Marekani yazitisha nchi za Afrika zisinunue mafuta ya Urusi

Marekani yazitisha nchi za Afrika zisinunue mafuta ya Urusi

Diversity

Senior Member
Joined
Oct 21, 2019
Posts
139
Reaction score
230
Picha.jpg
Marufuku Afrika kununua Mafuta Urusi
Kupitia ziara ya Balozi wa Marekani Linda Thomas katika mahojiano kuhusu nchi za Afrika alitaka kutafuta masuluisho ya migogoro bila kutoa lawama kwa nchi za Afrika ambapo zimeathirika na vita ya Urusi zidi ya Ukraine.

Baada ya kufika Uganda aliziionya nchi za Afrika kuwa kuna mstari au mipaka wanatakiwa wasivuke kabisa ambapo alisema Afrika zinaweza kununua mambo mbalimbali ikiwemo mbolea, mazao na mambo mengine yanayohusu kilimo na ufugaji. Lakini nchi za Afrika zitazo jihusisha na biashara ya mafuta na Urusi hakika watakuwa wamevuka mipaka na makubaliano. Ambapo mwezi wa tatu, 2022 Marekani walizuia ununuzi wa Mafuta na Gesi kutoka Urusi.

Nchi nyingi za Afrika zimekaa mbali wamejaribu kukaaa mbali kuhusu vita ya Urusi japokuwa vita imesababisha mfumuko wa bei za mafuta na bidhaa nyingine na kusababisha anguko la kiuchumi baadhi ya nchi za Afrika. Kutokana na ripoti ya shirika la Humanitarian aid organization Zaidi ya watu milioni 100 hawana chakula cha kutosha na zaidi ya watu milioni wapo katika hatari ya kufariki kutokana na janga la njaa.

Kwakupitia ukurasa wa twitter Rais wa Uganda Yoweri Museven alichapisha chapisho kwa kusema kama kweli wanataka kutusaidia Afrika basi watutoe kwenye vikwazo amapo vita haituhusu sisi Afrika bali ni wao wenyewe mataifa makubwa Duniani.
 
Back
Top Bottom