MAREKEBISHO YA SHERIA: Sheria za Uhamiaji na Ardhi Zimefanyiwa Marekebisho. Je, Marekebisho Haya Yanatuletea Maendeleo au Hatari?

Abdul Said Naumanga

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2024
Posts
673
Reaction score
1,318
Mnamo tarehe 26 Juni 2024, Mwanasheria Mkuu aliwasilisha mswada wa Sheria ya Marekebisho Mbalimbali Na. 2 ya 2024, ambao umefanya marekebisho kadhaa ya sheria, lakini kinachovutia zaidi kwa Diaspora ni marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji na Sheria ya Ardhi.

Marekebisho haya mawili yameanzisha na kuelekeza masuala muhimu kwa Diaspora na kuendana na sera ya serikali kuhusu kukuza uchumi na kusukuma mbele ajenda ya maendeleo.​

⚖️Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji⚖️
Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji yameanzisha na kuhalalisha "HADHI MAALUM" kwa diasporas wasio raia wa Tanzania. Sheria hii kimsingi imeelezea:​
  • Maana ya Hadhi Maalum,
  • Watu wanaostahiki kupewa Hadhi Maalum,​
  • Vigezo vya ustahiki wa kupewa Hadhi Maalum,​
  • Madhumuni ambayo Hadhi Maalum itatumikia,​
  • Muda ambao Hadhi Maalum itadumu,​
  • Wategemezi wa waliopata Hadhi Maalum na haki zao,​
  • Masharti ya uhalali wa Hadhi Maalum na kufutwa kwake kwa uvunjifu wa masharti.​
⚖️Marekebisho ya Sheria ya Ardhi⚖️​
Marekebisho ya Sheria ya Ardhi yanakamilisha hadhi iliyotolewa na Sheria ya Uhamiaji na kutoa haki maalum zinazohusu umiliki wa ardhi nchini Tanzania. Marekebisho hayo yame:​
  • Ongeza kipengele cha umiliki wa ardhi kinachoitwa “Haki Maalum ya Derivative”,
  • Kueleza maana ya Haki Maalum ya Derivative,​
  • Kutoa masharti kwa watu wanaostahiki kupewa Haki Maalum ya Derivative,​
  • Kueleza haki zinazotokana na utoaji wa Haki Maalum ya Derivative na masharti yake.​
KWA MUHTASARI; marekebisho ya Sheria hizi mbili yatawezesha diasporas wasio raia wa Tanzania:​
  1. Kuingia, kukaa au kutoka nje ya Jamhuri ya Muungano,​
  2. Kuruhusu wategemezi wao kuingia, kukaa au kutoka nje ya Jamhuri ya Muungano,​
  3. Kumiliki na kutumia ardhi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa muda wa miaka 10, na uwezekano wa kuhuisha.​
Kwa maoni yangu, marekebisho haya ya sheria yanaashiria hatua muhimu katika uhusiano wa Tanzania na diaspora. Hata hivyo, mitazamo ya watu inatofautiana kuhusu athari zake. Wengine wanaridhika na hatua hii, wakiona kama sehemu ya juhudi za kuimarisha uchumi na maendeleo, huku wengine wakihofia kuwa itatoa mwanya kwa watu wasiokuwa raia kumiliki ardhi na kuishi nchini.

Tumeona kuwa marekebisho haya yanalenga kuboresha hali ya diaspora kwa kutoa hadhi maalum ambayo itawawezesha kuingia, kukaa, na kumiliki ardhi nchini. Hii inachangia katika sera ya serikali ya kukuza uchumi na maendeleo.

Kama tulivyoona, mchakato huu umeleta mitazamo tofauti, na ni muhimu kuendelea kujadili ili kuelewa vizuri athari na faida za marekebisho haya kwa jamii nzima.​
 
Wand , Bridger , Cookie au Mod mwingine yeyote, naomba title ichange iwe “MAREKEBIAHO YA SHERIA: Sheria za Uhamiaji na Ardhi Zinatarajiwa Kufanyiwa Marekebisho. Je, Marekebisho Haya Yanatuletea Maendeleo au Hatari?”​
 
Wand , Bridger , Cookie au Mod mwingine yeyote, naomba title ichange iwe “MAREKEBIAHO YA SHERIA: Sheria za Uhamiaji na Ardhi Zinatarajiwa Kufanyiwa Marekebisho. Je, Marekebisho Haya Yanatuletea Maendeleo au Hatari?”​
Mods naomba hili lifanyiwe kazi kuepusha taarifa kufika kwa namna ambaya haikukusudiwa🙏🏼​
 
Tumeisubiri kwa mda mrefu, na iwe hivyo
Sioni athari yoyote mbaya au hatari kwani wengi wana mashamba na majumba ya urithi pia huko na walijuwa imetoka hiyo

Kama anavyosema kuna wengine wanaona sio nzuri
Lakini ikumbukwe hao diaspora wana mchango mkubwa kwa Taifa pia
 
Diaspora sio watanzania, ni raia wenye asili ya Tanzania
View attachment 3055886
Aisee.
Mtu umezaliwa Tanzania, wazazi wote wawili ni Watanzania, baadaye ukaja Canada ukiwa na passport ya Tz, ukapata uraia ili tu kurahisisha mambo halafu unaambiwa wewe siyo Mtanzania!!

Ukweli ni kuwa unabaki kuwa Mtanzania halisi huku ukimiliki uraia wa mchongo wa Canada.
 
Iv inawezekana John aka silimu na bado akawa mkristo?🤔​
 
View attachment 3056332
Nadhani hapa utakua umeelewaa kwanini nilitoa mfano wa mtu kusilimu mkuu. (See Section 7)​

Cc: antimatter
Hivi vifungu navijua sana tu. Tunachohoji wengi ni uhalali wa hivi vifungu. Nadhani ulisikia ile kesi ya diaspora kuhusu uraia pacha. Na bado niko pale pale. Mfano wa dini na uraia havifanani. Dini ni kitu anachoamini mtu lakini uraia kitu ambacho hupatikana naturally. Hatukuzaliwa na dini zenu lakini tumezaliwa na uraia wetu.
 
Upo sahihi, mimi nilikua najaribu kuonyesha kuwa mtu ukichukua uraia wa nchi nyingine hata kama ni mzaliwa wa Tanzania, basi kutokana na sheria zetu, si mtanzania tena. Hii ndo ilikua maana yangu​
 
Upo sahihi, mimi nilikua najaribu kuonyesha kuwa mtu ukichukua uraia wa nchi nyingine hata kama ni mzaliwa wa Tanzania, basi kutokana na sheria zetu, si mtanzania tena. Hii ndo ilikua maana yangu​
Haya mabadiliko ndiyo yanaandaliwa siyo? I mean bado hayajapelekwa bungeni na kupishwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…