Marekani yatoa msaada wa Kijeshi wa Bilioni 627 kwa Ukraine

Russia nae aache tu vita maana atadhoofika hayo mataifa yote anayopambana nayo yana nguvu kiuchumu na yeye Russia kaingia kichwa kichwa tu,
Russia hii vita itamgharimu zaidi,
Aache asipoteze wanajeshi wake na fedha ataanguka kiuchumu.
Russia sio Zimbabwe , tulia tuli
 
Russia napenda aendelee kuwepo na awe strong zaidi, kubalance ubabe hapa kwenye sayari yetu pendwa. ila akiendelea ataumia maana jamaa wao vita hawataiacha, Marekani ndio kazi yake kazoea kupiginisha vita atakuwa na Experience kubwa zaidi.
 
Somalia ukipeleka trilioni 1 tu uneokoa maisha ya watu wengi sana wanaokufa kwa njaa kuliko kupeleka vitani ambako unaweza kupata hasara.
Ni kweli mkuu lakini hao watu, UN Marekani alienda kuwasaidia miaka ya 1992 wakati wa Muhammad Farrah Aydid aliekuwa wa Somalia National Alliance (SNA) wakawa wamewapunguza nguvu unapigana na vijana ambao mama zao wamewaficha ya nini sasa. Na wakati huo kulikuwa na vikundi vinavyopiga na serikali kama vinne, wengine ndio wapo pale somalia mashariki wamejikatia eneo wanajiita somali land.

Somalia mpaka wajitambue halafu kuna dini fulani ikiwa huku Africa ni usumbufu tu.
Marekani nae kaona nchi hata haina masirahi akaondoka.
 
Urusi sio wa kumuamini, jana kasaini chakula kisafirishwe leo kaanza lipua bandari
 
Somalia ukipeleka trilioni 1 tu uneokoa maisha ya watu wengi sana wanaokufa kwa njaa kuliko kupeleka vitani ambako unaweza kupata hasara.
Somalia ni uzembe wao kutolima, Ukraine biashara inafanyika hapo
 
Umoja wa Africa (AU) wapeleke hiyo pesa
Somalia ukipeleka trilioni 1 tu uneokoa maisha ya watu wengi sana wanaokufa kwa njaa kuliko kupeleka vitani ambako unaweza kupata hasara.
 
Russia iwasaidie hizo pesa
Hii dunia hii WHO si walisema wanahitaji dola bilion 6 tu kumaliza njaa, huku wanatumia dola bilioni 8.2 kuendeleza vita
[emoji23][emoji1787]
 
Misaada ya U.S kwa Ukraine inapotea paspo kufanya kazi,

Waambie walete summary ya matumizi ya apo awali tuone kama wanayo
 
Putin nimemkubali, kweli jamaa jembe,
Yaani hii sijui ni mara ya ngapi jamaa wanatuma na putin anapukutisha tu
Z
Mkuu, kinacho endelea hapa ni kutafuta mbinu za kufuja fedha za walipa kodi wa Amerika kwa kupitia kisingizio cha kuisaidia Ukraine, Bunge la Amerika lina idhinisha fedha chungu mzima, lakini nyingi ya fedha hizo zinaishia mifukoni kwa viongozi wajanja pamoja na wamiliki wa viwanda vya kuunda Silaha huko Merikani pia na baadhi ya wabunge na Biden anajuwa sana kuhusu michongo hii ya upigaji fedha ndefu kwa kuwa yeye na familia yake nao wananufahika na michogo hii. Kinacho sikitisha fedha taslimu zinazo kwenda kuwasaidia raia wa Ukraine ni ndogo sana.

Ndio maana nasema kwamba kutokana upigaji fedha ndefu huu, kuta sababisha uwezekano wa vita hii kuisha kuwa ni mdogo sana - kama nilivyo sema tangu mwanzo US inataka sana a-prolong vita hii ili viwanda vya silaha vipige hela ndefu, baadhi ya wabunge na mwanae Biden anaye julikana kwa jina la Hunter nae apatiwe mshiko/mgao kwa kuwa yuko karibu sana na Rais Zelensky kibiashara(kampuni ya mafuta na gesi Ukraine), narudia kukumbusha kwamba mpaka vita hii iishe Ukraine itakuwa imechakazwa sana na watu wengi kupoteza maisha. Sasa sijui kwa nini Zelensky hatumii busara na hekima ya kukaa meza moja na Putin wakamaliza tofauti zao kwa lengo la kuinusuru Ukraine na Raia wake.
 
Well said,
Lile jamaa si ni likomedi ndio maana
 
Hiyo minoti wanapeleka wapi?
Mbina hawalindi anga lao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…