Marekebisho ya lazima, TPLB/TFF wanaipendelea Yanga au ni bahati mbaya tu?

Marekebisho ya lazima, TPLB/TFF wanaipendelea Yanga au ni bahati mbaya tu?

Ndugu,
Mnajua kulalamika sana.
Maelezo meeengi na huna research.

Hiyo match mwenyeji ni Tabora United, ndio mwenye maamuzi yakuchagua Uwanja wake.

Tuna shida sana
Kumbe una akili? Walau kuna Makolo wachache mnaojitambua.
 
Habari za uhakika kutoka TPLB naambiwa mechi ya Tabora United na Yanga inachezwa Dodoma na ile ya Tabora United na Simba ndiyo itachezwa Tabora.

Hii dhana ya upendeleo kwa Yanga itaendelea kuwatafuna TPLB/TFF aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Msimu uliopita yalikuwa haya haya ambapo Yanga hawakucheza Nyankumbu mechi yao na Geita ikachezwa KIRUMBA, Simba wakacheza mechi yao Nyankumbu.

Mechi ya Manungu kati ya Mtibwa na Yanga ilichezwa katikati ya dhana ya kwamba Yanga hawatocheza Manungu baada ya kiwanja kuonekana kibovuuuu lakini walicheza hali iliyofuta hiyo dhana, mechi hii ya Tabora pia kwamba Yanga hawatoenda Tabora na yametimia, kuweni makini watu wa mpira hatunaga siri.

Msimu huu yamejirudia yaleyale ya msimu uliopita, Yanga mechi na Tabora inachezwa Dodoma ila Tabora na Simba itachezwa Tabora, sababu ni zile zile kiwanja kinafungiwa halafu kinafunguliwa siku chache kabla ya mechi ya Yanga halafu wanasema kanuni inakataa kutumia hicho kiwanja kwahiyo Yanga wanakuwa kwenye faida.

Naambiwa kiwanja kimefunguliwa leo kwahiyo kanuni inataka baada ya siku 7 ndipo kianze kutumika, Yanga mechi yao ipo tarehe 23/12 siku 2 tu mbele, wakati ile ya Tabora na Simba ipo tarehe 29/12 siku 8 mbele ambapo ni ndani ya muda wa kikanuni.

Kumekuwa na dhana ya Yanga kupata “feva” kutoka kwa TFF/TPLB, wanaoharibu zaidi ni wapambe wanaojisifu kwamba Viongozi Wakuu Yanga na TFF wana nasaba kwahiyo wanafanya wanayotaka. Msiache dhana hii ikamea itapanda mbegu mbaya.

Siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.

Credit to: Bin Kazumari Mtipa (The voice of the voiceless)

View attachment 2849040
MBONA HUWAPA HONGERA TFF NA BODI YA LIGI KWA KUPELEKA MBELE MCHEZO WA SIMBA VS AZAM.

WAPE HONGERA BHANA.
 
Kumbe una akili? Walau kuna Makolo wachache mnaojitambua.
Dah! mambo mengine marahisi sana. Anyway, karibu Uhuru kesho.
Ushuhudie dhahama ya magoli watakayokula KMC
 
Dah! mambo mengine marahisi sana. Anyway, karibu Uhuru kesho.
Ushuhudie dhahama ya magoli watakayokula KMC
Siwezi kwenda uwanjani mara 2 kwa wiki, nachoka sana.
Nitaangalia from home…

Mechi itakuwa ngumu, KMC sio warahisi.
 
Huko ndio sijawahi kwenda na sitokaa, labda hadi aje mtoto wa mtu niende nae.
Hivihivi sikanyagi huko.
Ubaya wa Chamazi ni mdogo.
Ukitaka upate nafasi hasa kwa game za Simba au Utopolo uende mapema sana.

Kama mechi ni saa Moja basi wewe saa kumi uwepo. Otherwise hupati nafasi.

Ila ni pitch nzuri na inatoa clear vision
 
Kwani kuna faida gani Yanga asipocheza Al Hassan Mwinyi?
 
Hapa ni Serikali ya mkoa wa Tabora ndio imepush match hii ichezwe Tabora. Kanuni zingeza pindishwa, hata Yanga wangeenda.
 
Back
Top Bottom