- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
- Tunachokijua
- Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.
Taarifa inayohusishwa na Maria Sarungi
Ipo taarifa inayosambazwa mtandaoni ikitumia utambulisho wa grafiki za Millard Ayo, Nipashe na Mwananchi ikinukuu Ujumbe unaodaiwa kuandikwa na Maria Sarungi kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X ukisema,
'Kama ni kufa, CHADEMA ilishakufa kitambo !! Heche ameshindwa kuunganisha chama, Mnyika yupo tu kimya nyumbani, Lema amekimbia kwa mke wake yupo Canada. Kwa lugha nyepesi CHADEMA si chama kikuu cha upinzani, ni chama cha nyongeza tu'
Uhalisia wa taarifa hiyo
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key Word Search) umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani ujumbe ulionukuliwa haujaandikwa na Maria Sarungi, bali ni wa kutengenezwa na wapotoshaji.
Aidha grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kughushi kwani haijachapishwa na vyombo hivyo (Mwananchi, Nipashe na Millard Ayo) kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.