SI KWELI PreGE2025 Maria Sarungi ameandika kwenye ukurasa wake wa x kuwa Godbless Lema apokea bilioni 4 kuisambaratisha Chadema

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
MARIA SARUNGI AMEANDIKA KWENYE UKURASA WAKE WA X KUWA GODBLESS LEMA APOKEA BILIONI 4 KUISAMBARATISHA CHADEMA.

"๐Ÿšจโ€ผ๏ธKaka yangu GODBLESS LEMA ametuchoma wapigania Haki.๐Ÿšจโ€ผ๏ธ Wakati tunalilia haki, tunapambana kwa ajili ya Mdude, yeye anapokea bilioni 4 kwa ajili ya kuizamisha CHADEMA polepole. Anawaumiza waliompigania, anahujumu harakati, halafu anapanga kuondoka nchini kujiweka salama huku akituacha kwenye mateso. Huu siyo usaliti wa kawaidaโ€”ni usaliti wa kihaini. #FreeMdude #UsalitiMtupu #Tunaona"
๐Ÿ”š๐Ÿ”š๐Ÿ”š๐Ÿ”š๐Ÿ”š๐Ÿ”š๐Ÿ”š๐Ÿ”š๐Ÿ”š

Ameandika Maria Sarungi kwenye Ukurasa wake wa X zamani Twitter.
 
Tunachokijua
Godbless Lema ni mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA ambaye aliwahi kuwa mwenyekiti wa chama hicho kanda ya Kaskazini. Lema amekuwa ni moja kati ya viongozi wa chama hicho ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kufanya uchechemuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu demokrasia pamoja na kukosoa utendaji wa serikali, hasa kupitia ukurasa wake wa X.

Aidha Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.


Madai

Kumekuwapo na Chapisho linalosambazwa mtandaoni linalodaiwa kuchapishwa na Maria Sarungi kwenye mtandao wa X kuwa Godbless Lema amepokea bilioni 4 kwa ajili ya kuizamisha CHADEMA.

Uhalisia

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) ulibaini kuwa Chapisho hilo si la kweli ni la kutengenezwa na wapotoshaji kwani halijachapishwa na Maria kwenye ukurasa wake wa X.

Vile vile chapisho hilo lina mapungufu kadhaa yanayodhihirisha kuwa ni la kutengenezwa kwani linatofautiana na machapisho kutoka katika mtandao wa 'X'. Moja ya mapungufu hayo ni pamoja na muonekano wa picha zilizotumika ambazo muundo wake katika sehemu zenye kona ni tofauti na machapisho kutoka X, kwani huwa na muundo wa duara na si kona yenye nyuzi 90.​
Hope hii ni trash tu kama zingine..

Kwa kuwa sisiemu wananunulika basi mnajua kila ntu ana bei ๐Ÿšฎ ๐Ÿšฎ ๐Ÿšฎ
 
Maria hiyo siyo account yake. Japo na wewe umetumwa na CCM
 

Thread takataka Kama hii ambazo hazina Ushahidi ni vyema Sana Mods wa JF mkazifuta.
 
Sawa bibie tumekuelewa.
 
FAKE NEWS, FAKE NEWS, FAKE NEWS, CCM WANADHANI WATANZANIA NI WAJINGA. MAFALA NINYI CCM NA SERIKALI YENU
 
Kuna mbunge wa CCM mambo ya nchi anazungumzia Tiktok kuondolewa na hawa wajinga Fake news
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ