- Source #1
- View Source #1
kumekuwa na chapisho linalo samba kwenye mitandao ya kijamii hususani facebook linaeleza kuwa Mwanaharakati Maria Sarungi amekamtwa na jeshi la polisi nchini kenya huku ikieleza kuwa taarifa hiyo imechapishwa na godbless Lema huku x pia chombo cha Habari cha Jambo tv kuchapisha huko X
Taarifa hizo sio sahihi kwani hazina uhalisia wowote na hazijachapishwa sehemu yoyote ile.
Taarifa hizo sio sahihi kwani hazina uhalisia wowote na hazijachapishwa sehemu yoyote ile.
- Tunachokijua
- Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X.
Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook wamekuwa wakisambaza taarifa kuwa Maria Sarungi anashikiliwa na jeshii la polisi nchini Kenya akituhumiwa kwa utakatishaji fedha
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
JamiiCheck imebaini kuwa machapisho ya Jambo TV na KTN News yanayotumika kusambaza taarifa hiyo si ya kweli bali ni ya kutengenezwa na wapotoshaji kwani hayajachapishwa na vyombo hivyo.
Vilevile andiko lililonukuliwa, likidaiwa kuchapishwa na Godbless Lema kwenye mtandao wa X ni la kutengenezwa kwani halikuchapishwa na Lema katika ukurasa wake.