Mkuu, kinacho endelea hapa ni kutafuta mbinu za kufuja fedha za walipa kodi wa Amerika kwa kupitia kisingizio cha kuisaidia Ukraine, Bunge la Amerika lina idhinisha fedha chungu mzima, lakini nyingi ya fedha hizo zinaishia mifukoni kwa viongozi wajanja pamoja na wamiliki wa viwanda vya kuunda Silaha huko Merikani pia na baadhi ya wabunge na Biden anajuwa sana kuhusu michongo hii ya upigaji fedha ndefu kwa kuwa yeye na familia yake nao wananufahika na michogo hii. Kinacho sikitisha fedha taslimu zinazo kwenda kuwasaidia raia wa Ukraine ni ndogo sana.
Ndio maana nasema kwamba kutokana upigaji fedha ndefu huu, kuta sababisha uwezekano wa vita hii kuisha kuwa ni mdogo sana - kama nilivyo sema tangu mwanzo US inataka sana a-prolong vita hii ili viwanda vya silaha vipige hela ndefu, baadhi ya wabunge na mwanae Biden anaye julikana kwa jina la Hunter nae apatiwe mshiko/mgao kwa kuwa yuko karibu sana na Rais Zelensky kibiashara(kampuni ya mafuta na gesi Ukraine), narudia kukumbusha kwamba mpaka vita hii iishe Ukraine itakuwa imechakazwa sana na watu wengi kupoteza maisha. Sasa sijui kwa nini Zelensky hatumii busara na hekima ya kukaa meza moja na Putin wakamaliza tofauti zao kwa lengo la kuinusuru Ukraine na Raia wake.