Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Ikitaja uwezekano wa kuwanyanyasa raia wa Marekani, onyo hilo linarudia wito kwa Wamarekani kutosafiri kwenda Urusi au kuondoka "mara moja". Pia ilionya Wamarekani kuhusu "utekelezaji holela wa sheria za mitaa".
Ushauri huo pia ulisema kulikuwa na ripoti zinazoendelea za raia wa Marekani "kutengwa na kuzuiliwa na jeshi la Urusi" wanapokuwa Ukraine, au wanapohama kwa ardhi kupitia eneo linalokaliwa na Urusi.
"Ikiwa unataka kuondoka Urusi, unapaswa kufanya mipango peke yako haraka iwezekanavyo,"onyo hilo lilisema. Marekani ilisimamisha ubalozi wake na ubalozi mdogo nchini Ukraine siku chache baada ya Rais Putin kutangaza uvamizi wake.
BBC Swahili