Marekani yaungana na Russia, Korea Kaskazini na Belarus kupinga azimio la Umoja wa mataifa kulaani uvamizi wa Russia

Marekani yaungana na Russia, Korea Kaskazini na Belarus kupinga azimio la Umoja wa mataifa kulaani uvamizi wa Russia

Hakika hizi ni zama mpya, Marekani imeungana na mataifa kadhaa ya hovyo kupinga azimio la baraza la usalama la Umoja wa mataif(UN) lililowasilishwa na Umoja wa Ulaya kulaani uvamizi wa Russia nchini Ukraine na kuitaka iondoe majeshi yake Ukraine.

Hata hivyo azimio hilo limepita kwa wingi ws kura 93 dhidi ya 18 zilizopinga ikiwemo US huku mataifa 65 yakiharibu kura zao.
View attachment 3248382
Trump kaitosa Ukraine na washirika wake wa Ulaya hadharani.
 
fanyen uislam kuwa dini ya amani ili USA mnaedai anafadhiri ugaid akose chaka
Ni wewe tu na mawazo yako, dini inajielexa..Mtu kama mweupe ukitaka kumchafua unampala rangi nyeusi.

Fikiria mara mbili!
 
Trump anaweza kuigeuza Marekani kuwa nchi ya kikomunisti huyu jamaa. Wamwangalie sana.
Huyu Mzee anaichukia sana China ila 'role model' wake ni Putin...... anafanya yote hayo akiamini ataweza kuugeuza Ushawishi wa Urusi kutoka China kurudi kwa US, amesahau kuwa taifa lake (US ) na Urusi ni mahasimu wa kihistoria.
 
Huyu Mzee anaichukia sana China ila 'role model' wake ni Putin...... anafanya yote hayo akiamini ataweza kuugeuza Ushawishi wa Urusi kutoka China kurudi kwa US, amesahau kuwa taifa lake (US ) na Urusi ni mahasimu wa kihistoria.
US na Russia ni mahasimu kweli, lakini wote ni superpowers wa Dunia.

Pili, wote wana silaha za Nyuklia ambazo kila mmoja alitengeneza kwa siri wakati wa vita kuu ya pili ya Dunia.

Tatu, US na Russia ni washirika wa kistratejia na ndo maana leo Putin kasema Russia ipo tayari kutumia kwa pamoja raslimali (malighafi) zilizopo Ukraine.

Nne, wote wana idara za Ujasusi wa hali ya juu ulimwenguni na wamepeana ruhusa ya kuwa na maofisa ujasusi katika nchi zao na makazi rasmi ya balozi na ofisi za kijasusi. Hii ni kwa wao tu na nchi zingine hazina ruhusa hiyo.

Tano, Russia tayari iko juu kwa utengenezaji aina tofauti za silaha na kazitumia zote pale Ukraine na zafanya kazi kwa ufanisi wa hali ya juu.

Kwenye hili, Russia kashinda SMO yake Ukraine na itabidi EU na NATO wakubali kwani ni lazima wakubaliane na usitishwaji wa vita ya Ukraine kwa masharti ya Russia.
 
Wewe unaijua North Korea. North Koreani nchi ya hovyo sana. Maisha yao huenda ni mabaya kuliko jehanamu!!

Wastani wa mshahara kwa north Korea ni kati ya dola 1 na dola 3 kwa mwezi. Hakuna nchi ya namna hiyo nyingine Duniani.

What is the salary in North Korea?

Official Salaries and Real Value

Official salaries in North Korea are very low, typically ranging between 5,000 and 10,000 won per month (equivalent to $1-$3). These salaries are insufficient to meet basic needs, forcing most citizens to rely on the informal market for essential goods.

Sisi pamoja na umaskini wetu, lakini tunawazidi GDP mpaka GDP per capita:

North Korea vs Tanzania: Economic Indicators ComparisonTanzania with a GDP of $58B ranked the 80th largest economy in the world, while North Korea ranked 89th with $43.3B. By GDP 5-years average growth and GDP per capita, Tanzania and North Korea ranked 18th vs 172nd.
Duh ila nchi yetu ni fukara aiseeeee..GDP ya 58 billion USD…..?

Utaambiwa tuna maliasili kibao. Ila sasa hatuna uwezo wa kuzisimamia na kuzibadili kwenye uhalisia wa pesa.
 
wewe akili kumbe huna!
NK ana vikwazo, hivyo biashara nyingi anafanya kimagendo so huwezi jua GDP yake kwa sababu huna takwimu halisi....

nchi inatengeneza rocket, satelite, nyuklia, silaha za kila aina, nyambizi, afu unalinganisha na gdp ya tz?

sijui kwanini mnapojadili haya mambo huwa mnajitoa akili, au ndio kuwa brainwashed?

Hata mimi nimemshangaa huyo jamaa, NK kila siku inazindua ICBM na very successful alafu anataka kujilinganisha na sisi hadi risasi tunanunua, kweli propaganda za magharibu zimearibu watu wetu
 
Hakika hizi ni zama mpya, Marekani imeungana na mataifa kadhaa ya hovyo kupinga azimio la baraza la usalama la Umoja wa mataif(UN) lililowasilishwa na Umoja wa Ulaya kulaani uvamizi wa Russia nchini Ukraine na kuitaka iondoe majeshi yake Ukraine.

Hata hivyo azimio hilo limepita kwa wingi ws kura 93 dhidi ya 18 zilizopinga ikiwemo US huku mataifa 65 yakiharibu kura zao.
View attachment 3248382
Wamarekani wanamlaumu Sana Donald Trump kwa Uamuzi wake huu.

Hata baadhi ya Maseneta kutoka katika Chama chake cha Republican pia wanamlaani Sana kwa jambo hili.
 
Sikujua kuwa Rais wa US ana power kubwa mno kiasi cha ku-influence foreign policy na kuigeuza nyuzi 180! Power ambayo nailinganisha na dictatorship.
Udikteta kivipi wakati katiba yao ndio imempa Rais mamlaka makubwa katika sera za mambo ya nje, ubalozi, majeshi na ujasusi wa nje ya nchi??
 
US anahiitaji sana NATO ktk operation zake nyingi tu za kijeshi Trump sijui kaona Nini.
Hapana. Ulaya ndiyo inaihitaji US mno katika masuala ya ulinzi. Ndio maana UK naye kapunguza kiwango cha misaada inachotoa ili kuongeza bajeti ya ulinzi baada ya kuona ulinzi wa US una mashaka.
 
Back
Top Bottom