Sijapewa username bado
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,775
- 2,891
Leo Februari 2, 2026, nikiwa katika harakati zangu, nilipita Stendi ya Daladala Mbezi Luis maarufu Mbezi Mwisho na kushuhudia ukarabati wa vyoo ukiendelea.
Awali, niliwahi kuona andiko hapa JF likieleza changamoto za miundombinu hiyo, hususan baada ya uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, 2025.
Napongeza mamlaka husika kwa kuchukua hatua ya uwajibikaji kuanza kuboresha miundombinu hiyo, hatua ambayo natarajia itasaidia kurejesha huduma hii muhimu ya kijamii katika mazingira rafiki.
Hata hivyo, nitoe wito kwa mamlaka zinazohusika kutumia fursa hii kufanya maboresho zaidi, hasa kwa kuweka miundombinu rafiki ya maji katika maeneo ya vyoo.
Hili ni muhimu kwani awali kulikuwapo changamoto ya upatikanaji wa maji, hali iliyolazimu watumiaji kuchota maji kwenye pipa na kuyajaza kwenye ndoo ili kuweza kutumia vyoo.
Choo kilivyokuwa awali ~ Manispaa ya Ubungo fungeni vyoo vya Mbezi Kituoni ni hatarishi kwa afya, havifai kabisa kutumika