Marekani yazuia Tanzania misaada ya trilioni 1

Marekani yazuia Tanzania misaada ya trilioni 1

Msulibasi

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2014
Posts
5,947
Reaction score
7,939
Vitendo vya rushwa vimeendelea kuligharimu taifa baada ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC) kuzuia misaada yake kwa Tanzania yenye thamani ya dola za Marekani milioni 472.8 (Sh. trilioni 1.006).

Taarifa iliyotolewa jana na MCC ilieleza kuwa mkutano wa robo ya mwaka wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika hilo linalomilikiwa na serikali ya Marekani kwa ajili ya kutoa misaada kwa nchi zinazoendelea ulijadili pendekezo la mkataba mpya na serikali ya Tanzania wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 472.8 na kuamua kuwa fedha hizo zitolewe baada ya Tanzania kutimiza kigezo cha kuzuia rushwa. Ilielezwa kuwa msaada huo ni maalum kwa ajili ya kuimarisha sekta ya umeme nchini, lengo likiwa ni kuwawezesha Watanzania wengi zaidi kupata nishati hiyo kwa uhakika na kwa bei nafuu.

Kadhalika, ilieliezwa kuwa msaada huo ungehusisha pia uimarishaji wa taasisi zinazohusika na usambazaji wa umeme na usimamizi wake, kusaidia utekelezaji wa mipango ya mageuzi katika sekta ya nishati na kuchochea uwekezaji wa sekta binafsi.

Hata hivyo, taarifa hiyo inaeleza kuwa baada ya mkutano huo uliofanyika juzi (Septemba 17), Bodi ya Wakurugenzi wa MCC ilitoa taarifa rasmi ya kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa kufanya mageuzi muhimu kama sehemu ya maandalizi ya utekelezaji wenye ufanisi wa mkataba, lakini haitapewa msaada huo hadi itakapofaulu kigezo cha kiashiria cha kuzuia rushwa (Control of Corruption indicator).

"Pamoja na kutambua mageuzi hayo, Bodi iliendelea kuelezea wasiwasi wake kuhusu hali ya rushwa nchini Tanzania na kukubaliana kwamba ni lazima kwanza Tanzania ifaulu kufikia kigezo cha udhibiti wa Rushwa (Control of Corruption indicator) katika tathmini ya mwaka 2016 ya jinsi nchi husika zinavyokidhi vigezo vya kusaidiwa na MCC," inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, taarifa hiyo ilimkariri Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Mark Childress, akisema kuwa wanafurahishwa na jitihada za serikali ya Tanzania kuinua ufanisi katika sekta ya nishati lakini bado kuna kazi ya kufanywa kwani tatizo la rushwa linaendelea kuathiri karibu kila nyanja."Tunafurahishwa na jitihada za Tanzania katika miezi kadhaa iliyopita za kufanya mageuzi ya kimuundo na kitaasisi ili kuinua ufanisi, tija na uwazi katika sekta ya nishati.

Hata hivyo, kama ambavyo Bodi ya MCC imebainisha, pamoja na jitihada kadhaa zilizochukuliwa kukabiliana na rushwa, bado tatizo hili limeendelea kuwa kubwa likiathiri nyanja zote za maendeleo na ufanisi katika utendaji wa serikali."

Taarifa inaeleza kuwa kwa kawaida, shughuli za MCC hufanyika katika msingi wa kuamini kuwa msaada unaotolewa unaleta ufanisi na matokeo makubwa zaidi ikiwa unaimarisha pia utawala bora, uhuru wa kiuchumi na uwekezaji katika watu kwa nia ya kukuza uchumi na kuondoa umasikini.

Kashfa ya Escrow
Katika taarifa yake, Bodi ya MCC haikutaja tukio lolote la rushwa linalowapa hofu katika kutekeleza mktaba huo mpya wa dola milioni 472.8. Hata hivyo, miongoni mwa matukio makubwa yaliyotikisa nchi hivi karibuni ni sakata la fedha za Akaunti ya Tegeta Escrow, ambalo lilisababisha baadhi ya mawaziri kujiuzulu na vigogo kadhaa kufikishwa mahakamani na wengine kupelekwa mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma.

Mpaka sasa mhusika mkuu katika kashfa hiyo Harbinder Singh Sethi bado hajakamatwa na kufunguliwa mashtaka na vyombo husika kama ilivyoagizwa na Bunge mwishoni mwa mwaka jana.

Aidha baadhi ya vigogo toka CCM walihusika katika kashfa hii wamepitishwa na chama hicho mapema Julai kugombea nafasi kadhaa za uongozi ikiwamo ubunge, licha ya baadhi yao kulazimishwa kujiuzulu nyadhifa zao mapema mwaka huu.

Chanzo:
Nipashe
 
Hii imeripotiwa na Nipashe gazeti la leo, kwamba marekani imeshikilia msimamo wake kwamba bado kuna rushwa kubwa Tanzania na hivyo imezuia misaada na itaendelea kuzuiwa hadi hatua zitakapochukuliwa na serekali.


Kutokana na habari hiyo= Je marekani inatutaka tuitoe ccm madarakani? Je kwakuwa hatua haziridhishi tuichague ccm kwa kumtenganisha na magufuli ili magufuli awe mwenyekiti wa ccm? Hivi tunajua kuwa watanzania tusiokuwa wana ccm unaenda kuwachagulia ccm mwenyekiti?

Hata kuandika trilioni hujui
 
Hii ni habari za kuandika ukiwa na mhemko,tulia uandike watu waelewe.
 
Hata kuandika trilioni hujui

hiyo ni bilioni moja sasa mara alfu moja kweli fisiem mnatunyima maendeleo nimeandika zero hadi nikachoka nikakuta nimeandika za tibaijuka tu kumradhi ongezea mazero hapo mkuu iwe 1000,000.000.000=du!
 
Ha ha ha
Hiyo ni tlion ama bilion iliyoandikwa hapo juu?
 
Hata kuandika trilioni hujui

Ndio ulichokiona cha msingi apo..!!
Mtu ukiwa Ccm ujue ni mzigo mkubwa kwenye hii jamii..!!
Badala yakuangalia hoja na point za msingi unaangalia trilion inaandikwa vipi...!!
Nyie ndio mnatufanya kufikia apa tulipo sasa...!!
 
Ushabiki mbaya tarakimu ya trlioni haiandikwi hivyo hatudanganyiki
 
Halafu unakuta yupo mtu tena msomi anaishabikia ccm, Hii ni moja ya aibu yetu waTz.
 
Tuiondoe ccm madarakani haraka iwezekanavyo ili kuitimisha aibu hii ya kuwa ombaomba...!!
 
...wacha serikali hii ya ccm ikose hizo pesa...maana hata wangezipata wangezipeleka kwenye uchaguzi....wacha wakose wajifunze....kama watarudi madarakani...
 
He he he haya sasa halaf bado mijitu inashabikia chama cha majambazi !

Magamba lazima tu wapige chini ili kuondokana na aibu hizi !!
 
Hii ni habari njema. as long as wamesema wamezuia tu mpaka pale tutakapojirekebisha, hiyo haina shida. mbaya ni kama wangesema tumekata kabisa.
Haya mlioko madarakani kazi kwenu kurekebisha mambo tuendelee kufaidisa na umeme wa REA huko vijijini.
 
Tunachokijua ni kuwa tumekosa fedha kwakuwa serikali iliyopo chini ya JK. Siyo adilifu.

Pia wana hofu kuwa tulivyo malofa na wapumbavu tutamchagua lowasa kuwa rais ilhali wao wana taarifa kamili za ufisadi wake!!!!!!!!
 
Sasa wanatudanganya,

Hawa Wamarekani wa Buza, kuwa wameacha kutoa hio misaada kwasababu za kipumbavu sana.
 
Sasa wanatudanganya,

Hawa Wamarekani wa Buza, kuwa wameacha kutoa hio misaada kwasababu za kipumbavu sana.
 
Back
Top Bottom