SI KWELI PreGE2025 Maria Sarungi amesema CHADEMA inazidi kusambaratika na kufa

SI KWELI PreGE2025 Maria Sarungi amesema CHADEMA inazidi kusambaratika na kufa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
MARIASARUNGI24JUN2025.jpg

SARUNGI24JUN2025.jpg
 
Tunachokijua
Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.

John Heche ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambaye alichaguliwa kutumikia nafasi hiyo Januari 21, 2025 akichukua nafasi ya aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Tundu Lissu ambaye alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama hicho aliyeko mahabusu akituhumiwa kwa kesi ya uhaini na uchochezi ambapo kesi yake inatarajiwa kuendelea tarehe 02 Juni, 2025.

Aidha John Mnyika aliteuliwa na kamati kuu ya chama hicho kukaimu nafasi ya Katibu baada ya ofisi ya msajili kutengua uteuzi wa wajumbe nane wa sekretarieti na kamati kuu walioteuliwa na Tundu Lissu.


Taarifa inayomuhusisha Maria, Mnyika na Heche.

Ipo taarifa inayosambazwa mtandaoni ikinukuu andiko linaloonekana kuchapishwa na Maria Sarungi kuwa "harakati za Mnyika na Heche kutaka CHADEMA ishiriki uchaguzi, ni usaliti kwa msimamo wa chama" huku machapisho yenye utambulisho wa Jambo TV na Mwananchi yakitumika kusambaza taarifa hiyo.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli, ni ya kutengenezwa kwani andiko hilo halikuchapishwa na Maria Sarungi kwenye ukurasa wake wa X.

Vilevile machapisho yaliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani hayajachapishwa na Mwananchi wala Jambo TV. Hata hivyo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii Maria Sarungi amekanusha taarifa hiyo na kwamba si ya kweli​
Acha apige udalali

Akisema hivyo zole pesa za akina george sorrows atapataje?
 
Back
Top Bottom