Tatizo ni mikataba uchwara tunayoingia na hawa wazungu koko kwa kudhania kuwa wanatuthamini.
Daima, mzungu koko yeyote anaangalia maslahi yake mfano, ukiona mzungu koko anakupatia kitu bure au kwa bei ndogo unatakiwa uwe makini sana. Niandike hivi ili tuelewane, yaani mzungu koko anakuwa tayari ameishaona eneo la kukubana siku zote za maisha yako .
Sasa angalia, mkataba Kama huo, tena tunaanza kuonywa Kama vitoto vidogo vya chekechea.
Mfano. Trump, amesema USA itajitoa kwenye Paris Climate change agreement, na hakuna nchi ya Africa inayotoa uchafu wa viwanda kwenye anga Kama USA, ulaya na Asia ndiyo wachafuzi.
Sasa, hapo USA yeye ameona atapata hasara na nchi hizo za ulaya na Asia hataweza kupata faida yeyote kwenye hii agreement ndiyo maana anataka kujitoa. Ila jambo kubwa ni kwamba, hakuna faida atakayoipata kutoka kwenye hili jambo la climate change.
Africa, tulijisahau sana katika mikataba, makubaliano ya kirafiki na n.k. sasa wazungu koko wakaona hapo ndipo pa kuponea.
Ila, tunahitaji kusimama kidete na kukataa huu upuuzi wa wazungu koko, bila hivyo tutakuwa soko la wazungu koko hadi mwisho wa Dunia.
Hii naweka Kwa manufaa ya wote humu JF wenye akili waelewe
Baba yangu mzazi, siku moja akanifundisha jambo hili akasema:-
"Mwanangu, #Poise# Uwe makini sana, pale mzungu koko, atakapo kupatia Zawadi hata ndogo sana kama bic"/pen. Ukiipokea tu, ni lazima pana siku utaandika makubaliano Kwa kutumia pen ✒ ✒ aliyokupatia Kama Zawadi, mkataba au makubaliano ambayo yatakuwa na faida kwake kwa wakati huo au siku zote za maisha yao.
Maana, kitu chochote kutoka kwa mzungu koko akitoacho huwa anategemea kupata faida maradufu"
Yaani mzungu koko ni sawa kabisa na nyani "maana ukicheka na nyani utavuna mabua"