MARIA SARUNGI AMEANDIKA KWENYE UKURASA WAKE WA X KUWA GODBLESS LEMA APOKEA BILIONI 4 KUISAMBARATISHA CHADEMA.
"🚨‼️Kaka yangu GODBLESS LEMA ametuchoma wapigania Haki.🚨‼️ Wakati tunalilia haki, tunapambana kwa ajili ya Mdude, yeye anapokea bilioni 4 kwa ajili ya kuizamisha CHADEMA polepole. Anawaumiza waliompigania, anahujumu harakati, halafu anapanga kuondoka nchini kujiweka salama huku akituacha kwenye mateso. Huu siyo usaliti wa kawaida—ni usaliti wa kihaini. #FreeMdude #UsalitiMtupu #Tunaona"
🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚🔚
Ameandika Maria Sarungi kwenye Ukurasa wake wa X zamani Twitter.

- Tunachokijua
- Godbless Lema ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini. Lema amekuwa ni moja kati ya viongozi wa chama hicho ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kufanya uchechemuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu demokrasia pamoja na kukosoa utendaji wa serikali, hasa kupitia ukurasa wake wa X.
Aidha Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.
Madai
Kumekuwapo na Chapisho linalosambazwa mtandaoni linalodaiwa kuchapishwa na Maria Sarungi kwenye mtandao wa X kuwa Godbless Lema amepokea bilioni 4 kwa ajili ya kuizamisha CHADEMA.
Uhalisia
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) ulibaini kuwa Chapisho hilo si la kweli ni la kutengenezwa na wapotoshaji kwani halijachapishwa na Maria kwenye ukurasa wake wa X.
Vile vile chapisho hilo lina mapungufu kadhaa yanayodhihirisha kuwa ni la kutengenezwa kwani linatofautiana na machapisho kutoka katika mtandao wa 'X'. Moja ya mapungufu hayo ni pamoja na muonekano wa picha zilizotumika ambazo muundo wake katika sehemu zenye kona ni tofauti na machapisho kutoka X, kwani huwa na muundo wa duara na si kona yenye nyuzi 90.