Marekani yaziondoa Ethiopia, Mali na Guinea kwenye Mfumo wa AGOA

Marekani yaziondoa Ethiopia, Mali na Guinea kwenye Mfumo wa AGOA

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Serikali ya Marekani imeanza rasmi kutekeleza agizo la Rais Joe Biden la kuziondowa Ethiopia, Mali na Guinea kutoka makubaliano ya kibiashara kati ya taifa hilo na Afrika kutokana na uvunjwaji wa haki za binaadamu.M

Marekanihivi leo imeziondosha Ethiopia, Mali na Guinea kutoka kwenye programu ya biashara ya AGOA kutokana na vitendo vya kila serikali kwenye kuvunja Mkataba wa AGOA," ilisema Ofiis ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani kwenye taarifa yake iliyotolewa siku ya Jumamosi (Januari Mosi).

Mkataba uliopewa jina la Sheria ya Ukuwaji wa Uchumi na Fursa Barani Afrika (AGOA) ulianza kufanya kazi mwaka 2000 chini ya utawala wa rais wa wakati huo wa Marekani, Bill Clinton, kuwezesha na kusimamia biashara kati ya Marekani na Afrika.

Lakini taarifa hiyo inasema Marekani "inatiwa wasiwasi sana na mabadiliko ya serikali yanayokwenda kinyume na katika nchini Guinea na Mali na uvunjwaji mkubwa wa haki zinazotambuliwa kimataifa za binaadamu unaochochewa na serikali ya Ethiopia na pande nyengine wakati mzozo ukiongezeka kaskazini mwa Ethiopia."

"Kila nchi ina jukumu la wazi la kufuata njia ya kurejeshwa kwenye AGOA na serikali ya Marekani itashirikiana na serikali zao kufikia lengo hilo," ilisema taarifa hiyo ya Mwakilishi wa Biashara wa Marekani.
 
Nashangaa Tanzania bado hawajashushiwa shoka kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, kubambikia watu vyesi feki na kukataa kufanya uchaguzi na badala yake kubaki kufanya uhuni kwenye vituo vya kupigia kura.
 
Us nijinamizi la shida na machafuko mengi katika nchi nyingi maskini duniani.
 
Back
Top Bottom