SI KWELI PreGE2025 Maria Sarungi amesema CHADEMA imepotea njia, hakuna muelekeo, chama kimepotea

SI KWELI PreGE2025 Maria Sarungi amesema CHADEMA imepotea njia, hakuna muelekeo, chama kimepotea

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
photo_2025-07-03_10-19-51.jpg
 
Tunachokijua
Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.

Siku za karibuni kumekuwapo na taarifa nyingi zisizo za kweli zikisambazwa mtandaoni kumhusu Maria Sarungi akihusishwa na CHADEMA, pamoja na viongozi wa chama hicho. Rejea hapa, hapa na hapa.

Baadhi ya watumiaji wa mtandao wa Facebook wamekuwa wakisambaza taarifa iliyotumia grafiki yenye utambulisho wa Jambo TV, iliyonukuu andiko linaloonekana kuchapishwa na Maria Sarungi kwenye mtandao wa X, kuwa amesema CHADEMA imepotea njia, hakuna muelekeo, chama kimepotea.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani andiko lililonukuliwa halikuchapishwa na Maria Sarungi bali ni la kutengenezwa na wapotoshaji.

Vilevile Grafiki iliyotumia utambulisho wa Jambo TV na kunukuu Ujumbe huo ni ya Kughushi kwani televisheni hiyo ya mtandaoni haikuchapisha katika kurasa zake.​
Back
Top Bottom