Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken amesema Washington inapania kuchukua hatua mpya ili kushinikiza utawala wa jeshi nchini Myanmar kurudisha serikali ya kiraia, katika wakati ambapo wasiwasi unazidi kuongezeka kutokana na kukandamizwa wapinzani.
Akizungumza wakati wa ziara nchini Malaysia, Blinken amekiri kuwa hali nchini Myanmar bado ni mbaya.
Marekani imeiwekea baadhi ya vikwazo utawala wa jeshi nchini Myanmar, huku Jumuiya ya mataifa ya kusini mashariki mwa Asia ikipendekeza mpango wa kukomeshwa kwa vurugu nchini humo japo kuna mashaka juu ya kujitolea kwa utawala wa jeshi kukomesha vurugu. Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa ulitahadharisha juu ya ongezeko la visa vya ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Myanmar.