SI KWELI PreGE2025 Maria Sarungi adai Mpina ni dikteta, hafai kuonewa huruma

SI KWELI PreGE2025 Maria Sarungi adai Mpina ni dikteta, hafai kuonewa huruma

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
photo_2025-07-03_10-25-47.jpg
 
Tunachokijua
Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.

Luhaga Mpina ni mbunge wa jimbo la Kisesa kwa miaka ishirini (20) sasa ambaye amewahi kuwa waziri wa mifugo na uvuvi mwaka 2017 hadi 2020.

Mwezi Juni 17, 2025, ulifanyika mkutano wa hadhara wilayani Meatu, mkoa wa Simiyu, ikiwa ni sehemu ya ziara ya Rais Samia, ambap moja kati ya viongozi waliopata nafasi ya kuzungumza kabla ya hotuba ya Rais, alikuwa ni Mpina ambaye pamoja na mambo mengine aliwasilisha ujumbe kwa Rais Samia kuwa jimbo lake bado linamdai, na kwamba maeneo mengine yanayodai hayamdai, fedha zao zihamishiwe Kisesa kwani wana mipango mingiya maendeleo.


Chapisho linalosambazwa mtandaoni
Katika mtandao wa Facebook lipo chapisho lenye utambulisho wa Jambo TV, likinukuu andiko linaloonekana kuchapishwa kwenye mtandao wa X kuwa Maria Sarungi adai Mpina ni dikteta, hafai kuonewa huruma.


Je, ni upi uhalisia wa chapisho hilo?
Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani andiko lililonukuliwa halikuchapishwa na Maria, bali ni la kutengenezwa na wapotoshaji.

Aidha chapisho lililotumika kusambaza taarifa hiyo si la kweli ni la kughushi, kwani halijachapishwa katika kurasa rasmi za Jambo TV.

Kumbuka wapotoshaji wanaweza kutumia utambulisho wa vyanzo vya taarifa vinavyoaminiwa kusambaza taarifa zisizo za kweli, hivyo ni muhimu kuthibitisha uhalisia wa Taarifa kabla ya kuamini na kusambaza.​
Back
Top Bottom