidi ya Afghanistan kwa kisingizio cha “kupambana na ugaidi”. Wakati huo, Marekani ilikuwa na malengo mawili ya kimkakati: moja lilikuwa kuondoa utawala wa Taliban ili kuondoa "mwavuli wa kinga" wa kundi la kigaidi la al-Qaeda lililokuwa likiongozwa na Osama Bin Laden, na lingine lilikuwa kuifanya Afghanistan itekeleze "demokrasia" ya kimarekani. Lakini, miaka 20 baadaye, baada ya kulipa zaidi ya dola trilioni 2 za kimarekani kwa matumizi ya vita na maisha ya wanajeshi 2,461, Marekani imeshindwa kutimiza malengo hayo.

Awali, wakati Rais Joe Biden wa Marekani alipoeleza sababu ya uamuzi wa kumaliza vita huko Afghanistan, alisema Marekani imepata "ushindi mzuri" nchini humo, na kwamba “jeshi la Marekani limeondoa kabisa wapiganaji wanaopinga Marekani, na hawawezi kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Mareknai”. Lakini, mara tu sauti yake iliposhuka, tawi la Khorasan la Kundi la Kigaidi la IS lilifanya shambulizi kubwa la kigaidi katika Uwanja wa Ndege wa Kabul tarehe 26 Agosti, kwa kulenga wanajeshi wa Marekani waliokuwa wanaondoka, na kusababisha vifo vya watu 170, wakiwemo wanajeshi 13 wa Marekani.

Marekani imepigana na magaidi nchini Afghanistan kwa miaka 20, lakini idadi ya makundi ya kigaidi nchini humo imeongezeka hadi zaidi ya 20 kutoka chini ya 10. Takwimu zinaonesha kuwa, mwaka 2001, kulikuwa na mashambulizi 20 ya kigaidi nchini Afghanistan, ambayo yalisababisha vifo vya watu 177. Lakini mawaka jana, mashambulizi 2,373 ya kigaidi yalitokea nchini humo na kusababisha vifo vya watu 6,617. Afghanistan imekuwa nchi iliyokumbwa zaidi na mashambulizi ya kigaidi duniani. Vita iliyoanzishwa na Marekani na kuwepo kwa vikosi vya nchi hiyo nchini Afghanistan kwa muda mrefu vimeleta uhasama mkubwa wa wenyeji kwa Marekani, na kuchochea kukua kwa makundi ya kigaidi. Baada ya shambulizi la Uwanja wa Ndege wa Kabul, Gazeti la New York Times la Marekani limesema, ingawa Marekani na washirika wake wamezuia makundi ya kigaidi yakiwemo IS na Al Qaeda kupata maeneo ya kujiendeleza, lakini zimeshindwa kuyazuia kuendelea kufanya mashambulizi ya kigaidi. Makundi hayo yamepata njia za kukabiliana na shinikizo kubwa la jeshi la Marekani.

Licha ya hayo, jaribio la Marekani la kukuza “demokrasia ya Kimarekani” nchini Afghanistan pia limeshindwa. Wakati jeshi la Marekani lilipoingia nchini Afghanistan, aliyekuwa Rais wa Marekani George W Bush alifuata “nadharia ya amani ya kidemokrasia”. Kwa maoni yake, utawala wa uovu, uonevu na chuki katika Mashariki ya Kati, ni vyanzo vya matishio dhidi ya Marekani, na njia ya kutokomeza vyanzo hivyo ni “demokrasia ya Kimarekani”.

Lakini sasa miaka ishirini imepita. Vita ya Marekani nchini Afghanistan imesababisha vifo na majeruhi ya zaidi ya Waafghanistan 100,000, na zaidi ya watu milioni 10 kukimbia makazi yao. Ile inayoitwa serikali ya kidemokrasia ya Afghanistan iliyoungwa mkono na Marekani imedhoofishwa na ufisadi. Kile Marekani inacholeta kwa watu wa Afghanistan sio amani na demokrasia, bali ni maumivu na uchungu usio na mwisho. Balozi wa zamani wa Marekani nchini Afghanistan Peter Michael McKinley kwenye makala yake juu ya hali ya hivi karibuni nchini Afghanistan, amesema jaribio la Marekani la kuilazimisha Afghanistan kupokea mfumo wa demokrasia ya kimagharibi limeshindwa. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema, hali ya Afghanistan inathibitisha tena kwamba mfumo wa demokrasia uliolazimishwa kupokelewa na nchi nyingine hautadumu kwa muda mrefu.

Kuanzia Vietnam hadi Afghanistan, hali halisi imethibitisha kwamba vita haitaweza kuileta Marekani manufaa kila mara. Sasa ni wakati wa Marekani kusahihisha vitendo vyake!
Wakati fulani tunaweza kuacha ushabiki tukatembea na uhaliasia. Hivi ni kweli Marekani hawakupata walichokiendea Afuganstan! Tunayo ya kujiuliza ,moja ni Alkaeda ipo! Na kama ipo kwa ukubwa gani? Lakini pia je viongozi wake na makamnda wake wapo? Je mfumo wa Alkaeda hajavunjwa? Tukipata majibu ya hayo km ni ndiyo hapo tunaweza kusema Us hawakupata kitu
 
Hoja mfu hii!

Lengo kubwa la Marekani ilikuwa kuondoa uwezekano wa mashambulizi makubwa kama lile la Sept 11 kuendelea kutekelezwa. Hakuna ubishi kuwa wamefanikiwa kwny hilo.

Kuhusu demokrasia, Taliban wenyewe wanakiri kuwa wamebadilika kwa mambo mengi sasa. Mfano, watatoa uhuru kwa wanawake kwny nyanja za masomo, ajira, nk.
Pia, wameahidi kuwa kamwe hawatokubali tena Afghanistan kuwa maficho ya magaidi wa kimataifa (global terror haven) kama mwanzo, nk.

Wametambua makosa yao, wamejifunza kwa gharama kubwa, na hawataki kusababisha kushambuliwa tena.

So, kusema Marekani imetoka mikono mitupu kabisa, si kweli

Ni kweli lengo kuu lilikuwa kuisambaratisha Al Qaeda,lakini hujamalizia "kuhakikisha Afghanistan haiwi tena Breeding ground/safe heaven ya Magaidi"..kinyume chake..kwa sasa kuna vikundi vingi sana hatarishi huko..
Baada ya Taliban kukataa kumtoa OBL bila masharti nao wakaunganishwa kwenye mission ya kuwaeliminate kabisa..Kinyume chake tumeona..
Licha ya OBL kuuawa 2011, bado US iliendelea kubaki kwa kuwa mission haikuwa fully accomplished ..
Kuhusu Taliban kusema wamebadilika..ni mapema sana(japo natamani iwe hivyo)..
Unatambua baraza limetangazwa na hakuna hata mwanamama mmoja..?
Kama kweli "wamebadilika" ni kwanini mpaka sasa Jumuiya nyingi za Kimataifa inasita kuwatambua..ukiachana na washirika wachache waliokuwa nao bega kwa bega tangu nyuma(Qatar,Pakistan Nk)..
Ni failed mission tukubali tukatae..

Sent from my SM-A405FN using JamiiForums mobile app
 
Mbona sababu za US kuingia Kabul ziko wazi? Hivi mlitaka wacheke na wale magaidi? Ukisema wametoka mikono mitupu kwani mtandao wa Al Qaeda haukusambaratishwa? Nini chanzo cha kuuwawa kwa Osama kama sio hao wapiganaji waliokamatwa huko Afghanistan?
Na hata sasa US, amesema licha ya kutoka huko lakini hata kubali kuona inakuwa tena sehemu ya maficho ya magaidi, nadhani hata taliban hawatakubali hali hiyo, kwani na wao kwa miaka 20 wameishi maisha ya tabu sana!!kwani wakiruhusu hilo US, anaweza kuwa anawashambulia kwa kutokea angani tu, na kwa sasa itakuwa hata rahisi kwa viongozi wa taliban kuuawa, kwani watajulikana sasa wako jengo gani, wanaishi wapi!!tofauti na hapo zamani walipokuwa wakiishi kwa kujuficha!!ila hao magaidi waliokuwa wanatafutwa na US, waliopewa uongozi cjui kama atawaacha tu, kuna kitu tu atakifanya ili kuwamaliza!!sasa hivi anawaunga mkono ili raia wake, waliobakia huko watoke, zile ndege za kiraia nazo zitoke huko, ndio aanzishe zengwe.kwani sioni ni namna gani hiyo serikali itakuwa ikijiendesha bila kupata misaada toka nje, sio umtegemee mrusi na mchina!!!
 
Back
Top Bottom