SI KWELI Maria Sarungi: CHADEMA imechoka

SI KWELI Maria Sarungi: CHADEMA imechoka

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu ni kweli Maria alisema kuwa Chadema imechoka?

si kweli (8).jpg
 
Tunachokijua
Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, Maria amekuwa akijihusisha na masuala mbalimbali ya siasa kwa kipindi kirefu sasa, amekuwa akizifanya harakati zake katika mitandao ya kijamii ikiwemo X zamani ikijulikana kama twitter ambapo amejizolea umaarufu mkubwa.

CHADEMA ni chama cha siasa nchini Tanzania kwa kirefu kinajulikana kama Chama cha Demokrasia na Maendeleo ambacho kimewahi kuwa chama kikuu cha upinzani Tanzania. Zimekuwepo baadhi ya taarifa mtandaoni zilizokuwa zikidai kuwa hakuna mahusiano mazuri kati ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na Makamu mwenyekiti wake Tundu Lissu.

Viongozi hao walifanya mkutano na waandishi wa habari tarehe 10/12/2024 ambapo walizungumza vitu mbalimbali ikiwemo hali ya uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa 2024 pamoja na uhusiano baina yao na walieleza kuwa kutofautiana mawazo katika chama ni jambo la kawaida.

JamiiCheck imefuatilia madai ya grafiki inayosambaa mitandaoni ambayo imehifadhiwa hapa ikiwa na nembo ya Jamiiforums huku ikiwa na maneno yanayosomeka "MARIA SARUNGI ADAI, CHADEMA IMECHOKA" ikiwa imeambatana na screenshot inayoonesha ukurasa wa Maria Sarungi ndiye aliyasema maneno. Ufuatiliaji wa kimtandao umebaini kuwa madai hayo si ya kweli na hayajachapishwa na JamiiForums.

JamiiCheck imefuatilia katika ukurasa wa Maria katika mtandao wa wa X ambapo ndipo inadaiwa alichapisha maneno hayo na kukuta kuwa hakuna maneno au taarifa inayofanana na hiyo. Lakini pia grafiki inayoonekana ni ya JamiiForums si sawa na grafiki zinazotumiwa na JamiiForums lakini pia katika tarehe hiyo wanayodai 10/12/2024 JamiiForums haikutoa wala kuchapisha taarifa yenye kufanana na hiyo.
Back
Top Bottom